Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Rais Samia: Awamu ya 5 heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ukimgusa sharubu anakurarua, hatukukua kivile

Huyu ni ndumilakuwili,mbona aku step down

Tuseme tu ukweli umejaribu kwenda kwenye taasisi za serikali ukaona huduma zao zikoje ukifananisha na simba wa chato huduma ilikuaje.

Ameshasema alikuwa hajui wakati ule na sasa ndiyo kagundua kwamba heshima ilikuwa ya kiuoga. Sasa angekuaje bila kuona

Ni bora anaeema ukweli badala ya wengine hapa ambao mnapenda uongo kabla ya 2025 atasema ukweli kwamba chaguzi ilikuwa na wizi mwingi maana ndiyo ukweli huo. Ili akishinda kwa 60% watu wajue kwamba 2020 uchaguzi ulikuwa fake
 

"Tunasifiwa kwamba adjustments [maboresho] tuliyoyafanya awamu ya tano kidogo zimekuza heshima ndani ya utumishi wa umma.

“Heshima iliyokuzwa ni ya woga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ambaye alikuwa ukimgusa sharubu anakurarua. Lakini hata hivyo hatukukua kivile, heshima inayotakiwa iwe ya moyoni, kila mmoja aheshimu mstari wa mwenzie, hicho ndicho tunachokosa Serikalini.

“Kila siku unasikia Waziri kakwaruzana na Katibu…upande wetu tunaenda kuimarisha Chuo cha Utumishi na Chuo cha Uongozi ili kufundisha watu majukumu ya utumishi wa umma, lakini Baraza la Maadili likisimama kwenye sheria na kurekebisha maadili ya watenda kazi wa Tanzania, tutaenda vizuri,"- Rais Samia Suluhu akiwaapisha viongozi watule leo Aprili 2, 2022, Chamwino Ikulu, Dodoma

---

Hakika kila chenye mwanzo lazima kiwe na mwisho.

Kumbe zile sifa za ooo nchi imerudisha heshima kwenye sehemu za kazi ilikuwa ni nidhamu ya uoga tu.

Magufuli alikuwa anawatishia watu na wakawa wanaonyesha heshima ya uoga.
Mama amenena fact. # Kazi iendelee
 
Huyu mama anataka uwachekee watumishi wa umma.

Heshima ya moyoni hiyo haipewe serikalini, hiyo inatolewa nyumbani.

Huyu mama ni kimeo.
Ukisoma na kusikia hizi dots kwa kweli inatia mashaka sana kuhusu mwendazake
 
Tunaomba na wewe utupe Upande wa pili wa SAMIA
... uko sahihi. Kuna wajinga wanalazimisha bango aliloacha Magufuli lisomwe upande mmoja tu; hawataki kabisa upande wa pili wa bango lake uonekane. That's very wrong!
 
Ukweli unauma lakini Rais ni bora anakuwa mkweli. Cha kushangaza bado kuna watu wanataka Raisi naye asiwe mkweli na kuaminisha watu uongo maana siku hizi Watanzania wengine wanapenda uongo kuliko ukweli. Nakushukuru Raisi kwa kuwa mwazi. Wafanyakazi wa Serikali wanatakiwa kutengeneza heshima ya kazi sio kumuogopa Raisi bali utamaduni wa kazi, heshima, kufuata sheria na kutopenda rushwa
Hongera sana kwa comment yenye uweledi.
 
Wakati Jiwe anamtukana JK hadharani mlikuwa wapi
Walishatolewa akili zao hivyo walibakia mazuzu
2022-03-22_23%3A36%3A446.jpg
 
Yesu mwenyewe alitembeza fimbo kwa waliokuwa wanaofanya biashara katika nyumba ya Mungu.Sembuse Magufuli, nendeni Korea mkajifunze walifikaje pale walipo Leo.Hakuna maendeleo bila kufunga mikanda na kuhimiza nidhamu kibabe.RIP papa
 
Tunaomba na wewe utupe Upande wa pili wa SAMIA
... Samia bado anaendelea kutengeneza bango lake; halijakamilika bado. Siku zaja litapaswa kuwekwa hadharani. Muhimu kwake ajitengenezee bango lililo bora.
 
Asante sana, ukimalizana ma marehemu utaanza na wajinga wenzio na hilo lichama la Ndiyoo
 
Kama hao watu hawana hiyo heshima huko moyoni unafanyaje.?
 
Hakika Jiwe alikuwa anaitawala Tanzania kwa mkono wa chuma.
 
Back
Top Bottom