Rais Samia avunja Bodi ya TRC, atengua uteuzi wa Wakala wa Ndege za Serikali. Aagiza wabadhirifu washughulikiwe

Rais Samia avunja Bodi ya TRC, atengua uteuzi wa Wakala wa Ndege za Serikali. Aagiza wabadhirifu washughulikiwe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amevunja Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Aidha, Rais Samia ametengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Mhandisi John Nzulule.

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais amemuelekeza Katibu Mkuu Kiongozi kuhakikisha kuwa Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wote wa Taasisi za Serikali wanaipitia kwa kina tarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kujibu na kuzifanyia kazi kwa haraka hoja zote zinazogusa maeneo yao.

Vile vile, Mhe. Rais ameelekeza kuwa watendaji wote watakaobainika kuhusika na uzembe au ubadhirifu wachukuliwe hatua za kisheria.

View attachment 2582469
Huyu mtendaji mkuu ndo aliongeza 49m $ kwenye invoice bila shaka
 
Timu sifia sifia tayari ndani ya nyumba. Mwanzoni ilikuwa kimya kusubiria upepo.

Cc: Paskali
Paskali kuna wito wako au wenu huku
Pasikale atakuwa anabubujikwa na machozi tu muda huu
Pascal hana la kuongea zaidi ya kummwagia sifa marehemu
Mkuu brazaj , kiukweli kuniweka mimi team sifia kama machawa sio kunitendea haki!.
Mimi nasifia pale tuu panapostahili sifa.
Mimi sio chawa!.

P
 
Mkuu brazaj , kiukweli kuniweka mimi team sifia kama machawa sio kunitendea haki!.
Mimi nasifia pale tuu panapostahili sifa.
Mimi sio chawa!.

P
Wewe ni mwanasheria,mwanahabari n.k,we unaona mama kuwasukumizia makatibu na baadhi ya wakuu,hili suala la intentional fraud,ni sawa?
Je yeye(mama),anazuiwa na katiba,kuwaweka wote waliohusika au kutuhumiwa na fraud,pembeni,kupisha uchunguzi?
Mama angefukuza baadhi ya washauri wake,mi naona wanampotosha huku nchi ikiliwa,kwa manufaa yao.
 
Dunia inavisa sana , huyu Rais, kama yeye ni muoga ,siatupishe .

Kwann Urais uwe mtamu Kwa fahari na ulaji ,lkn yeye mwenyewe mzembe na muoga ?.

Kwa kauli hiii inamaana Hawa Mawaziri waloguswa na CAG, wataendelea kudunda tu vizuri
Hapana mama anasubiri majibu ya hao aliowatuma kufanya kazi likiweno bunge kama kuna mtu atahusika ambaye yeye ndio mwenye mamlaka ya uteuzi akipewa jina kwa mfano Mwigulu nchemba kahusika yeye atamtengua tu lakini mama anaonyesha wazi anataka uchambuzi wa kina ufanyike ili asimuonee mtu
 
Inashangaza sana, kwanini Rais anawaagiza makatibu wakuu na watendaji wakuu wahakikishe wanapitia ripoti na kuwawajibisha wale waliohusika na uzembe?
...
Alichokifanya Rais hapo ni sawa na kufunika kombe mwanaharamu apite, kuhangaika na dagaa huku mapapa wapo tu ofisini, mimi sioni jipya, kapanua magoli tu hao jamaa wapate visingizio.

Nami sioni jipya.

Hao Watendaji hawakutoa majibu ya kuridhisha kwa CAG na wanawajua wahusika wa huo ubadhirifu, lakini hawakuchukua hatua. Wafutwe kazi kwa kutokuwajibika na wachunguzwe kama wanahusika
 
Wewe ni mwanasheria,mwanahabari n.k,we unaona mama kuwasukumizia makatibu na baadhi ya wakuu,hili suala la intentional fraud,ni sawa?
Je yeye(mama),anazuiwa na katiba,kuwaweka wote waliohusika au kutuhumiwa na fraud,pembeni,kupisha uchunguzi?
Mama angefukuza baadhi ya washauri wake,mi naona wanampotosha huku nchi ikiliwa,kwa manufaa yao.
Hili ndilo tatizo la kumtegemea executive president kwa kila kitu!. Naendelea kusisitiza need ya kuwa na an effective system. Uki mess tuu unagundulika, system ina kueject https://www.jamiiforums.com/threads...ot-dramas-ze-comedy-na-one-man-shows.1223270/
Wanabodi,
What are Priorities Zetu, Tanzania?. Nini ni Vipaumbele Vyetu? .
Taifa linakabiliwa la viongozi wasio na vision hivyo kukosa mission to accomplish, we seriously lack visionary leaders ndio maana karibu kila kitu ni mpaka rais aje!. Je nini vipaumbele vyetu?, Tanzania kama nchi inayotaka maenddeleo ya kweli, tunatakiwa tujue ni nini tunataka na tutapataje. Kama hujui unachotaka, huwezi kutafuta maana hujui utafute nini!. Ukiishajua unataka nini, ndipo unajipanga utapataje hicho unachokitaka na njia za kukitafutia ili ukipate!. Ukiisha kosa vision, huwezi kuwa na mission to accomplish ya unatekeleza nini, hivyo tumekuwa ni nchi ya kuendeshwa na matukio.

