Rais Samia awatumbua Wakurugenzi wa Halmashauri wanne kwa ubadhirifu wa Fedha zikiwemo za UVIKO-19

Hao kosa lao itakuwa wamekula wakavimbiwa, Rais hapendi hilo anataka ule kwa kiasi.

Huyo mkurugenzi wa Iringa sio yule alieshutumiwa kwa ubakaji siku chache zilizopita? kama ndie akapumzike tu, yeye alikuwa hachagui vyakula anabugia chochote.
Ndio yeye
 
Hawapiiii kosa lao ni kula wakati wao siyo VIP WA TEAM MSOGA .
 
Anatumbuliwaje mtu kwa sababu tu ya tuhuma? Je tuhuma zikishindwa kuthobitishwa? Namkumbuka yule Mkurugenzi aliyechongewa na mbunge wake kuwa kajinunulia Vieiti kinyume na utaratibu! Mwisho wa siku ikagundulika kuwa alikuwa na baraka zote zilizotakiwa. Utumbuaji wa namna hii inawapa nguvu wale wanaopenda kuchonganisha na kuwaharibia watu.

Amandla...
Ameshafanya preliminary investigation na majibu yamethibitisha tuhuma ni za kweli. DED wa Geita vijijini uchunguzi bado unaendelea. Mama hakurupuki, anafanya uchunguzi kwanza.
 
Mbeya kwaspwika watu wanatafuna uviko monei... Kwani spwika anasemaje???
Ila tuache masihara wanawake wamesheheni kweli mkurugenzi Tantrade ndoyule?? Amewahi Fanya biashara yyte kweli?? Hayabana!!!
 
Ameshafanya preliminary investigation na majibu yamethibitisha tuhuma ni za kweli. DED wa Geita vijijini uchunguzi bado unaendelea. Mama hakurupuki, anafanya uchunguzi kwanza.
Preliminary investigation hata siku moja haikupi majibu ya mwisho. Inachofanya ni kuthibitisha haja ya kufanya uchunguzi kamili. Kumtumbua mtu kwa sababu uliyosema ni kumuonea.

Amandla...
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa njiani kutoka Mwanza kwenda mkoani Mara, leo Ijumaa ametangaza kutengua uteuzi wa wakurugenzi wanne wa Halmashauri ya Buchosha, Iringa, Mbeya na Singida Mjini baada ya kubainika kutumia vibaya fedha za UVIKO-19.

---

Rais Samia Suluhu Hassan amewatengua Wakurugenzi wa Halmashauri nne kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha na amesema Mkurugenzi wa Geita kama akikutwa na ubadhirifu pia tataenguliwa

Wakurugenzi waliotenguliwa ni Mkurugenzi wa Buchosa, Iringa, Mbeya Mjini na Singida Mjini. Utenguzi umefanyika baada ya Waziri wa OR-TAMISEMI Innocent Bashungwa kusema wanafanya uchunguzi wa haraka kwa wakurugenzi walioripotiwa kufanya ubadhirifu

Halmashauri ya Buchosa ilikuwa chini ya Mkurugenzi Paulo Malala, Mkurugenzi wa Iringa ni Limbe B. Limbe, Mkurugenzi wa Singida Mjini ni Zefrin Kimolo Lubuva, na Mbeya Mjini ni Amede E.A Ngwanidako
Mbona wote wa dini Moja 🤣🤣🤣🤣
 
Wakati anawateua watu walipiga kelele kuhusu teuzi za makada wa CCM, wengine watoto walio hitimu vyuo jana yake. Wengine vibinti toka visiwani kuwa wakurugenzi bara!
 
Kwa namna ya pekee kabisa napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuchukua hatua kwa Wakurugenzi wanne waliofanya ubadhirifu wa fedha za miradi ya COVID-19, huku akimuweka kipolo Mkurugenzi wa Geita vijijini.

Kwa Mkurugenzi wa Geita vijijini tuhuma zake zi wazi kwani zimeshasemwa kwa ufasaha na mbunge wa jimbo hilo mhe, Joseph Kasheku Musukuma.

Tujipe muda kuona hatua zipi zitachukuliwa japo kuna za chini chini zinasema yeye anabebwa na mtu mkubwa huko juu tujipe muda tuone.

Lakini nipende kutoa ombi kwa mhe,Rais hawa watu hawapaswi kuishia kutolewa kazini tu bali wanapaswa kufikishwa mahakamani kwani wametuibia sisi Watanzania.

Mwisho nitoe pongezi pia kwa mhe Rais kwa Kutoa maelekezo kwa waziri mkuu kuunda tume kwa ajili ya kuchunguza mauaji huko Mtwara.
Asante sana mhe Rais kazi iendelee.
 
Wao hawahusiki na yale maelekezo ya kujipimia............
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa njiani kutoka Mwanza kwenda mkoani Mara, leo Ijumaa ametangaza kutengua uteuzi wa wakurugenzi wanne wa Halmashauri ya Buchosha, Iringa, Mbeya na Singida Mjini baada ya kubainika kutumia vibaya fedha za UVIKO-19.

---

Rais Samia Suluhu Hassan amewatengua Wakurugenzi wa Halmashauri nne kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha na amesema Mkurugenzi wa Geita kama akikutwa na ubadhirifu pia tataenguliwa

Wakurugenzi waliotenguliwa ni Mkurugenzi wa Buchosa, Iringa, Mbeya Mjini na Singida Mjini. Utenguzi umefanyika baada ya Waziri wa OR-TAMISEMI Innocent Bashungwa kusema wanafanya uchunguzi wa haraka kwa wakurugenzi walioripotiwa kufanya ubadhirifu

Halmashauri ya Buchosa ilikuwa chini ya Mkurugenzi Paulo Malala, Mkurugenzi wa Iringa ni Limbe B. Limbe, Mkurugenzi wa Singida Mjini ni Zefrin Kimolo Lubuva, na Mbeya Mjini ni Amede E.A Ngwanidako

Mwana Ilboru mwenzangu Zefrin Kimolo Lubuva kapigwa chini. Nilimwambia aachane na siasa atafute kazi nyingine au afanye biashara. Jafo alikuwa anamsumbua wakati wa nyuma nikajua hana muda
 
Back
Top Bottom