Hakuna kitu kibaya kama uchawa uliopitiliza, sasa Steve Nyerere na genge lake wametoswa hadharani na Rais wa jamhuri ya muungano tayari amewaambia yeye hana kundi na ni mama wa wote habagui mtu, tabia za kujipendekeza siku zote mwisho wake ni mbaya.
Nasikia Jamaa tangu juzi anaogopa kuonana na watu baada ya Rais kumsema hadharani na kundi lake la kihuni! Sasa ni wakati wa Steve Nyerere kujitathimini yeye mwenyewe kauli anazozitoa mara kwa mara akiwa na waandishi wa habari.
Tabia ya huyo bwana amekuwa akitumika Sana na kundi linalokula vinono ndani ya CCM! Kutukana watu wenye mawazo tofauti na serikali sasa nadhani meseji ameipata kutoka kwa mhusika mkuu.