Rais Samia awasilisha Hati ya dharura Bungeni

Rais Samia awasilisha Hati ya dharura Bungeni

Wakati ana saini alikuwa amesinzia? Mwingulu atammaliza huyu bibi
Hiyo sheria alipitisha mungu wenu wa Chatttle, Rais wa Sasa kwakuwa muungwana,sheria zote kandamizi zakuwaumiza wananchi anazipiga chini,

Sasa unavyosema Mwigulu atammaliza ammalizaje kilaza wewe!!
 
Hiyo sheria alipitisha mungu wenu wa Chatttle, Rais wa Sasa kwakuwa muungwana,sheria zote kandamizi zakuwaumiza wananchi anazipiga chini,

Sasa unavyosema Mwigulu atammaliza ammalizaje kilaza wewe!!
Tozo kwenye miamala imeanzishwa na nani?
 
Naunga mkono hoja


Umaskini mwingi uko vijijini wakati wao ndio wanaongoza kuleta pesa za kigeni kwa kuuza mazao ya biashara tunauza nje mazao kwa hela za kigeni wao wanapewa vihela vya Tanzania napendekeza wanunuzi wote wauza nje wawalipe wakulima kwa hela za kigeni kwenye akaunti zao kwa kila kilo ya zao

Tozo zifutwe na ruzuku kwa wakulima zitolewe ku stimulate rural economy ili kuzuia pia migration ya vijana kukimbia vijiji kwenda mijini kuwa machinga
 
Bunge kama mdoli yani. Serikali inapeleka mswada usiofaa unapitishwa. Baadae serikali ile ile ndani ya miezi miwili mitatu inapeleka mswada wa kubatilisha sheria ile ile bunge linapitisha. Hapa kuna bunge au bange?
 
Ilitakiwa iachwe iendelee ukizingatia asilimia 2 ambayo inazidiwa na kodi nyingine kibao kuanzia payee mpaka ya tozo za simu pia kiasi kidogo kwa wakulima ambao ndio uti wetu wa mgongo na hakika hakiwezi kuwashinda ukizingatia wanapewa upendeleo mwingine kwenye pembejeo na nyenzo nyingine za kilimo ndo inabidi wachangie pakubwa kwenye maendeleo ya nchi yetu kuliko kuwawekea wafanyabiashara asilimia 18 peke yao ilhali wao sio uti wa mgongo wa taifa letu......


ni kusema kuwa kuwaachia wafanyabiashara pekee jukumu la kuleta na kuhudumia maendeleo ya nchi ni mzigo mkubwa na tutabaki hapa kwenye kutegemea wafadhili daima dumu
 
Back
Top Bottom