Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Hakuna mtanzania anampenda yule mtu katili
Mkuu mbona unaonokana una chuki kuu na bwana yule?
Ama wewe ni moja kati ya waliotumbuliwa na vyeti feki?
Unapata wapi ujasiri wa kuwazungumzia watanzania wote kwamba atumpendi rais wetu mpendwa?
Kama wewe unamchukia ni sawa ila mimi sina chuki wala makasiriko nae hata kidogo.
Kuwa na aman ameshafariki ni mwaka sasa.
Mwache apumzike kwa amani.
 
Eti eeh
02158EE2-9329-4FAC-B276-EEAE0B9A0042.jpeg
 
Hali yetu ndani ya civil service si nzuri sana, tunasifiwa kwamba adjustments tulizofanya awamu ya tano kidogo zimekuza heshima, lakini heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwasababu kulikuwa na Simba wa Yuda ambaye ukimgusa sharubu anakurarua hata hivyo haikukua vizuri, ” Rais Samia

View attachment 2172747
---

Hakika kila chenye mwanzo lazima kiwe na mwisho.

Kumbe zile sifa za ooo nchi imerudisha heshima kwenye sehemu za kazi ilikuwa ni nidhamu ya uoga tu.

Magufuli alikuwa anawatishia watu na wakawa wanaonyesha heshima ya uoga.
Mama akituambia yeye na mwendazake ni jora moja, sasa leo mbona kunatokea haya? au Ni kinyume chake???
 
Nafikiri kinachofanyika sasa ni ku out smart uongozi uliopita. Kama magu alimfanyia kikwete ni kukandia madhaifu tuu ili wewe uonekane unabadili muelekeo
watu walijengwa kwenye nidhamu ya woga, unafiki mwingi. Wanadamu timamu hatutakiwi kuishi hivyo. Maza katoa fact sio suala la ku out smart

YESU NI MWOKOZI
 
watu walijengwa kwenye nidhamu ya woga, unafiki mwingi. Wanadamu timamu hatutakiwi kuishi hivyo. Maza katoa fact sio suala la ku out smart

YESU NI MWOKOZI
Kama ilikuwa inaketa tija safi sana!
.
Sasa yeye ajenge huo mfumo sasa anaotaka wa kutoka moyoni, aujenge ili mambo yaende hicho ndio watu wanataka

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Tulihangaika sana enzi za lile jiwe lililoanguka. Yaani hakuna mtu mwenye maono alipaza sauti wote tulikaa kimya tukijiongelesha moyoni huku tukiona vituko na tunavisifia ili tuonekane ni wenzao. Kwa kweli kuna zama za unafki
 
Sasa kuogopa kufukuzwa kazi sindio nidhamu inayohitajika. Kama huna hofu ya kupoteza kitu ambacho ni cha maana kwako utakuwaje makini?
Sio nidhamu ni woga, hivyo mtu anafanya kitu hata ambacho kisheria hakikupaswa ili kumfurahisha Mh Rais. Hiyo hautakiwi. Nidhamu ya woga.
 
Sasa kuogopa kufukuzwa kazi sindio nidhamu inayohitajika. Kama huna hofu ya kupoteza kitu ambacho ni cha maana kwako utakuwaje makini?
Muheshimiwa,kufukuzwa kazi ni sehemu ndogo sana katika utumishi iwezayo kumtokea mfanyakazi.Hatupaswi kuwajenga watumishi kwa fikra za kufukuzwafukuzwa.Bali,wajengewe matumaini ya kudumu,kustawi na kuufurahia utumishi.Kufukuzwa iwe ni kama ajali tu.
 
Nilichojifunza kutokana na kifo cha hayati Magufuli ni kuwa mtu wako karibu kabisa akikosa matarajio yoyote toka kwako ndio ataonyesha rangi zake zote either ni nzuri au baya. Hapa amesahau na yeye ni time will tell kwa upande wake. R. I. P our Icon, the late President John Joseph Pombe Magufuli.
 
View attachment 2172780

"Tunasifiwa kwamba adjustments [maboresho] tuliyoyafanya awamu ya tano kidogo zimekuza heshima ndani ya utumishi wa umma.

“Heshima iliyokuzwa ni ya woga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ambaye alikuwa ukimgusa sharubu anakurarua. Lakini hata hivyo hatukukua kivile, heshima inayotakiwa iwe ya moyoni, kila mmoja aheshimu mstari wa mwenzie, hicho ndicho tunachokosa Serikalini.

“Kila siku unasikia Waziri kakwaruzana na Katibu…upande wetu tunaenda kuimarisha Chuo cha Utumishi na Chuo cha Uongozi ili kufundisha watu majukumu ya utumishi wa umma, lakini Baraza la Maadili likisimama kwenye sheria na kurekebisha maadili ya watenda kazi wa Tanzania, tutaenda vizuri,"- Rais Samia Suluhu akiwaapisha viongozi watule leo Aprili 2, 2022, Chamwino Ikulu, Dodoma

View attachment 2172747
---

Hakika kila chenye mwanzo lazima kiwe na mwisho.

Kumbe zile sifa za ooo nchi imerudisha heshima kwenye sehemu za kazi ilikuwa ni nidhamu ya uoga tu.

Magufuli alikuwa anawatishia watu na wakawa wanaonyesha heshima ya uoga.
Awamu ya tano waliteseka watu wengi sana🤣🤣
 
Muheshimiwa,kufukuzwa kazi ni sehemu ndogo sana katika utumishi iwezayo kumtokea mfanyakazi.Hatupaswi kuwajenga watumishi kwa fikra za kufukuzwafukuzwa.Bali,wajengewe matumaini ya kudumu,kustawi na kuufurahia utumishi.Kufukuzwa iwe ni kama ajali tu.
Sasa kama mtu hapewi discpline atajifunzaje? Kwahio mule rushwa mdharau wateja hio kwenu ndio upendo au sio yani mjifanyie mnavyotaka mkiwa kazini muda wa kazi mpige soga wateja kitu cha kukamilika siku moja kichukue week sababu boss ana mambo yake hayupo ofisini mda wa kazi?
 
Back
Top Bottom