Ushauri wa A Way Forward and What to do.
Serikali yetu, kila wizara, kila idara na kila wakala, lazima ziwe na mission na vision statements, accompanied by a list ya Strategic Objectives ambazo ziko SMART (Specific, Measurable, Attainable, Realistic, Timely). Pia ziwepo timeline strategy ya utekelezaji hizo smart objectives, hivyo viongozi wajitokeze kutueleza na kutuonyesha achievements ya utekelezaji malengo kusudiwa na sio kutufanyia dramas na maonesho ya kuita media na kutoa maagizo na maelekezo kwa kusema tutafanya hiki au kile, lakini hatuoni, utekelezaji.

Mfano tunapo hubiri kuhusu Tanzania ya viwanda, where is the blue print ya Tanzania ya viwanda?, zenye smart objectives zenye malengo ya short term, medium term na long term strategies?. Ili tuwe na Tanzania ya viwanda tunahitaji land, where is the land set out kwa Tanzania ya Viwanda?. Tunahitaji labor, nguvu kazi ya Tanzania ya viwanda jee tumeishajua tutajenga viwanda gani na vya kuzalisha nini ili hiyo mainpower na labor force kuvihudumia hivyo viwanda itayarishwe?. Tunahitaji capital ya kuanzisha hivyo viwanda, kuna strategies gani kuwawezesha Watanzania kuimiliki Tanzania ya Viwanda?, au tunataka kujenga Tanzania ya viwanda lakini viwanda ni vya wawekezaji wageni, vya Mchina, Mhindi na Mzungu?, na Mtanzania kuja kuwa ni kibarua tuu kwenye hiyo,Tanzania ya Viwanda kama ilivyo kwenye Uchumi wa Gesi?.

Tanzania ya viwanda itahitaji malighafi ya viwanda, uchumi wa Tanzania unategemea kilimo, hivyo the biggest industries za Tanzania ya Viwanda zinapaswa kuwa ni agro processing industries, jee tuna mikakati gani ya kuinua sekta ya kilimo, ili izalishe malighafi ya viwanda?, au tunajenga Tanzania ya viwanda vya assembling imported components, or processing imported semi processed raw materials kama viwanda vya Bhakressa, vinatengeneza juices na kusaga unga wa ngano, lakini malighafi zote ni imported products, zinatoka nje!, hadi pulp ya mango juice tuna import, huku maembe ya Unyanyembe na Lushoto yakiozea mitini!. Tangu tumeanza kuhubiri wimbo wa Tanzania ya Viwanda, where is the blue print?, what is the plan?, tuko wapi, tumefanikisha nini? , tumekwama wapi and what is a way forward? .

Badala ya kuwahimiza ma bullies, impersonators, impostors na forgerist kuchapa kazi, tupewe matokeo ya hizo kazi zinazochwapwa, watu wanataka matokeo, na sio tuu kupokea maagizo na maelekezo tuu,kwa vitendo vya kuona sifa kutokelezea tuu kwenye TV huku wakitoa maagizo, maelekezo, na kuandikwa magazetini, sasa tujikite kwenye utendaji unaozingatia matokeo, na sifa zisiwe katika kutoa maagizo, bali ziwe katika matokeo ya utekelezaji wa maagizo hayo.

Tuanze ku demand kuonyeshwa results oriented events nini kilichofanyika na sio kututengenezea maigizo ya matukio. Kila siku tunaonyeshwa jinsi viongozi wetu wakizindua miradi, Viwanda, etc, lakini hatupewi mrejesho wowote hiyo miradi imeleta faida gani kwa wananchi na maendeleo ya taifa. Badala ya kuonyeshea viongozi wanasema nini na wanafanya nini, tuonyeshwe matokeo, results oriented actions.

