Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Huo mpasuko uliotokea kwenye jamii uko wapi?Au umetokea moyoni mwako?Acha kukuza mambo!Hakutajwa mtu.Piga kazi.Unajilazimishia kupata magonjwa ya moyo bure!
 
Mlikuwa mnasubiri chambo? Mwachen amalize muda wake mama wa watu.Hiz dini zipo tu
 
Umenielewa lakini mkuu au umekurupuka tu na makasiriko kwa Magufuli?

Nimesema huwezi kufanya starehe utakavyo kwa maana starehe nyingi zipo kwenye matendo ya dhambi, lakini hapa duniani hatujaja kufanya starehe hivyo kama utaishi maisha ya kuendekeza starehe sana kuliko ibada basi moto unaweza ukakuhusu.

Jaribu kuzuia hasira zako kwa simba wa yuda maana hazina msaada wowote mtu mwenyewe ameshakufa wewe unabaki kukosa amani ya moyo kila anapotajwa huyo Magufuli.
 
Haya ngoja tuone heshima ya moyoni. Hautasahau maisha yako yote. Watendaji wa serikali yako bila misuli utavuna mabua.
 

Safi kabisa kwa kuweka ukweli hadharani. Haya mafuta ya kupikia yalipanda bei wakati wake alipoingilia biashara ya mafuta. Toka wakati ule bei haikushuka tena. Na sukari mwenendo ulikuwa huo huo. Kama kina kitu kiliniuma na kufariki kwa watu wa ajali ya lori la mafuta kwa kisingizio cha kutubiwa kizalendo hapa nchini. Baba yangu alikuwa muhanga wa moto wa gas huko Arusha nikiwa mtoto mchanga. Anasema walikuja wataalamu toka Ujerumani ambapo watu wengi sana walipona. Sasa kwa ukuaji huu wa technology miaka karibia 40 mbele watu wamekufa hapo Muhimbili kwa porojo eti wanatibiwa kizalendo. Kwanini wasingeletwa wataalamu kuwatibu au kupelekwa nje kupata matibabu? Yaani hata Lisu wangekosea wamlete hapa Muhimbili leo hii angekuwa marehemu tayari.
 
Tofauiti na baba na mama hakuna mtu mwibgine hapa tz anaweza heshiniwa toka moyoni
 
2030 sio mbali subiri tu ataondoka
 

Nyie ndio mnalilia huyo simba wenu wa yuda ukweli wake ukiwekwa hadharani. Narudia tena, huyo mama yuko sahihi kuwa kipindi cha dhalimu hakukuwa na nidhamu za kweli, bali watu walitii chochote bila kujali sheria inasema nini kwa kumuhofia kiongozi muovu. Sasa mama ameweka wazi, nidhamu ya woga iiondoke, watu wafanye kazi kwa kufuata sheria, na sio kutaka kumfurahisha kiongozi hata kama ni kinyume cha sheria. Kufa kwake sio kinga ya uovu wake kutokusemwa.
 
Meza panadol mkuu hii nchi ni mali ya wana siasa
 

Hakuna kiongozi alileta maneno ya mgawanyiko kwa watanzania kama dhalimu vwa chattle, msidhani tumesahau. Umesahau maneno kuwa watu wa mwanza wasivunjiwe nyumba maana ndio wamenipa kura? Umesahau maneno kuwa sileti maendeleo maeneo haya maana mmechagua wapinzani? Au wakati wa lugha zile ulikuwa hujajiunga hapa jf uanzishe uzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…