Rais Samia awasili mkutano wa COP27 Sharm El Sheikh Egypt 2022

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
07 November 2022
Sharm El Sheikh, Egypt

MKUTANO WA COP27 SHARM EL SHEIKH EGYPT 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan pamoja na wakuu wengi wa nchi wapo kuhudhuria Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa Kimataifa wa tabianchi COP27 mwaka huu 2022 unafanyika mjini Sharm el-Sheikh, nchini Misri.

Ajenda kuu ni kunusuru ulimwengu ambapo dunia inashuhudia ongezeko la hali mbaya ya hewa duniani kote, shida ya nishati iliyochochewa na vita vya Ukraine, na takwimu za wanasayansi zinasisitiza kwamba ulimwengu haufanyi vya kutosha kukabiliana na utoaji wa hewa ya kaboni na kulinda mustakabali wa sayari yetu.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa / UN Bw. General António Guterres amepeleka ujumbe kwa dunia kuwa mpaka sasa ktk mapambano ya kunusuru uhai wetu, tunaelekea kushindwa.
António Guterres - “We are on a highway to climate hell with our foot on the accelerator.”
Katibu mkuu wa UN Bw. António Guterres anaongeza tupo katika spidi kali barabara kuu kuelekea mazingira ya hali ya hewa ya kuzimu huku tukikandamiza vikali accelerator ya mwendo wa gari . Maneno hayo mazito yanaashiria kuwa inabidi dunia kuchukua hatua za ziada kupunguza uharibifu wa mazingira unaoleta mabadiliko ya tabia nchi .

Rais Abdel Fattah El-Sisi wa Egypt nchi ambayo imekuwa mwenyeji wa mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa TabiaNchi amesisitiza kuwa dunia yote inawaangalia viongozi wanaohudhuria mkutano huo waje na mkakati unaoweza kukabiliana na tishio la mabadiliko la tabianchi.

United Nations Secretary General António Guterres' at the Opening Ceremony of the World Leaders Summit at COP27. Source : UN Climate Change

Mkutano huu utakuwa na vikao vingi vya wakuu wa nchi kukubaliana utekelezaji wa mkakati wa makubaliano ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia-nchi, usipozingatiwa basi unaotishia uwepo wa maisha ya binadamu, ekolojia na viumbe duniani

Angekuwa ni Kiongozi anaye jitambua, angeahirisha kuhudhuria huo mkutano na hivyo kurejea nyumbani mara moja, ili kuungana na wananchi wake kuomboleza vifo vya wapendwa wao.

Ila ndiyo hivyo tena! Uchungu atautoa wapi! Kwanza ameupata huo unanihii wenyewe kupitia mgongo wa katiba mbovu! Mbaya zaidi ana asili ya nchi nyingine ya Visiwa! Haishangazi kumuachia PM wake, na yeye kwenda kuputanga kama ilivyo desturi yake!
 
By the way makamu wa Raisi yuko wapi vile ?
 
Kongamano La COP 27, Rais William Ruto wa Kenya kuwakilisha yafuatayo:

Mkutano Wa 27 Wa Umoja Wa Mataifa Kuhusu Mabadiliko Ya Tabia Nchi (COP 27) Unaendelea Mjini Sharm El Sheikh Misri.

Kwa Mara Ya Kwanza Ajenda Ya Fedha Za Fidia Ya Madhara Yanayosababishwa Na Mabadiliko Ya Tabia Nchi Itajadiliwa Kwenye Mkutano.

Kenya Inawakilishwa Na Rais William Ruto mwenyekiti wa kamati ya marais wa Afrika atotoa taarifa mbili moja inayohusu Afrika na nyingine ni ya Kenya inayokabiliwa na ukame mkali uliosababishwa na mabadiliko ya tabianchi

Source : Ebru TV Kenya,
 
Angekuwa ni Kiongozi anaye jitambua, angeahirisha kuhudhuria huo mkutano na hivyo kurejea nyumbani mara moja, ili kuungana na wananchi wake kuomboleza vifo vya wapendwa wao.

Ila ndiyo hivyo tena! Uchungu atautoa wapi! Kwanza ameupata huo unanihii wenyewe kupitia mgongo wa katiba mbovu! Mbaya zaidi ana asili ya nchi nyingine ya Visiwa! Haishangazi kumuachia PM wake, na yeye kwenda kuputanga kama ilivyo desturi yake!
Aise umeandika kwa uchungu sana!
 
Mama aungerudi Home uje tujadiliane Namna Ya kuunda Kikosi Cha kuokoa watu..Huko tutaenda hata Mwakani...Hili suala la Precision limeleta Taharuki kubwa
 
07 November 2022
Sharm El Sheikh, Egypt

MKUTANO WA COP27 SHARM EL SHEIKH EGYPT 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan pamoja na wakuu wengi wa nchi wapo kuhudhuria Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa Kimataifa wa tabianchi COP27 mwaka huu 2022 unafanyika mjini Sharm el-Sheikh, nchini Misri.

Ajenda kuu ni kunusuru ulimwengu ambapo dunia inashuhudia ongezeko la hali mbaya ya hewa duniani kote, shida ya nishati iliyochochewa na vita vya Ukraine, na takwimu za wanasayansi zinasisitiza kwamba ulimwengu haufanyi vya kutosha kukabiliana na utoaji wa hewa ya kaboni na kulinda mustakabali wa sayari yetu.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa / UN Bw. General António Guterres amepeleka ujumbe kwa dunia kuwa mpaka sasa ktk mapambano ya kunusuru uhai wetu, tunaelekea kushindwa.

Katibu mkuu wa UN Bw. António Guterres anaongeza tupo katika spidi kali barabara kuu kuelekea mazingira ya hali ya hewa ya kuzimu huku tukikandamiza vikali accelerator ya mwendo wa gari . Maneno hayo mazito yanaashiria kuwa inabidi dunia kuchukua hatua za ziada kupunguza uharibifu wa mazingira unaoleta mabadiliko ya tabia nchi .

Rais Abdel Fattah El-Sisi wa Egypt nchi ambayo imekuwa mwenyeji wa mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa TabiaNchi amesisitiza kuwa dunia yote inawaangalia viongozi wanaohudhuria mkutano huo waje na mkakati unaoweza kukabiliana na tishio la mabadiliko la tabianchi.

Mkutano huu utakuwa na vikao vingi vya wakuu wa nchi kukubaliana utekelezaji wa mkakati wa makubaliano ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia-nchi, usipozingatiwa basi unaotishia uwepo wa maisha ya binadamu, ekolojia na viumbe duniani

Kuna game ya yanga Tunisia.. apitie na hapo akawasupport vijana wa jangwani ili aendelee kuupiga mwingi...
 
Tukiwambia nchi inajiongoza muwe mnaelewa sasa sio mnapinga tu na kusema anaupiga mwingi.
 
Back
Top Bottom