Rais Samia awasili Saudi Arabia kushiriki mkutano unaozikutanisha nchi za Afrika na Saudi Arabia kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano

Rais Samia awasili Saudi Arabia kushiriki mkutano unaozikutanisha nchi za Afrika na Saudi Arabia kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano

Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania,mama wa shoka,chuma cha reli, jasiri muongoza njia,shujaa wa Afrika,simba wa nyika amewasili salama nchini saudi Arabia ambako atashiriki mkutano unaozikutanisha nchi za Afrika na Saudi Arabia utakao fanyika November 10 mjini Riyadh,unaoangazia kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano katika sekta za biashara,kilimo,utalii,nishati,uwekezaji na madini.

Ikumbukwe na kueleweka ya kuwa mikutano ya aina hii ni muhimu kwa kuwa inawakutanisha wafanyabishara na wawekezaji wakubwa sana katika Secta hizo tajwa,ambapo ni fursa nzuri kwetu kama Taifa kupata wawekezaji wenye tija na manufaa kwa maslahi mapana ya Taifa letu na ustawi wa watanzania.

Ikumbukwe kuwa fursa zinatafutwa na kila mtu ,hivyo ukikaa tu pasipo kuzitafuta na kuzivutia nchini mwako usifikiri zitakuja tu zenyewe kana kwamba Tanzania tupo pekee yetu au tunavitu vya kipekee ambavyo havipo kwingineko. Ni kupitia fursa hizo ambapo tutatengeneza fursa za ajira kwa vijana, maendeleo ya viwanda,kilimo,utalii, uchumi,kuongeza mapato na kupanua wigo wa kodi.

Hakuna nchi isiyotaka au kuhitaji wawekezaji wakubwa.kila nchi inahitaji wawekezaji na ndio maana tuna ona kila nchi ikijaribu kuweka sera na sheria zitakazovutia wawekezaji wengi ,huku ikilinda na kuhakikishia kuwa wawekezaji wanaokuja ni wenye tija ,kwa kusaini mikataba yenye matokeo chanya yenye kuzingatia maslahi ya Taifa na usalama wake,yenye kuzingatia utamaduni wetu na uwekezaji usio pora uhuru wa Taifa letu lakini ambayo haitaliumiza Taifa wala kuleta maumivu kwa kizazi cha sasa na kizazi kijacho .

Kikubwa watanzania tuendelee kuchangamkia fursa ambazo mh Rais anazileta hapa Nchini.lakini pia serikali yetu ihakikishe ya kuwa kila itakapoweka wino wake kusaini mkataba wa aina yoyote ile basi uwe ni mkataba ambao hata vizazi vijavyo baada ya miaka mingi mbele vikija kuusoma vitikise kichwa kwa Tabasamu na kusema kuwa kwa hakika mkataba huu ulisainiwa na wazalendo wa kweli na wenye upendo na Taifa letu na haya ndio matunda yake.

Serikali ihakikishe kwa kila namna wafanyabiashara wetu hapa nchini wanapata nafasi ya kushirikiana na wawekezaji wa nje ili hata siku wageni wakitaka kuondoka basi tusiteteleke na tubakiwe na ujuzi na maarifa ya namna ya uendeshaji.tuzoe fursa zote popote pale Duniani zenye kulifaidisha Taifa na zile zenye kulinyonya Taifa tuziache na kuzipa kisogo.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Mkuu hizo sifa zote za bi samia????
Siku hizi anaitwa simba wa nyika????
 
Ndiyo hivyo....si mnajua ukioa mzaramo lazima ukubali zile safari zake za kwenda kwao ngomani kila uchao....hawa watu wa pwani ni watu wa shughuli na vitu laini laini...kama shughuli haipo nyumbani itatafutwa popote ilipo.
Mzee wa Msoga mpaka aliitwa Vasco da gama.
Huyu ndiyo kwanza anaanza
 
Awamu ya arabuni hii.
Hii ni awamu ya maendeleo kwa Taifa letu ndio maana unaona chini ya uongozi wa Rais samia tumefanikiwa kupata mafanikio katika sekta zote.ndio maana uchumi wetu unaendelea kufanya vizuri,mzunguko wa fedha mitaani ni wenye afya,fursa za ajira kwa ajira zinaendelea kuongezeka kila uchwao pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo inaendelea kuchipuka Nchini
 
Ni lini rais samia ataalika mataifa ya nje yaje tanzania kama huo mkutano wa saudia kumbuka sisi ni matajiri na tuna fursa na raslmali nyingi ili waje kuwekeza na ikibidi tuwakopeshe.
Kwa Uchumi gani wa Mataifa kujikisanya Kwa Ajili ya Tanzania?

Watakuja kama Kiongozi mmja mmja kama ambavyo wamekuwa wanakuja.

Saudia ndio Largest Economy sio tuu ya Waarabu Bali the Middle East yote.
 
Hii ni awamu ya maendeleo kwa Taifa letu ndio maana unaona chini ya uongozi wa Rais samia tumefanikiwa kupata mafanikio katika sekta zote.ndio maana uchumi wetu unaendelea kufanya vizuri,mzunguko wa fedha mitaani ni wenye afya,fursa za ajira kwa ajira zinaendelea kuongezeka kila uchwao pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo inaendelea kuchipuka Nchini
Malipo yako kwa hii comment mkuu!!
 
Ila huyu Mama kuna nchi hajaenda?
Kwa hiyo unataka alifungie Taifa letu chumbani?au unafikiri Tanzania ni kisiwa? Kwani kuna mipaka ambako inatakiwa asiende kuliwakilisha Taifa letu? Kwani umesikia kuna vikwazo vya aina yoyote ile ambavyo tumewekewa kama nchi kwa Rais wetu kutokwenda sehemu fulani?
 
Back
Top Bottom