Rais Samia autengua uteuzi wa Mkurugenzi mpya wa TPDC. Amrejesha Mataragio

Mama keshafahamu analishwa matango pori, mama awe makini team inayomzunguka kuna watu wanapanga safu zao asipoangalia 2025 atajikuta nje...
Ndiyo maana Magu alikuwa anajilipua mwenyewe tu na misalaba anaibeba yeye.
 
Mama amezungukwa na mafisadi, walitaka kumuingiza mkenge; thanks to JF ndio iliyomuamsha.

Local largest trading partner wa Tanzania ni Kenya, raisi wao alimpa ushauri wa bure hadharani; stick to Magufuli road map mama aache kuleta ubunifu wake.

Asikilize tena na ushauri wa JF akae karibu na Jaffo, Majaliwa, Biteko na Dr Mpango; hao ndio wanaweza mwambia what would Magufuli do.
 
Amuulize Jiwe alokuwa anateua watu baada ya muda anawatengua?
 
Zaidi ya tisa?????
Miaka tisa na miezi kadhaa, na kuna uwezekano huko mbele ya safari, tukaja kumuongezea na bonus nyingine ya miaka kadhaa kwa sababu hatujawahi kupata Rais mwanamke tangu tupate Uhuru
 
Miaka tisa na miezi kadhaa, na kuna uwezekano huko mbele ya safari, tukaja kumuongezea bonus ya miaka minnine kadhaa mingine kwa sababu hatujawahi kupata Rais mwanamke tangu tupate Uhuru
Mapema sana kusema hivo
 
Mkuu hapo halijatolewa tamko lingine kuwa anapelekwa wapi tena baada ya utenguzi.
Kujibu swali lako ni kuwa anatakiwa kusalia nyumbani/ aendelee na mambo yake binafsi tu.

Ila kuhusu kutolewa sehemu ambako alikuwepo mwanzoni, urejeshwaji wa huko mpaka tamko tena.
 
Kwanini Rais anateua mtu ambaye hamjui vizuri na hana CV zake mezani? washauri wa Rais kwenye mambo ya uteuzi ni akina nani!?
Hapo ndipo kwenye Tatizo kuu
 
Mama anaharaka gani wakati tushamwambia nchi yake hii???

Atulie bhana..
 
Hizi sifa rukuki kwa jambo dogo lifanywalo na viongozi wetu linawaharibu. Wa Tz mmepatwa na kirusi gani hiki?
Mbona hizo sifa "lukuki" wengine hatuzioni. Ziainishe tuchambue kama anazo kweli au hana.
 
Mkuu wenye mamlaka ya utenguzi hawajatoa tamko lingine aende wapi tena.
Kujibu swali lako ni kwamba bwana Mwesiga kesho aendelee tu mambo yake binafsi.

Akienda ofisi ambayo alikuwepo awali, walinzi lazima wamzuie getini. Akishatoa maelezo huko ofisini anakwenda kufanya nini, wanaweza wakamruhusu au vinginevyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…