#COVID19 Rais Samia azindua Chanjo ya COVID-19 na kuchanjwa. Asema hawezi kujipeleka kwenye Kifo
SAUTI YA VITA, NI SAUTI YA VITA YA KORONA Naa Joseph #Yona

Miaka ya Tisini naa nikiwa Shule ya Msingi tulizoea katika nyimbo za mchaka mchaka tulipenda kuimba wimbo mmoja nilikuwa naupenda sana na mpaka leo bado nakumbuka.

#WIMBO
SAUTI YA VITA INAPORINDIMA, ASKARI WOOTE MATUMBO HUWA JOTO, LAKINI MASHUJAA HUWA YU TAYARI KUFA NA KUPONA APATE USHINDIIII, WATANZANIA TUMO KATIKA VITA..................OK TUUITE VITA YA KORONA.

Jana tarehe 28/07/2021 ilikuwa siku ya kusisimua kwa watanzania, siku ambayo Shujaa, Amiri Jeshi Mkuu, Mfariji mkuu wa nchi, Mkuu wa nchi, Mwenyekiti wa Ccm taifa, Mama yetu, Bibi wa wanetu, Mtanzania namba moja Opppppppp! Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania #Samia Suluhu Hassan aliamua kwa dhamira na kujiridhisha kupata chanjo ya Korona na vyombo vyake vyote vya ulinzi na usalama wa nchi.

Huko nyuma niliwahi sema Mama #Samia ni Mama na siku zote mama hawezi wapa wanae Sumu, nasema SAUTI YA VITA IMERINDIMA, NA SHUJAA WETU NAMBA MOJA RAIS #SAMIA SULUHU HASSAN AMEONESHA NJIA, Hivyo chanjo iko sahihi na kubwa tumechanjwa chanjo nyingi huko nyuma tukiwa wadogo na sasa watoto wetu wana chanjo nyingi sana, nasema kama mzungu angekuwa na nia mbaya na Afrika angetengeneza Coronavirus ya Afrika tu.
Kila mtu ana aproach yake ya kuyakabili matatizo, hiyo nayo ni Aproach ya Mama, twende Mbele tuimalize Korona.

Mwisho, Njia za kuikabili Korona ziko nyingi na njia ni njia, kuna njia ya kupeana ujasiri kuwa hakuna Korona huku wataalamu wakiwa wamejifungia ndani kusaka Suluhu njia ni nzuri kwa watu wenye umri wa Immunity nyingiii na strong, ila wale wenye umri bye bye hulambwa tu, na kuna njia ya Chanjo hii huokoa woote wenye umri bye bye na Wenye Immunity strong, #Yona Nasema Twende na Mama #Samia,
IMG_20210729_194006_688.jpg
 
Ila watu mmejipa matumaini makubwa sana na hizi chanjo.
Kama tulijipa matumaini na mifukizo ya kila aina ya mmea bila majaribio yoyote kwanini tusiamini za mzungu zilizojaribiwa🤣
 
Kama tulijipa matumaini na mifukizo ya kila aina ya mmea bila majaribio yoyote kwanini tusiamini za mzungu zilizojaribiwa🤣
Binafsi sijawahi kujifukiza ila nachojua ilikuwa inatumika kama tiba asili na tukizungumzia tiba asili zipo ambazo zimefanyiwa chunguzi za kisayansi na nyingi hazijafanyiwa uchunguzi wa kisayansi. Ila kuhusu chanjo imekuwa ni jambo lenye kuzungumziwa sana dunia kote na ukweli ni kwamba bado ipo kwenye majaribio.
 
SAUTI YA VITA, NI SAUTI YA VITA YA KORONA Naa Joseph #Yona

Miaka ya Tisini naa nikiwa Shule ya Msingi tulizoea katika nyimbo za mchaka mchaka tulipenda kuimba wimbo mmoja nilikuwa naupenda sana na mpaka leo bado nakumbuka.

#WIMBO
SAUTI YA VITA INAPORINDIMA, ASKARI WOOTE MATUMBO HUWA JOTO, LAKINI MASHUJAA HUWA YU TAYARI KUFA NA KUPONA APATE USHINDIIII, WATANZANIA TUMO KATIKA VITA..................OK TUUITE VITA YA KORONA
.

Jana tarehe 28/07/2021 ilikuwa siku ya kusisimua kwa watanzania, siku ambayo Shujaa, Amiri Jeshi Mkuu, Mfariji mkuu wa nchi, Mkuu wa nchi, Mwenyekiti wa Ccm taifa, Mama yetu, Bibi wa wanetu, Mtanzania namba moja Opppppppp! Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania #Samia Suluhu Hassan aliamua kwa dhamira na kujiridhisha kupata chanjo ya Korona na vyombo vyake vyote vya ulinzi na usalama wa nchi.

