Rais Samia avunja Bodi ya TRC, atengua uteuzi wa Wakala wa Ndege za Serikali. Aagiza wabadhirifu washughulikiwe

Huyu mtendaji mkuu ndo aliongeza 49m $ kwenye invoice bila shaka
 
Timu sifia sifia tayari ndani ya nyumba. Mwanzoni ilikuwa kimya kusubiria upepo.

Cc: Paskali
Paskali kuna wito wako au wenu huku
Pasikale atakuwa anabubujikwa na machozi tu muda huu
Pascal hana la kuongea zaidi ya kummwagia sifa marehemu
Mkuu brazaj , kiukweli kuniweka mimi team sifia kama machawa sio kunitendea haki!.
Mimi nasifia pale tuu panapostahili sifa.
Mimi sio chawa!.

P
 
Mkuu brazaj , kiukweli kuniweka mimi team sifia kama machawa sio kunitendea haki!.
Mimi nasifia pale tuu panapostahili sifa.
Mimi sio chawa!.

P
Wewe ni mwanasheria,mwanahabari n.k,we unaona mama kuwasukumizia makatibu na baadhi ya wakuu,hili suala la intentional fraud,ni sawa?
Je yeye(mama),anazuiwa na katiba,kuwaweka wote waliohusika au kutuhumiwa na fraud,pembeni,kupisha uchunguzi?
Mama angefukuza baadhi ya washauri wake,mi naona wanampotosha huku nchi ikiliwa,kwa manufaa yao.
 
Dunia inavisa sana , huyu Rais, kama yeye ni muoga ,siatupishe .

Kwann Urais uwe mtamu Kwa fahari na ulaji ,lkn yeye mwenyewe mzembe na muoga ?.


Kwa kauli hiii inamaana Hawa Mawaziri waloguswa na CAG, wataendelea kudunda tu vizuri
Hapana mama anasubiri majibu ya hao aliowatuma kufanya kazi likiweno bunge kama kuna mtu atahusika ambaye yeye ndio mwenye mamlaka ya uteuzi akipewa jina kwa mfano Mwigulu nchemba kahusika yeye atamtengua tu lakini mama anaonyesha wazi anataka uchambuzi wa kina ufanyike ili asimuonee mtu
 

Nami sioni jipya.

Hao Watendaji hawakutoa majibu ya kuridhisha kwa CAG na wanawajua wahusika wa huo ubadhirifu, lakini hawakuchukua hatua. Wafutwe kazi kwa kutokuwajibika na wachunguzwe kama wanahusika
 
Hili ndilo tatizo la kumtegemea executive president kwa kila kitu!. Naendelea kusisitiza need ya kuwa na an effective system. Uki mess tuu unagundulika, system ina kueject https://www.jamiiforums.com/threads...ot-dramas-ze-comedy-na-one-man-shows.1223270/
CAG ni Mdhibiti na Mkaguzi, tunapewa tuu Ripoti ya Ukaguzi lakini hakuna Ripoti ya Udhibiti!. Kama tunaibiwa hivi bila udhibiti, halafu madudu yanakuja kuonekana kwenye ukaguzi, mdhibiti alidhibiti nini?.

Ili watendaji wa serikali wswajibishwe na kuadhibiwa, tunataka sasa Ripoti ya Udhibiti kwanza kabla ya Ripoti ya ukaguzi.
P
 
Nami sioni jipya.

Hao Watendaji hawakutoa majibu ya kuridhisha kwa CAG na wanawajua wahusika wa huo ubadhirifu, lakini hawakuchukua hatua. Wafutwe kazi kwa kutokuwajibika na wachunguzwe kama wanahusika
Ccm ni majizi sana
 
Incompetent
 
Mawazo yangu ni haya, hiyo hatua aliyochukua Rais kwangu ni sawa na amekimbia wajibu wake kwa kutatua tatizo kwa njia nyepesi huku akiwa na uwezo wa kufanya kubwa zaidi.

Nasema hivyo kwa sababu, haiwezekani anaagiza wadogo waitwe kuhojiwa, tena na wale wakubwa wao ambao inawezekana walishirikiana kwenye wizi.

Hilo kwangu naona ni igizo tu, yeye kwa nafasi yake anachukua hatua gani kuwawajibisha wale walio chini yake? kwanini amekimbilia kuhangaika na hao wadogo, hawa wakubwa juu yao amemuachia nani?

Mnasema ndio taratibu, kwanini hizo taratibu zisiende sambamba, wakati wadogo wakishughulikiwa na makatibu wakuu, yeye ashughulike na walio chini yake?

Tatizo lake anaonekana ni mtu wa kusubiri tu kuletewa taarifa, hataki kuisumbua akili yake, hii itasababisha apelekewe taarifa za uongo ili hao jamaa waliohusika walindane, huku nyie mkishangilia kwa hatua za kudanganyika alizochukua!
 
H
Ikulu haiwezi kukwepa uhusika katika ufisadi mkubwa kiasi hiki
 
wewe kuna sheria,kanuni na taratibu za kiserikali,rais hakurupuki tu
 
Ungekuwa wewe ungefanyaje? Unazijua kazi na majukumu ya katibu mkuu kwenye wizard?
Duh watz wajuaji sana. Sasa hizi si ndio hatua zenyewe jamani ??? Mlitaka Whitwell wanyongwe bila hata kusikilizwa
.mkuu hawa jamaa wanataka rais atawale badala ya kuongoza marehemu yeye alikuwa anatawala hakuwa anaongoza hivyo jamaa wanapenda kusikia rais kafukuza au kasimamisha kazi rais anatoa maelekezo watendaji wanaghulikia mfano takukuru ndiyo inapewa KAZI
 
Mimi siangaishwi na chawa
 
Kama nakuelewa vile. Report ya Udhibiti!
 

Mkuu Paskali, hiyo ni fikira sadikika kwa maana kwamba binadamu aishi na kutenda kama malaika, je, ushetani wake wa ubinafsi auweke wapi?

Kila Taasisi na Serikalini kuna mifumo ya udhibiti na ndiyo maana watumishi watendao kinyume na Taratibu za kazi hugundulika na kuadhibiwa, iweje ufisadi na ubadhirifu huo usigundulike hadi CAG!! Na kwa utaratibu wa ukaguzi wa CAG ubadhirifu usio na majibu ndio huingia kwenye ripoti yake. Kwa sababu hiyo Watendaji wakuu husika hawana sababu ya kutokuchukua hatua pale CAG anapogundua ubadhirifu pasipo kusubiri maagizo ya mamlaka ya uteuzi wao.

Taasisi yoyote kusimama imara hutegemea msimamo wa Mtendaji Mkuu. Hata kwenye familia kama Mkuu wa Kaya hajali kuchukua hatua kali, hiyo familia maisha yake ni ya hovyo hovyo.

Hivyo basi, Rais anapaswa kuchukua hatua kali, kwa uwezo (mamlaka na madaraka) aliyopewa kiKatiba: 34(3) na (4) Mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengineyo yote yahusuyo Tanzania Bara, yatakuwa mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano. (4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii,
madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.


WAHUNI sasa ndio wanaendesha nchi na CHAWA kutetea maamuzi ya Rais
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…