PostGE2025 Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Novemba 18, 2025 ameunda Tume huru ya kufanya uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa amani yaliyotokea nchini wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Jumatano Oktoba 29, 2025.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, imeeleza kuwa Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu Mstaafu wa mahakama ya Tanzania ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo.

Soma pia: Rais Samia aunda Tume Huru ya Uchunguzi wa matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi 2025



Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Wajumbe watakaofanya kazi na Jaji mstaafu Chande ni pamoja na Prof. Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Balozi Ombeni Yohana Sefue, Mwanadiplomasia na Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu na Balozi Radhia Msuya, Mwanadiplomasia na Balozi Mstaafu.

Wengine ni Balozi Luteni Generali Paul Meela, Mwanadiplomasia na Balozi mstaafu, Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu IGP Said Ally Mwema, Balozi David Kapya, Mwanadiplomasia na Balozi mstaafu na Dkt. Stergomena Lawrence Tax, Katibu Mtendaji mstaafu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)
 
Tume huru halafu ameiteua yeye mwenyewe! Au ni kwamba yeye hahusiki kwenye kusababisha hizo vurugu za tarehe 29 Oktoba? Haya mambo ya kuwaona wananchi hawana akili ya kufikiri na kuchanganua mambo, ifikie wakati na yenyewe yaachwe sasa.
 
Tume ya watu wake na Kikwete...hii si ndiyo kama tume huru ya uchaguzi? Nani anamshauri huyu mama afanye hizi sarakasi?
 
Hadidu za rejea ziwe hizi zifuatazo maana ndizo zilizo trigger yote haya.
1. Utekaji.
2. Kesi za mchongo.
3.Wizi wa kura.
4.ukosefu wa haki.
Na mengineyo
 
Tume huru
Kila siku amekua anaunda Tume , na zimekua zikimshauri vizuri tu ila amekua chura kiziwi.
Hii pia itakula kodi zetu itaendoka bila majibu.
Kifupi yeye aachie ngazi na tume huru iundwe na AU AU UN.
 
Hiyo ni sawa na kujitekenya kisha unacheka mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…