Jana Rais Samia Suluhu alimteua Thobias Mwesiga Richard kuwa Mkurugenzi mkuu wa shirika la maendeleo ya petroli nchini (TPDC). Hii ilikua imani kubwa sana kwa vijana kupewa nafasi kubwa kama hiyo.
Thobias kijana wa miaka 34 ni kada wa CCM na mwaka 2017 aligombea uenyekiti wa UVCCM akaangushwa na Heri James. Mwaka 2020 alitia nia ya ubunge huko Nkenge lakini akaangushwa kwenye kura za maoni.
Wakati Thobias na MATAGA wenzie wakishangilia, leo Mama samia katengua uteuzi wake. Kafurushwa TPDC. Yani leo ni siku mbaya sana kwa vijana wa MATAGA.
Kama mnakumbuka mama Samia wakati akiwaapisha mawaziri alisema atakua anaangalia rekodi katika teuzi anazofanya. Na akasema jicho macho yake yamelegea lakini yanaona. Kwahiyo kila mtu rekodi yake itamfuata.
Bila shaka Mama Samia ameangalia rekodi na kukuta Thobias ni moja ya vijana waliowahi kutuhumiwa kuhusika na magenge ya kuteka na kutesa watu. Tarehe 20 January mwaka 2019, aliyekua Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe alitishiwa kuuawa na Thobias.
Akapeleka malalamiko kwa Spika kwamba usalama wake upo mashakani lakini akapuuzwa. Akaenda kuripoti polisi lakini Polisi hata hawakumkamata wala kumhoji Thobias. Baadae Zitto akaamua kuweka wazi taarifa za kijana huyo mtandaoni kwa ajili ya usalama wake.
Zitto akasema Thobias ni afisa wa TISS na amekua akitumia nafasi hiyo kutisha, kuteka na kutesa watu hasa wanaoikosoa serikali. TISS hawakutoa tamko lolote la kupinga au kukubali kama Thobias ni afisa wao. Lakini wakurya husema silence means YES.
Jana Thobias kapewa heshima kubwa sana ya kuongoza shirika kubwa la TPDC. Shirika linaloshughulikia masuala yote ya mafuta na gesi nchini. Lakini rekodi yake imemmaliza mwenyewe, akaishia kufurushwa kabla hata jogoo hajawika.
Hii iwe fundisho kwa MATAGA na vijana wengine wanaotumia nafasi zao kunyanyasa, kudhulumu au kutesa wengine ili waonekane wanaitetea serikali. Zama zimebadilika. Mama hataki huo upuuzi.
Hata wale maDC na maRC mliotumia nafasi zenu kuumiza wengine jiandaeni kisaikolojia. Soon mtanyolewa kama Thobias, maana mama amesema anaangalia rekodi.