Rais Samia avunja Bodi ya TRC, atengua uteuzi wa Wakala wa Ndege za Serikali. Aagiza wabadhirifu washughulikiwe


kama nimeelewa vibaya utanisahihisha
Ina Maana Makatibu wakuu+Wakurugenzi waisome report na kuifanyia kazi!
Ina Maana Kama kuna Makosa/Mapungufu ambayo yanefanya say na Afisa A,Au Meneja fulani,Afisa fulani,Mkuu wa Idara,Mhasibu,Engineer,Afisa ugavi,Mwanasheria,nk nk
hao wakuu waliotajwa wamepewa Rungu wamuwajibishe!
Kwani Kuna Makosa hapo?
Nisahihishe kama Nitakuwa nimekosea kiutendaji!(Protocol)
Instead ya Kuwawajibisha Mawaziri/Makatibu wakuu au wakurugenzi.
Wewe Una mawazo gani na Kwa nini?
Nadhani Kama ulivyosema wakuu hao wa Mashirika Labda hawahusiki moja kwa moja na Utendaji!…Labda kuna wa Chini anaanzisha yeye Anaidhinisha…
sasa Anatafutwa alieanzisha? Kuomba manunuzi fulani Au Sijui nisemeje bt nadhani
Kila kitu kinawnzia chini kwenda Juu!
Kuna Uwajibikaji kwa nafasi hata kama hujatenda(Yaani Kiongozi,Na Kuwajibika kiutendaji…Alietenda say Afisa A.
nisahihishe Mkuu kama nimekosea
 
Nampongeza mno kwa hili, binafsi sikutegemea hata kama anaweza kunyanyua ukucha. Sikumdharau ila kwa jinsi huu utawala ulivyoshabihiana na ule wa janjajanja Jakaya, kwakweli sikutegemea hili.
Kadogosa anafanya nini TRC?
 
NHIF na hasara ya zaidi ya Bilioni 204 ndani ya mwaka mmoja tu, Mbona bodi haijahuswa? Mama kazi imekuwa ngumu.
 
Sasa hizi si ndio hatua zenyewe! Sio lazima ziwe zile kichwa chako kinatamani
 
Ningetamani siku ripot ya CAG Inasomwa nchi nzima akae isikilize wote wajue nanii wanao kwamisha maendeleo.
 

Mh. Rais wetu yuko makini sana.. Naona kaanza na Bodi ya TRC na Wakala wa Ndege za Serikali.

Asante sana Mama yetu, Rais wetu, hakika unafanya kazi bora sana kwa nchi yetu, Mungu akubariki sana. Mh. Rais kaagiza wabadhirifu wote washughulikiwe tena kwa haraka kabisa, Mwenyezi Mungu mlinde sana Rais wetu, amen..
 
Hujui governance
 
Kwani hizi anazochukua sio hatua? Kumbuka Rais Huwa hana mihemko na hataki kumuonea mtu.

Ukweli ukibainika wote wataondoka.
Hujaelewa alichokiandika?

What if aliowatuma nao wanahusika?

Wakachunguze nini tena wakati inaeleweka na yeye ndio msemaji wa mwisho?

Nyie kazaneni mihemko sijui kuonea watu wakati Taifa linaangamia
 

Acha ujuaji wee kijana, you are talking nosense. Mh. Rais akichukua hatua anajua sbb za msingi, acha kupiga makelele kama uko bar..
 
Halafu watanzania jamani tuache au tupunguze huku kusifusifu yaani hata kama ndio sehemu yako ya kula duh yaani imekuwa too much.
 

Acha kiherehere i told you..
 
Msifikiri kudukuza serikali ni rahisi rahisi hivyo kuna sheria na taratibu na kama rais amejinasibu ni muumini wa utawala bora basi hana budi kuzifuata.
 
Msifikiri kudukuza serikali ni rahisi rahisi hivyo kuna sheria na taratibu na kama rais amejinasibu ni muumini wa utawala bora basi hana budi kuzifuata.
 
Wanaotakiwa kushuhulikia wabadhirifu wenyewe ndio hivyo tena.

Maskini mama kashaaharibu boxing day ya pasaka
 
kweli Mama yuko kazini
 
Maagizo si vitendo,tunataka watu wote walioliingizia Taifa hasara wafanyiwe yafuatayo:
1.Wasimamishwe kazi.
2.Wachunguzwe,na ikithibishwa kwamba wameingizia Serikali hasara,wafukuzwe kazi.
3.Wafirisiwe mali walizozipata kwa kuiibia Serikali.

Short of that,Samia bado atakuwa hajafanya kitu.Tunataka Rais anayeuma,mpaka sasa bado.
 
Hii ni sinema tu ya ‘Bi Tozo’ kukimbia wajibu wake wa kuchukua hatua.

Jukumu la kuzuia fraud ndani ya shirika ni MD na senior team, sio auditor yeye anatoa tu taarifa.

Sasa CAG anaposema kuna fraud (jitihada za makusudi kuiba) mfano manunuzi hayana receipt, matumizi hayana ledger entry maana yake hela imetoka bank bila ya kueleweka imeenda wapi rasmi, falsification of documents na mambo mengine ya ovyo ya wizi.

☝️Hizo sio unintentional errors zinazohitaji maelezo ni fraud (wizi) nchi ina sheria ya fraud; hilo tena sio swala la kujadiliana na management ni swala la polisi au sijui TAKUKURU majizi husika yakamatwe na kutupwa lupango kabla ya hapo yatapike hizo hela.

Sio hizi porojo za sijui katibu mkuu asome report na kuchukua hatua. Hapo anatakiwa kamanda wa polisi au TAKUKURU kuhusika sio hadithi za siasa na uzembe wa kuchukua hatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…