Rais Samia awaapisha Wakuu wa Mikoa. Afanya mabadiliko madogo, Kafulila apelekwa Simiyu, Mongella aletwa Arusha

Rais Samia awaapisha Wakuu wa Mikoa. Afanya mabadiliko madogo, Kafulila apelekwa Simiyu, Mongella aletwa Arusha

Yaan hapo ni kama alifanya demotion Kwa Mongela , yaan unamtoa mwanza unaenda kumtupa Simiyu? Daah Bora amembalansia aisee
Hakuna watu walio na furaha kama watu wa Simiyu kuondolewa huo mzigo,Simiyu wanahitaji mtu mbunifu na mchapakazi kama Mtaka, walikuwa wameumia watu wangu hatimae God kawasikia huyo mzoefu acha akapumzikie ARUSHA, Simiyu wanahitaji kukimbia sio kutembea.
 
Wakati anampanga Kafulila Arusha alikuwa hajui kama ndiyo mgeni? mbona Makonda alianzia Dar?
Taaarifa ndg mwenyekiti... taaarifa ndugu mwekekiti. Eeer. Eeeer! Kama sababu ni hiyo, kwanini Kunenge kapelekwa pwani, tuseme ni demotion ile au ni nini?
 
Sijafurahia reason ya kubadilisha wakuu wa mikoa. Mongela anapelekwa Arusha kwa sababu ni "mzoefu" na majiji na Kafulila ni mpya. This is not a reason for sure kwa sababu yule David, although ni "mpya" ni mbunifu sana kuliko Mongela (kwa mtazamo wangu).

Kama kweli hayo ndiyo majukumu ya mkuu wa mkoa as per VP Phillip, wakuu wa mikoa wanaoweza kufanya kazi hiyo popote pale ni Kafulila, Mtaka, and Queen.
Mwenye cv ya Mongella tafadhali.
 
Kwani hujasikia
kuna majaribio Simiyu,Jembe lililokuwa huko limepanda hadhi hadi DODOMA halafu unasema mkoa wa majaribio?
Kwani hujasikia sababu za kumtoa Arusha na kumpeleka simiyu si wamesema wanampeleka huko kwa kuwa ndio anaanza nafasi ya ukuu wa mkoa
 
Kwani hujasikia
Kwani hujasikia sababu za kumtoa Arusha na kumpeleka simiyu si wamesema wanampeleka huko kwa kuwa ndio anaanza nafasi ya ukuu wa mkoa
Kwa ujumla wasaidizi wa mama inabidi wajipange hawako sawa,ukienda Simiyu hutaamini kuwa huo ni mkoa umeanzishwa miaka kama kumi tu iliyopita,ni mkoa unakimbia kimaendeleo,lakini kwangu naamini Kafulila yupo vizuri kuliko Mongela,alifeli Mwanza kila mtu aliona.
 
There is a difference between creativity and innovation. By the way, my bro Abubakar kupelekwa Pwani ni demotion right?You wanna tell us that kuna mikoa ya kujifunzia?Probably, ndiyo maana maendeleo kwenye hiyo mikoa hakuna maana ni ya kujifunzia?Really?Are you guys serious?
Utafikir mikoa mingine wanaishi watu nusu....kuna mikoa mikubwa kieneo lakini inazidiwa na mikoa midogo kieneo and vice versa katika suala la complicity na maendeleo
 
Kwani hujasikia
Kwani hujasikia sababu za kumtoa Arusha na kumpeleka simiyu si wamesema wanampeleka huko kwa kuwa ndio anaanza nafasi ya ukuu wa mkoa
Kwa hiyo Simiyu ni kwa majaribio?! Mbona mkoa mpya ule na umekimbia na kukimbiza kuliko mikoa mikongwe in the shortest period of time
 


Dkt. Mpango: Wakuu wa Mikoa wasiwe walevi na wazinzi
Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango, amewataka Wakuu wa Mikoa walioapishwa Mei 19, 2021 wafanye kazi kwa weledi Asema Kiongozi mzuri ni yule mwenye busara na bidii ya kazi

Jaji Mkuu: DPP ni chujio la kwanza la haki
Prof. Ibrahim Juma amesema, "DPP hawezi kuingiliwa na mtu yeyote, hata Jaji Mkuu hana mamlaka ya kuingilia kazi yake" Asema Mkurugenzi wa Mashtaka amepewa wajibu wa kuangalia maslahi ya Taifa

Spika Ndugai: Wakuu wa Mikoa msijione Marais
“Wapo Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wanaamini kule waliko wao ni Marais, utasikia Mimi Rais wa Mkoa huu au Wilaya hii nani kasema?, Rais wa Nchi hii ni mmoja tu, Samia Suluhu Hassan, ukijivisha koti ambalo si lako matokeo yake unaweza kufanya mambo ukidhania wewe Rais”

Rais Samia afanya Mabadiliko teuzi za Wakuu wa Mikoa Arusha na Simiyu
John Mongella aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha

David Kafulila ambaye awali aliteuliwa kuwa RC Arusha atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu

“Kuna mabadiliko madogo nimefanya, Kafulila nilimteua kuwa RC Arusha na Mongella RC Simiyu, nimeamua Mongella kwasababu ulikuwa unaongoza Mkoa mkubwa basi ukawe RC Arusha na Kafulila kwasababu ndio anaanza alikuwa RAS basi akawe RC Simiyu” Rais Samia

“Baada ya shughuli hizi za kuapishana na kupiga picha Wakuu wa Mikoa na Wateuliwa wengine mtarudi hapa na tutakuwa na kikao cha kazi kwahiyo kwasababu nina mambo mengi ya kuongea na nyinyi leo tuishie hapa tutakutana kwenye kikao cha kazi”

“Wote mlioapa na mlioteuliwa hongereni sana, nasema hongereni kwasababu Tanzania kuna Watu wengi na 15% wangefaa kuteuliwa lakini mmeteuliwa nyinyi, naamini mnapokwenda kufanya kazi zenu mtasimama na Mungu”
View attachment 1790979View attachment 1790981

Huyo jirani nae kapata shavu, alishaukana uraia wa Burundi?
 
Hakuna watu walio na furaha kama watu wa Simiyu kuondolewa huo mzigo,Simiyu wanahitaji mtu mbunifu na mchapakazi kama Mtaka, walikuwa wameumia watu wangu hatimae God kawasikia huyo mzoefu acha akapumzikie ARUSHA, Simiyu wanahitaji kukimbia sio kutembea.



Mtaka ni hitaji la wengi!

Hata huku Tanga ninamuota tuletewe aje ahamaishe elimu na kuhimiza mindsets za watu kupenda kufanyakazi Kwa bidii.

Sema sasa ni kama wana mvuruga ki-psychologically.
 
Back
Top Bottom