Nakamilisha taratibu za kurusha Vipindi Maalum vya TV vitakavyoitwa "Kwa Maslahi ya Taifa" ambavyo vitaangazia nini kimefanyika, nini kifanyike kuitoa Tanzania hapa ilipo kwenda kwenye Tanzania tunayoitaka.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
CAG ni Mdhibiti na Mkaguzi, tunapewa tuu Ripoti ya Ukaguzi lakini hakuna Ripoti ya Udhibiti!. Kama tunaibiwa hivi bila udhibiti, halafu madudu yanakuja kuonekana kwenye ukaguzi, mdhibiti alidhibiti nini?.

Ili watendaji wa serikali wswajibishwe na kuadhibiwa, tunataka sasa Ripoti ya Udhibiti kwanza kabla ya Ripoti ya ukaguzi.
P
 
Nami sioni jipya.

Hao Watendaji hawakutoa majibu ya kuridhisha kwa CAG na wanawajua wahusika wa huo ubadhirifu, lakini hawakuchukua hatua. Wafutwe kazi kwa kutokuwajibika na wachunguzwe kama wanahusika
Ccm ni majizi sana
 
Inashangaza sana, kwanini Rais anawaagiza makatibu wakuu na watendaji wakuu wahakikishe wanapitia ripoti na kuwawajibisha wale waliohusika na uzembe?

Yeye kama Rais anachukua hatua gani kwa hao wakuu waliosimamia huo uzembe wakiwemo mawaziri? Kama yupo serious angetakiwa kuwaita mawaziri awaulize, wakati huo wizi ukitokea kwenye wizara zao walikuwa wapi? asiporidhishwa na majibu fukuza.

Haiingii akilini, hawa ambao inawezekana wameshirikiana kwenye wizi, unaagiza wachunguzane, huku ni kudanganyana tu, ndio maana kuna wakati Rais nae anatiliwa shaka.

Alichokifanya Rais hapo ni sawa na kufunika kombe mwanaharamu apite, kuhangaika na dagaa huku mapapa wapo tu ofisini, mimi sioni jipya, kapanua magoli tu hao jamaa wapate visingizio.
Incompetent
 
kama nimeelewa vibaya utanisahihisha
Ina Maana Makatibu wakuu+Wakurugenzi waisome report na kuifanyia kazi!
Ina Maana Kama kuna Makosa/Mapungufu ambayo yanefanya say na Afisa A,Au Meneja fulani,Afisa fulani,Mkuu wa Idara,Mhasibu,Engineer,Afisa ugavi,Mwanasheria,nk nk
hao wakuu waliotajwa wamepewa Rungu wamuwajibishe!
Kwani Kuna Makosa hapo?
Nisahihishe kama Nitakuwa nimekosea kiutendaji!(Protocol)
Instead ya Kuwawajibisha Mawaziri/Makatibu wakuu au wakurugenzi.
Wewe Una mawazo gani na Kwa nini?
Mawazo yangu ni haya, hiyo hatua aliyochukua Rais kwangu ni sawa na amekimbia wajibu wake kwa kutatua tatizo kwa njia nyepesi huku akiwa na uwezo wa kufanya kubwa zaidi.

Nasema hivyo kwa sababu, haiwezekani anaagiza wadogo waitwe kuhojiwa, tena na wale wakubwa wao ambao inawezekana walishirikiana kwenye wizi.

Hilo kwangu naona ni igizo tu, yeye kwa nafasi yake anachukua hatua gani kuwawajibisha wale walio chini yake? kwanini amekimbilia kuhangaika na hao wadogo, hawa wakubwa juu yao amemuachia nani?

Mnasema ndio taratibu, kwanini hizo taratibu zisiende sambamba, wakati wadogo wakishughulikiwa na makatibu wakuu, yeye ashughulike na walio chini yake?

Tatizo lake anaonekana ni mtu wa kusubiri tu kuletewa taarifa, hataki kuisumbua akili yake, hii itasababisha apelekewe taarifa za uongo ili hao jamaa waliohusika walindane, huku nyie mkishangilia kwa hatua za kudanganyika alizochukua!
 
H
Inashangaza sana, kwanini Rais anawaagiza makatibu wakuu na watendaji wakuu wahakikishe wanapitia ripoti na kuwawajibisha wale waliohusika na uzembe?

Yeye kama Rais anachukua hatua gani kwa hao wakuu waliosimamia huo uzembe wakiwemo mawaziri? Kama yupo serious angetakiwa kuwaita mawaziri awaulize, wakati huo wizi ukitokea kwenye wizara zao walikuwa wapi? asiporidhishwa na majibu fukuza.

