PostGE2025 Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia za Uchaguzi mwaka 2025

PostGE2025 Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia za Uchaguzi mwaka 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Tume ya Jaji Chande imeleta kizaazaa! Je, na hii nayo tutegemee nini? Hizo hela zinazotumika hazina matumizi muhimu na ya msingi?
Kama ni Tume ya Rais hilo ni dodoki la kumsafisha Samia na genge lake, hapo suala la mauaji ya watu zaidi ya 10,000 halizungumziwi tena bali kinachozungumziwa ni watu waliofanya ghasia ambao awali walikamatwa na kushtakiwa kisha yeye akawasamehe.Samia anachofanya ni kupoteza muda akiamini Watanganyika watasahau jinsi watoto wao walivyouwawa na polisi wake. Hatudanganyiki.
 
Acha propaganda mkuu, CCM ni chama makini na well ahead of time, kina wanachama na ofisi mpaka nje ya nchi kwa taarifa yako
Kuwa ni ofisi ndio ubora? Chama makini cha siasa hakitegemei mbeleko ya vyombo vya dola. Siku vyombo vya dola vinasimamia sheria hiyo ccm utaenda kuishi kaburi moja na KANU ya Kenya. Na uzuri siku hiyo haiko mbali.
 
Kuchunguza chanzo na kilichotokea
Hii ya pili ni Kuchunguza jinai kwa polisi walio ua watu kwa makosa,
Kwa lugha ya kiingereza
Tume ya kwanza ili inquiry ya Kuchunguza what happened
Hii ya pili ni Kuchunguza criminal liability
P
"...kuchunguza polisi walio ua watu kwa makosa..."

Nimemsikiliza mzee Warioba kwenye mahojiano yake ya juzi na mzee Ulimwengu;

Kwa nilivyomuelewa hakuna Polisi au mwana usalama yoyote atakayetiwa hatiani kwasababu hakuna ushahidi utakaopatikana zaidi ya ushahidi wa maneno labda na maganda la risasi tu;

Hizi picha za huku mitandaoni wameshatwambia nyingine ni za gaza na nyingine ni AI. Hadi hapa tatu bila tayari

Kingine naamini kwa ubobevu wako na weredi umeandika hii sentensi kimtego ila haumaanishi ulichokiandika (umeandika code)

Hisia zangu zinaniambia kuwa kazi kubwa ya hii tume itakuwa "kutengeneza" majina ya wale waliotajwa kama waandaaji wa vurugu, waendesha mafunzo na waliofadhili kwa kutoa hela kwa waandamanaji
 
Rais Samia Suluhu amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani, Shabani Ally Lila, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya ghasia ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.


Soma Pia: Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi 2025

Tume hiyo inalenga kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani ili kuchukua hatua stahiki na kuimarisha usalama wa taifa, huku Jaji Lila akisaidiana na Majaji Wastaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Gad John Mjemmas, Awadh Mohamed Bawazir na Aishieli Nelson Sumari.

====

TUME YA UCHUNGUZI WA KIJINAI WA MATUKIO YA GHASIA YA WAKATI NA BAADA YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025

Katika kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Yaliyotokea Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025 na kwa kuzingatia mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia ya Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Aidha, Mhe. Shabani Ally Lila, Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameteuliwa kuwa Kamishna na Mwenyekiti wa Tume na wafuatao wameteuliwa kuwa Makamishna wa Tume hiyo:-

(i) Mhe. Gad John Mjemmas - Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania;
(ii) Mhe. Awadh Mohamed Bawazir Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania; na
(iii) Mhe. Aishieli Nelson Sumari Tanzania. Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Ana tapatapa wewe mwache aondoke kitini ndiyo atajua uovu wake na wahuni wenzie
 
wameuliwa Christians kwa wingi na hata wanajitapa kabisa kwamba hakuna muslims aliouliwa, halafu jaji kateuliwa ni muslm, na zilikuwa ni targeted killings, hizi sarakasi zote zina mwisho ...
Mkuu Kija, wee Kijakazi, usituletee hapa maudini yako na hiyo misalaba yako, uteuzi unaangalia sifa ya mtu sio dini ya mtu!.
P
 
