Hongera sana Mtendaji Mkuu wa Mahakama
Elisante Gabrieli, hakika unalo jukumu la kuuboresha zaidi Muhimili huu wa Mahakama ambao ni muhimu kwa wananchi.
sisi wananchi tunataka kutendewa haki.
hakikisha watumishi wa mahakama wanapendana wao kwa wao, wapunguze majungu maana majungu yanapunguza ufanisi wa kazi. kwanza hakikisha haki inatendeka miongoni mwa watumishi wa Muhimili wa Mahakama kwa kufanya hivyo na sisi wananchi tutakuwa na imani kuwa tutatendewa haki. Haki lazima kwanza itawale kwenye Muhimili wenyewe hiyo itajenga imani kwa wananchi.
ondoa uonevu, haki itawale. usikubali kuhadaiwa na wachache, simamia weledi wako.
watumishi wa Mahakama badilikeni acheni kusemana semana na majungu maofisini, mmeaminwa kutenda haki acheni tabia zisizo faaa zinatukera sisi wananchi.
Mtendaji Mkuu Prof. Elisante atasafisha uozo wote, tabia za kinafiki, tabia za kujipendekeza kwa nia ya kupata upendeleo n.k safisha.
watumishi wa mahakama badilikeni.