Haiingii akilini, hawa ambao inawezekana wameshirikiana kwenye wizi, unaagiza wachunguzane, huku ni kudanganyana tu, ndio maana kuna wakati Rais nae anatiliwa shaka.

Alichokifanya Rais hapo ni sawa na kufunika kombe mwanaharamu apite, kuhangaika na dagaa huku mapapa wapo tu ofisini, mimi sioni jipya, kapanua magoli tu hao jamaa wapate visingizio.
Ikulu haiwezi kukwepa uhusika katika ufisadi mkubwa kiasi hiki
 
wewe kuna sheria,kanuni na taratibu za kiserikali,rais hakurupuki tu
 
Ungekuwa wewe ungefanyaje? Unazijua kazi na majukumu ya katibu mkuu kwenye wizard?
Duh watz wajuaji sana. Sasa hizi si ndio hatua zenyewe jamani ??? Mlitaka Whitwell wanyongwe bila hata kusikilizwa
.mkuu hawa jamaa wanataka rais atawale badala ya kuongoza marehemu yeye alikuwa anatawala hakuwa anaongoza hivyo jamaa wanapenda kusikia rais kafukuza au kasimamisha kazi rais anatoa maelekezo watendaji wanaghulikia mfano takukuru ndiyo inapewa KAZI
 
Mmawia wewr ni mpumbavu na hujaelimika. Kwa maana hiyo unataka tuamini kuwa kibarua cha Rais Dkt Samia enzi akiwa chini ya Dkt Magufuli ilikuwa kuratibu maujai ya bosi wake afe ili yeye awe rais???? Hii kauli yako Mmawia ni mbaya sana na inaharibu taswira ya uzalendo wa Rais Dkt Samia. Sisi kama chawa wa Rais Dkt Samia tunasema Dkt Samia na Dkt Magufuli ni kitu kimoja, wembe ule ule, yeye alitoa uhuru wa watendaji na wamejisahau sasa ngoja panga lipite.
Mimi siangaishwi na chawa
 
CAG ni Mdhibiti na Mkaguzi, tunapewa tuu Ripoti ya Ukaguzi lakini hakuna Ripoti ya Udhibiti!. Kama tunaibiwa hivi bila udhibiti, halafu madudu yanakuja kuonekana kwenye ukaguzi, mdhibiti alidhibiti nini?.

Ili watendaji wa serikali wswajibishwe na kuadhibiwa, tunataka sasa Ripoti ya Udhibiti kwanza kabla ya Ripoti ya ukaguzi.
P
Kama nakuelewa vile. Report ya Udhibiti!
 
Hili ndilo tatizo la kumtegemea executive president kwa kila kitu!.
...
CAG ni Mdhibiti na Mkaguzi, tunapewa tuu Ripoti ya Ukaguzi lakini hakuna Ripoti ya Udhibiti!. Kama tunaibiwa hivi bila udhibiti, halafu madudu yanakuja kuonekana kwenye ukaguzi, mdhibiti alidhibiti nini?.

Ili watendaji wa serikali wswajibishwe na kuadhibiwa, tunataka sasa Ripoti ya Udhibiti kwanza kabla ya Ripoti ya ukaguzi.
P

Mkuu Paskali, hiyo ni fikira sadikika kwa maana kwamba binadamu aishi na kutenda kama malaika, je, ushetani wake wa ubinafsi auweke wapi?

Kila Taasisi na Serikalini kuna mifumo ya udhibiti na ndiyo maana watumishi watendao kinyume na Taratibu za kazi hugundulika na kuadhibiwa, iweje ufisadi na ubadhirifu huo usigundulike hadi CAG!! Na kwa utaratibu wa ukaguzi wa CAG ubadhirifu usio na majibu ndio huingia kwenye ripoti yake. Kwa sababu hiyo Watendaji wakuu husika hawana sababu ya kutokuchukua hatua pale CAG anapogundua ubadhirifu pasipo kusubiri maagizo ya mamlaka ya uteuzi wao.

Taasisi yoyote kusimama imara hutegemea msimamo wa Mtendaji Mkuu. Hata kwenye familia kama Mkuu wa Kaya hajali kuchukua hatua kali, hiyo familia maisha yake ni ya hovyo hovyo.

Hivyo basi, Rais anapaswa kuchukua hatua kali, kwa uwezo (mamlaka na madaraka) aliyopewa kiKatiba: 34(3) na (4) Mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengineyo yote yahusuyo Tanzania Bara, yatakuwa mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano. (4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii,
madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

WAHUNI sasa ndio wanaendesha nchi na CHAWA kutetea maamuzi ya Rais
 
Back
Top Bottom