Samia Suluhu ni kiongozi wa siasa za ndani. Anaturudisha nyuma sana. Hizi kazi zilifanywa na Mwalimu na comrades wengine. Hii nchi na Afrika kwa ujumla umoja na mshikama tuko mbali sana.
Sasa hivi tunataka viongozi watakaopigania interesting zetu mbele ya wazungu.
Hizi tume za kuchunguza mambo ya Mbagala ni matumizi mabaya ya pesa zilizopatikana kutoka kwenye kodi kubwa sana wanazotozwa watanzania.
Kama taifa kubwa kama Saudi Arabia wanapata 50% tu ya rasilimali zake, je wakina sisi tunapewa ngapi? Tunataka viongozi ambao watakuwa wazi kwenye mambo kama hayo ili watoto wetu wasije kudharauliwa na watu wa magharibi kama sisi.
Wakati umefika, wale wasio na uwezo wa kuongoza Afrika ya kisasa au nia njema kwa waafrika wakae pembeni tafadhari.
 
Kurukaruka kwa maharage ndiyo kuiva kwake ,waache waruke ruke tu ,Samia anataka kuwalinda wasaidizi wake IGP.GDIS ,CDF ila bila kuwatoa hao kafara ataingia yeye kitanzini.
Hao na wengine wengi awawezi kutoboa, huu ushenzi waliofanya ni mkubwa kupita kiasi ni swala la muda tu ..kundi kubwa sana linakwenda kulipa kwa ushenzi waliofanyia nchi ..na saa zinakimbia hatari
 
Rais Samia Suluhu amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani, Shabani Ally Lila, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya ghasia ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.


Soma Pia: Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi 2025

Tume hiyo inalenga kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani ili kuchukua hatua stahiki na kuimarisha usalama wa taifa, huku Jaji Lila akisaidiana na Majaji Wastaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Gad John Mjemmas, Awadh Mohamed Bawazir na Aishieli Nelson Sumari.

====

TUME YA UCHUNGUZI WA KIJINAI WA MATUKIO YA GHASIA YA WAKATI NA BAADA YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025

Katika kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Yaliyotokea Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025 na kwa kuzingatia mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia ya Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Aidha, Mhe. Shabani Ally Lila, Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameteuliwa kuwa Kamishna na Mwenyekiti wa Tume na wafuatao wameteuliwa kuwa Makamishna wa Tume hiyo:-

(i) Mhe. Gad John Mjemmas - Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania;
(ii) Mhe. Awadh Mohamed Bawazir Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania; na
(iii) Mhe. Aishieli Nelson Sumari Tanzania. Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Hizi ni hatua za awali kuelekea kufanya maridhiano, ila shida ripoti zinakuja na uongo mwingi, wananchi wamepoteza imani na serikali yao, wamejifunza vingi kupitia matukio ya oct29.

Huyu ile falsafa yake ni bure kabisa hana uwezo wa kuitekeleza akili zake ni ndogo sana☹️
 
Kuchunguza chanzo na kilichotokea
Hii ya pili ni Kuchunguza jinai kwa polisi walio ua watu kwa makosa,
Kwa lugha ya kiingereza
Tume ya kwanza ili inquiry ya Kuchunguza what happened
Hii ya pili ni Kuchunguza criminal liability
P
Ni mental gymnastics tu hizo.
 
Kuchunguza chanzo na kilichotokea
Hii ya pili ni Kuchunguza jinai kwa polisi walio ua watu kwa makosa,
Kwa lugha ya kiingereza
Tume ya kwanza ili inquiry ya Kuchunguza what happened
Hii ya pili ni Kuchunguza criminal liability
P
Kwa akili ndogo tu ya kawaida nani ataweza kutoa ushahidi ili Polisi walioua watu wawe liable?

Mfano lile tukio kule Mwanza watu kumi na tano walikuwa wanaangalia mpira wakapigwa risasi ndani ya banda la mpira.

Acha ushabiki.
 
Haki itendeke ,kuua watu kisa madaraka moja kwa moja The Hague ,SSH hakuchaguliwa na wananchi bali amechaguliwa na TUME(Sisi tumeona kulikuwa hakuna uchaguzi na Hata Jaji warioba amesema wazi).

