Pre GE2025 Rais Samia awekwe kwenye Noti/Sarafu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

More Chances

Senior Member
Joined
Jun 24, 2022
Posts
151
Reaction score
344

Tanzania ni moja ya nchi chache zenye bahati ya kupata Rais mwanamke.

Dr Samia kukalia kiti cha Urais kumebadilisha mtazamo wa wa Africa wengi kuweza kuwaamini wanawake.

Tangu mama ameshika nchi uchumi umekuwa kwa kasi na mambo yanaenda. Je, hamuoni kuwa ni sahihi mama awekwe kwenye noti yetu ili akumbukwe vizazi na vizazi?

Nawasilisha.
 
Hapana, ameuza bandari na mbuga kwa waarabu, itakuwa ni laana kumuweka kwenye sarafu
Hajauza bhana amewapa waendeshe kisasa zaidi ili kuboresha utendaji wa bandari.
mbn Dp world inaendesha bandari za nchi nyingi tu
 
Hata mumpambe vipi kwetu Tanganyika huyo ni kama Julius Von Soden. Muda wake ukifika tutamsahau kabisa.
Hana tofauti na magavana wa Kijerumani au Kiingereza waliotawala Tanganyika

Kumbuka hata Malkia alikuwa kwenye coin za Tanganyika. Ila kwa sasa ziko wapi hizo coin?
 
Sio muhimu
 
Mama anaongoza vzuri sana sema tu watu msha develop Negativity
ndio maana mnaongozwa na Chuki
 
Yeye si Rais wa kwanza Africa alikuwepo Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia, Akaja Joyce Banda wa Malawi. Na wapo wa nyazifa za Urais kama Sahel Wok Zewde wa Ethiopia nk. Tumeisha jiwekea utaratibu kuwa baada ya Nyerere kuwa kwenye noti ya elfu moja. Hakuna mwingine mwingine ataka yewekwa kwenye noti zetu. Kuna Marais wamefanya makubwa kwa nchi hii na hawakupewa fursa hiyo seuse Mama. Atulie amepewa nafasi adhim ya kutawala hii Tanganyika inatosha
 
Sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…