Rais Samia awasilisha Hati ya dharura Bungeni

Rais Samia awasilisha Hati ya dharura Bungeni

Wakulima wetu watapata unafuu, maana hiyo tozo ya 2% ilikuwa balaa, bei yenyewe ya mbolea haishikiki. Mtu kalima, kaweka mbolea, kavuna, unampiga tena 2% hii ilikuwa mbaya sana. Hongera Mama Samia.

Ila juzi tu walipitisha hii sheria, leo inaenda kufutwa, kuna wabunge walilala hii sheria ikiwa inapitishwa. Aibu kubwa kabisa.
 
M
Mchakato wa nini? Maendeleo au?

Anyway ngoja niamini kwamba ni mchakato wa maendeleo.
Sasa kama ni mchakato wa maendeleo mbona hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani? JPM si ndiyo alikuwa anasisitiza mchakato wa haraka haraka wa maendeleo ambao ndiyo ulikuja kutafsirika kama ni udikteta, upigaji, mabavu, maonevu, uvunjifu wa sheria... SSH alipoingia akapindua meza kwa kusisitiza uzingatiaji wa sheria za nchi, sasa tena leo tumebadilika tunarudi kwenye chorus ile ile ya JPM; kwa kupeleka hati ya dharura Bungeni ya kutaka mchakato uende haraka haraka? Baghosha!

JPM Fast-track Slogans:
1. Ni heri ufanye haraka ukosee kuliko kutofanya kabisa au kuchelewa kufanya maamuzi/utekelezaji Magufuli, J.P.
2. Muda hautusubiri! Wananchi wanataka matokeo/maendeleo Magufuli, J.P.
3. Tusipofanya leo nani atakuja kufanya? Magufuli, J.P.
4. Kazi ifanyike usiku na mchana ili kukabidhi mradi ndani ya muda wa mkataba Magufuli, J.P.
5. Natoa siku 7 Shule ya Msingi King'ong'o ikamilike Magufuli, J.P.
5. Natoa nyongeza ya muda hadi Disemba mradi wa Machinjio ya kisasa ya Vingunguti ukamilike, hakuna muda wa nyongeza
ehiiiii.... Magufuli, J.P

Nukuu zisizo rasmi.
mama alibadilisha kidogo, tukasema hatutaki,
Tunataka vile jpm alikuwa akifanya, sasa ndio tunarudi huko wengine wanalalamika
So hatuezi kuridhisha wote
Ngoja tu tuendelee
Ikiuma sana tutasema
 
Huko nchi ya ushelisheli unatengeneza sheria mbaya ya tozo kisha unaiondoa kwa hati ya dharura bungeni ili uonekane kuwa ni Rais bora kwa wananchi kumbe ni Paka pori fulani tu ambalo limepata urais kwa zali.
Mkuu,
Harmonize your post with your signature (I have decided to stick with love, hate is too great a burden to bear!) they are in conflict!
 
Zama za kale ndugai alitamba, kua bungee likiwa la kijani tupuu, watafanya watakavyo sasa tunayaonaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Miswada mingapi hupitishwa bungeni na ikarudishwa tena kurekebishwa? Tena worse enough ndani ya muda mfupi. Mswada umepitishwa kwenye la budget la mwaka huu. Wananchi tunaolipa gharama za wabunge wetu mle mjengoni tuna wasiwasi; ama miswada hupita wabunge wengi wanasinzia, hawapo bungeni au watoro NA au wabunge wetu wanakosa umakini (bunge dhaifu). Na hii ni mara ya kwanza tangu bunge la vyama vingi lianze tunashuhidia bunge likiwa na sehemu kubwa ya wabunge toka chama kimoja. Naamini kama Bunge lingekuwa lina wabunge toka vyama mbalimbali (mfano tumewamic sana kina Zitto, Mbatia, Mbowe na macovid-19 kabla hawasilimishwa kujiunga na CCM).
 
Hahahaaa... can you dare C-19 that much? What will you call the 14 from CUF?
 
Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kuanza kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia mbili kwa mazao nchini.
Mazao nilime mimi, pembejeo zote nijitegemee, viatilifu vyote juu yangu, mbolea ninunue mfuko wa 50 kgs 110,000, nipalilie, nivune afu nikiuza ndo mje mchukue 2% kweli jamani ?
 
Kwa hiyo mkuu unataka niwapetipeti walioingia madarakani kwa wizi wa kura?
View attachment 2005592
Hahahahaaa.. SSH hajaiba kura mkuu, msubirie 2025-2030-2035 ndiyo tuone tutamtathminije kwenye usalama/ulinzi wa kura. By the way, Mbowe aliishasema CDM haitagombea, sasa hao waliobaki wanamuweza mama kweli ukipiga hesabu vzr mkuu?
 
Mazao nilime mimi, pembejeo zote nijitegemee, viatilifu vyote juu yangu, mbolea ninunue mfuko wa 50 kgs 110,000, nipalilie, nivune afu nikiuza ndo mje mchukue 2% kweli jamani ?
Mkuu,
Mbona hiyo tone yako kama ya JPM vile?
 
Back
Top Bottom