SSH kulinda heshima aachie ngazi ,mali alizochuma ni nyingi sana zinatosha kula wanae ,wajukuu na vitukuu ya nini kung'ang'ania madarka?
Haiwezi kuachia madaraka yule. Wanawake Sana roho ngumu Sana na wanavumilia maumivu na stress kuliko wanaume
 
Sijui akili zake zinamtuma nn but kabla hata ajaanza ashafeli...HAKUNA MWANANCHI ANAWEZA KUMWAMINI TENA...
angalau kidoogo angeruhusu tume za nje hizo ndo hata azipange kumsafisha...za ndani anataka kuleta balaa kubwa zaid maana akiwataja watu nje na police na majesh yake watu hawez mwelewa
 
TOKA MAKTABA
Mapito ya waheshimiwa majaji

Mhe.Jaji (Mstaafu) Awadh Bawazir​

Awadh Bawazir photo

Mhe.Jaji (Mstaafu) Awadh Bawazir​

Mwenyekiti wa Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma PPAA


Retired Judge Gad John Mjemmas


The President of the United Republic of Tanzania, Her Excellency Dr. Samia Suluhu Hassan, has appointed Retired Retired Judge Gad John Mjemmas as the Chairperson of the Tax Revenue Appeals Tribunal (TRAT)


MAAMUZI YA KESI MUHIMU KABLA YA MAJAJI KUSTAAFU :
..


​

Panafrican Energy T. Ltd vs Commissioner General Tra (Civil Appeal 121 of 2018) [2019] TZCA 170 (31 May 2019) - [2019] TZCA 170​

​
TOKA MAKTABA:

09 October 2018
Na Charles Ndagulla, Moshi

Jaji Sumari majaribuni tena Moshi​

1779120869749.jpeg

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Aishiel Sumari, ameandamwa tena na wananchi wanaokataa asisikilize mashauri yaliyo mbele yake kwa madai kuwa hawana imani naye.
Hatua hii inakuja huku kukiwa na taarifa kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Moshi kuwa jaji huyo yuko katika maandalizi ya kustaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria.
Ally Hussein Mitta, ambaye ni mdaawa katika shauri Na. 41/2017 amemwandikia barua Jaji Sumari akimtaka ajitoe kusikiza shauri hilo lililopangwa kusikilizwa keshokutwa.
Akizungumza na JAMHURI mjini hapa, Mitta amesema msingi wa kumkataa Jaji Sumari kusikiliza shauri hilo ni kutokana na kuwepo kwa mazingira yanayowatia shaka.
Shauri hilo lilifunguliwa mahakamani hapo na Ramadhan Mohamed Mitti, anayepinga uamuzi wa Baraza la Ardhi la Wilaya ya Moshi, uliompa ushindi Ally kuwa ndiye mmiliki halali wa nyumba iliyopo kwenye kiwanja namba 40, kitalu E, Section III, iliyopo Mtaa wa Selous, Manispaa ya Moshi.

Uamuzi huo ulitolewa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza, Mussa Mahelela, Oktoba 31, 2013 na tangu wakati huo Ramadhan hakuwahi kuomba kukata rufaa kwa zaidi ya miaka mitatu hadi alipoomba kufanya hivyo mwaka jana.
Kwa mujibu wa barua aliyomwandikia Jaji Mkuu wa Tanzania ya Agosti 20, mwaka huu, Ally anadai kuwa shauri hilo linasikilizwa kinyume cha sheria za nchi na taratibu za mahakama.
“Mheshimiwa Jaji Mkuu, baada ya shauri kuanza kusikilizwa na Mahakama Kuu Kanda ya Moshi mbele ya Mheshimiwa Jaji Sumari, tuna ushahidi kuwa kuna mazingira ya ukandamizaji [yanayoendelea],” inasema barua hiyo ambayo nakala yake tunayo.

Ally anadai katika barua hiyo kuwa tangu shauri hilo litolewe uamuzi na Baraza la Ardhi la Wilaya mwaka 2013, Ramadhan hajawahi kuomba mapitio ya hukumu hiyo ili aweze kukata rufaa, huku akisisitiza shauri lililopo mbele ya Jaji Sumari linakosa uhalali wa kisheria wa kuendelea kusikilizwa.
Katika shauri hilo, Ramadhan ambaye ni ndugu yake Ally, anaiomba mahakama kubatilisha uamuzi wa Baraza la Ardhi na kumtambua yeye kama mmiliki halali wa nyumba hiyo.
Kwa mantiki hiyo, Ally anamwomba Jaji Mkuu kutumia mamlaka yake kuwachukulia hatua wote wanaoendelea kusikiliza shauri hilo akidai kuwa lilitolewa uamuzi na mhusika hakuwahi kuomba mapitio ndani ya muda wa siku 90 kama sheria inavyotaka.

