Kulikuwa na nidhamu ya kazi au nidhamu ya kukomoa watu? Au zile propaganda za kuwa hali imebadilika? Kama hali ilikuwa nzuri asingekuwa adui wa vyombo vya habari, yeye kutaka habari anazozipenda tu ndio ziandikwe tungeajua vipi kweli nidhamu au utendaji umeongezeka?
Kuingia mtaani hakuji ghafla, ni jambo linalochukua muda mrefu baada ya ushahidi wa haya tunayoyaandika huku mitandaoni. Yeye alifanya aliyoyafanya kutokana na nafasi yake, lakini hii mitandao ilikuwa haimpi raha hadi kufikia kutaka malaika washuke waifunge. Hukumbuki ni wati wangapi walitekwa, ama kufungwa kutokana na kumkosoa kupitia mitandao? Kama mitandao ilikuwa haimtesi asingefuatilia. Na kwa taarifa yako kwa dunia hii ya kidigitali, mitandao ni sehemu moja wapo ya pressure ya kupata jambo, labda kama ww ni mzee, hivyo njia ujuayo ya pressure kwa watawala ni kuingia mtaani tu.