Bani Israel
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 2,284
- 4,595
Hii tume itachunguza ni nani na nani waliratibu maandamano ili wapewe mzigo wa vifo na katu haitachunguza waliuwa waandamanaji.
Hawa wanafikiri watanzania wako enzi za TANU na RTD ndio chombo pekee cha kupika propaganda za Lumumba.Kumbe na wewe umegundua hapo wameficha....
Kosa la kiufundi!!!!Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax
Tume ipi, ile aliyounda kuhusu mauaji ya Ali Kibao na kutaka ripoti haraka una majibu yake? Ni hivi, tarehe 9 tunarudi barabarani, hiyo tume ya ccm ikampelekee majibu anayoyataka yeye, hatuna muda na hayo maigizo yake. Yeye ni rais aliyetangazwa kwa mtutu wa bunduki, na hana uhalali wa umma.Subiri tume ilete majibu acha kuwalisha maneno.
Hasira hasara. Kama umehusika mkono wa sheria utakupitia.Tume ipi, ile aliyounda kuhusu mauaji ya Ali Kibao na kutaka ripoti haraka una majibu yake? Ni hivi, tarehe 9 tunarudi barabarani, hiyo tume ya ccm ikampelekee majibu anayoyataka yeye, hatuna muda na hayo maigizo yake. Yeye ni rais aliyetangazwa kwa mtutu wa bunduki, na hana uhalali wa umma.
No, actually ni hivi: wewe utaundaje tume ya kuchunguza mauaji uliyoyaagiza?Utamuwekaje aliyekuwa waziri wako wa ulinzi katika tume ya kuchunguza matendo ya vyombo vyako vya ulinzi?
Huyu mama hayuko serious
Ni matusi makubwa kwa ndugu wa marehemu waliouawa kwa risasi wakidai nchi ya haki
Huyu bibi ana dharau kupita dharau yenyeweUongozi uliopita uliokuwa unatuhumiwa kwa mambo kama ya sasa na kudhoofisha mifumo ya haki ndio waje kufanya uchunguzi wa mauji haya yaliyofanyika kwenye serikali ya sasa (yako)? Juma, Tax, Mwema ndio the best you could do kweli?
Ripoti iliyotolewa na Jaji Chande juu ya ukatili wa polisi imefanyiwa nini mpaka leo? Rais Samia unawatanzania Watanzania ambao uvumilivu wao kwenye maumivu umebakia utambi tu halafu unaenda kutia kijiti machoni!
Lakini tume hii imewekwa na majina tu, haina vitu muhimu;
- Je, kazi hiyo inaanza lini?
- Ni yapi majukumu ya kila mmoja katika tume hii?
- Kazi ya tume hii inaisha lini?
La muhimu kabisa KWANINI IMEFICHWA KUWA TAX ALIWAHI KUWA WAZIRI WA ULINZI, ambaye chini yake aliwahi kutoa maagizo ya kipumbavu ili wanchi wafanyiwe ukatili na kuuliwa? Ili aonekane Mwanadiplomasia mbobevu wakati ni juzi tu hapo alisema akina Agather na mwenzake aashughulikiwe? Muuaji akamchunguze muuaji?!
Lakini hapo nyuma iliundwa tume ya haki jinai na ikaja na mapendekezo mazuri tu ambayo yangefanyiwa kazi tusingefika hapa na kushuhudia mauaji mabaya kabisa kuwahi kutokea katika historia ya nchi yetu.
Hii ripoti kuna ulichotekeleza Samia - Tume ya Haki Jinai: TAKUKURU ina watumishi Wala Rushwa na Wasio Wabobevu
Haya ni matokeo ya kuuza matokeo ya tume zote hizo, na wakulaumiwa ni wewe SAMIA.
=====
TAARIFA KWA UMMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32, ameunda Tume Huru ya kufanya uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea nchini wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba, 2025.
Aidha, Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo na wajumbe walioteuliwa ni wafuatao:-
(i) Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania;
(ii) Balozi Ombeni Yohana Sefue Kiongozi Mstaafu; Mwanadiplomasia na Katibu Mkuu
(iii) Balozi Radhia Msuya - Mwanadiplomasia na Balozi Mstaafu;
(iv) Balozi Lt. Gen. Paul Meela - Mwanadiplomasia na Balozi Mstaafu;
(v) IGP (Mstaafu) Said Ally Mwema Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Mstaafu;
(vi) Balozi David Kapya - Mwanadiplomasia na Balozi Mstaafu; na(vii) Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax Aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Imetolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi,
Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka
KATIBU MKUU KIONGOZI
18 Novemba, 2025
View attachment 3503744
Kuwa serious kwenye mambo yanayohusu maisha ya watu mkuu ,watu wameuawa wewe unaleta upuuzi wako wa UDINI.Tume huru unataka iundwe na Maaskofu wa TEC. Walio kwenye Tume ni majaji wakuu wastafu wanaoheshimika duniani kote. Wewe unataka wawekwe akina nani?
Jina la tume lina ukakasi sana.Tume Huru ya kufanya uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea nchini wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu
Hapo shetani ni refarii kwenye mechi ya fainali kati ya walokole na wachawi.. wazee wa mikeka tuna stake mpaka moyo, maini na figo maana bingwa tunamjua..Yeye ndiye anatuhumiwa. Halafu yeye ndiye anaunda tume kujichunguza😅😅
Mtuhumiwa namba moja ndio aliyeunda tume. Mtu mjinga tu ndii anaweza kuamini hao wahuni waitwao tume huru.Hasira hasara. Kama umehusika mkono wa sheria utakupitia.
Ulifanya fujo kwani Komwe?Ngoja nianze kujipanga.
Nimeshanunua njugu debe mbili nimeweka ndani.
Mkiona sipatikani baada ya disemba mjue nimetoroka niko mogadishu.
Bye bye Tanganyika.
Kwanini hawajesema kuwa alikuwa Waziri Wa Ulinzi?Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax Aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Subiri uone kitakachotokea. Unadhani kupindua serikali ni jambo dogo. Baada ya wiki mbili hii message utakuja kuirudia. Serikali haifanyi mambo kwa mihemko. Kila kitu kinawekwa kwenye utaratibu.Mtuhumiwa namba moja ndio aliyeunda tume. Mtu mjinga tu ndii anaweza kuamini hao wahuni waitwao tume huru.
Wote watu wa mfumo.Kichekesho. Tax anaenda kuchunguza Nini na alikuwa kwenye mfumo? Au anaenda kuvuruga uchunguzi?
Ingia sasa hivi na vpn yako 😅