Mapema mwaka jana, Ramadhan aliwasilisha maombi Mahakama Kuu ya kukata rufaa nje ya muda unaokubalika kisheria na maombi hayo yalikubaliwa, hivyo kufunguliwa shauri hilo namba 41/2017.
Awali shauri hilo lilikuwa mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Patricia Fikirini, kabla ya Ally kumkataa kwa kile alichodai jaji huyo alikataa kuidhinisha malipo ya wakili wake ya Sh milioni tatu na kuidhinisha kiasi cha Sh 1,040,000.
Mbali na barua hiyo, Ally pia amemwandikia barua Jaji Sumari mwenyewe ya Agosti 31, mwaka huu ambayo Gazeti la JAMAHURI linayo nakala yake, akimtaka ajitoe kusikiliza shauri hilo kwa kile anachodai hana imani naye.
Nakala ya barua hiyo imesambazwa kwenye taasisi 11, ikiwamo Ofisi ya Rais, Jaji Kiongozi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Waziri wa Sheria na Katiba, Tume ya Haki za Binadamu, Mkurugenzi wa Takukuru na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Frank Mahimbali, hakupatikana kuzungumzia barua hizo zinazomtaka Jaji Sumari kujitoa kusikiliza shauri hilo.
Tukio hili ni la pili kwa Jaji Sumari kuingia majaribuni ambapo hivi karibuni alipokwa jalada la kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Scolastica, Humphrey Makundi (16).
Hatua hiyo ilitokana na familia ya mwanafunzi huyo kumwandikia barua Jaji Kiongozi kulalamika kuwa haki isingetendeka katika shauri hilo baada ya Jaji Sumari kudaiwa kujipangia shauri hilo licha ya katazo la Jaji Kiongozi.
Kwa sasa jalada hilo liko chini ya Jaji Huruma Songoro, ambaye amewahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara, huku Wakili Mwandamizi wa Serikali, Abdallah Chavula, akiwa chini ya Wakili Mkuu wa Serikali, Joseph Pande.
Shauri hilo la jinai namba 48/2018 linawakabili washtakiwa watatu akiwamo Mkurugenzi wa Shule hiyo, Edward Shayo, aliyekuwa mlinzi wa shule hiyo, Hamis Chacha, ambaye ni mshtakiwa wa kwanza na Laban Nabiswa, aliyekuwa Mwalimu wa Nidhamu ambaye ni mshtakiwa wa tatu.

Kutokana na malalamiko hayo, Jaji Kiongozi, Eliezer Feleshi, alimtaka Jaji Sumari amjulishe mara tu kesi hiyo itakapofikia hatua ya ‘plea taking’ na ‘PH’ ili ateue jaji wa kuisikiliza, lakini kinyume cha maelekezo ya Jaji Kiongozi, Sumari alijipangia kuisikiliza kesi hiyo Agosti 27, mwaka huu lakini Jaji Kiongozi akampoka jalada hilo.
Barua hiyo ya Jaji Kiongozi ya Julai 31, mwaka huu yenye Kumb. Na. HA. 59/190/02 ‘C’/3, iliandikwa na kusainiwa na D. B. Ndunguru, ambaye ni Katibu wa Jaji Kiongozi na nakala ya barua hiyo kunakiliwa kwa Jackson Makundi ambaye ni baba mzazi wa marehemu Humphrey Makundi
 
Kuchunguza chanzo na kilichotokea
Hii ya pili ni Kuchunguza jinai kwa polisi walio ua watu kwa makosa,
Kwa lugha ya kiingereza
Tume ya kwanza ili inquiry ya Kuchunguza what happened
Hii ya pili ni Kuchunguza criminal liability
P
Unajua maana ya criminal liability?

Hiyo ni kazi ya Polisi wa Kitengo cha Upelelezi wa makosa ya Jinai (CID) chini ya Sheria ya mwenendo wa Makosa ya jinai (CPA).

Sasa kama tunahitaji majaji wastaafu wakae chini kuchunguza jinai ya polisi walioua, maana yake Jeshi la Polisi limefunga ofisi au limejifuta lenyewe?

Au ndio ile mtindo wa nyani haoni amfanyalo mwenzake?
 
Back
Top Bottom