Huko nyuma niliwahi sema Mama #Samia ni Mama na siku zote mama hawezi wapa wanae Sumu, nasema SAUTI YA VITA IMERINDIMA, NA SHUJAA WETU NAMBA MOJA RAIS #SAMIA SULUHU HASSAN AMEONESHA NJIA, Hivyo chanjo iko sahihi na kubwa tumechanjwa chanjo nyingi huko nyuma tukiwa wadogo na sasa watoto wetu wana chanjo nyingi sana, nasema kama mzungu angekuwa na nia mbaya na Afrika angetengeneza Coronavirus ya Afrika tu.
Kila mtu ana aproach yake ya kuyakabili matatizo, hiyo nayo ni Aproach ya Mama, twende Mbele tuimalize Korona.

Mwisho, Njia za kuikabili Korona ziko nyingi na njia ni njia, kuna njia ya kupeana ujasiri kuwa hakuna Korona huku wataalamu wakiwa wamejifungia ndani kusaka Suluhu njia ni nzuri kwa watu wenye umri wa Immunity nyingiii na strong, ila wale wenye umri bye bye hulambwa tu, na kuna njia ya Chanjo hii huokoa woote wenye umri bye bye na Wenye Immunity strong, #Yona Nasema Twende na Mama #Samia,View attachment 1873245
Utumbo wa Karne.
 
Lini chanjo ikawa kwa kusaini kwanza kana kwamba unaingia chumba cha upasuaji ambako kutoka salama ni pata potea? Kumbe wanajua chanjo kutoka salama ni pata potea! Huwa tunachoma chanjo za TT hakuna kusaini, tunachanja watoto kliniki hakuna kusaini, chanjo ya mabusha hakuna kusaini kulikoni corona? Jibu ni rahisi! Chanjo ya corona ni hatari! Chochote kinaweza kutokea! Kila mtu anakwepa kuwajjbika hivyo zigo anaachiwa mchanjwaji! Aliyekuchanja anakuruka kimanga! Katika hili mimi naungana na msemo wa hekima wa Kikwete: Akili ya kuambiwa changanya na ya kwako!
 
1627614571591.png
hawa viongozi wetu vipi? Wazee ilibidi ndiyo waanze kupewa, sasa naona ni vigogo tu. shame on you so called leaders. 15 years more of chaos, Mwungano oyeee.
Mbele wabunge watakoma kubadilisha katiba bila kutujulisha sisi.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Vigogo FEKI familia zao wastaafu na familia zao na maccm yoyote.


View attachment 1873612hawa viongozi wetu vipi? Wazee ilibidi ndiyo waanze kupewa, sasa naona ni vigogo tu. shame on you so called leaders. 15 years more of chaos, Mwungano oyeee.
Mbele wabunge watakoma kubadilisha katiba bila kutujulisha sisi.
 
Nn kimekusibu hadi kuomba chanjo?
umeambiwa ni hiyari itakufikia tuu
 
SAUTI YA VITA, NI SAUTI YA VITA YA KORONA Naa Joseph #Yona

Miaka ya Tisini naa nikiwa Shule ya Msingi tulizoea katika nyimbo za mchaka mchaka tulipenda kuimba wimbo mmoja nilikuwa naupenda sana na mpaka leo bado nakumbuka...
Tungojee mabaki ya vigogo wote, watoto wao na familia zao ndio watanzania wengine watachanjwa. Are we 60 milion na tunapewa moja million leo then next month. Hawa viongozi wetu akili zao ni za kuku kabisa. No wonder makao makuu yalipelekwa Dodoma ili wawe karibu na Mirembe Hospital.

These are all morons!! My god 15 years more. Na hawa viongozi wa dini nao watupe msimamo wao, kama wanaruhusu hawa morons kuingia misikitini na makanisani, vipe hiyo inakaaje, wanajua wanavyochezea resources za nchi bila kuogopa Mungu. Tuwapige stop hawa kuswali nao.
 
VCG111341214885.jpg


Serikali ya Tanzania imeidhinisha utaratibu wa kutoa chanjo kwa watu wake, ikiwa ni moja ya hatua za nyongeza za kupambana na janga la COVID-19. Uamuzi huu umefikiwa wakati nchi zote jirani zilitangulia kuidhinisha na zinaendelea kuwapatia chanjo watu wake, na Tanzania kuwa nchi ya mwisho katika eneo la Afrika Mashariki, na Afrika kwa ujumla kuruhusu watu wake kupewa chanjo.

Tayari Zanzibar imeanza kutoa chanjo ya Sinovac, ambayo ni msaada kutoka kwa serikali ya China. Jambo la kutia moyo ni kuwa waziri wa afya wa Zanzibar Bw. Mohammed Mazrui ndio alikuwa mtu wa kwanza kupewa chanjo hiyo, akiwahakikishia wananchi kuwa chanjo hiyo ni salama. Polepole watu wameanza kuelewa na kuamini kuwa chanjo sio njama ya wazungu, bali ni njia ya kupambana na COVID-19.

Rais Samia Suluhu Hassan naye amepewa chanjo hiyo Ikulu na kuwa mtu wa kwanza kwa Tanzania bara kupokea chanjo hiyo baada ya serikali kujiunga na mpango wa COVAX, na kupokea dozi zaidi ya milioni 1 chini ya mpango huo.

Tanzania iligonga vichwa vya habari duniani baada ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo John Magufuli kuonyesha msimamo mkali dhidi ya chanjo, na hatua nyingine za kupambana na janga la COVID-19. Wakati wimbi la kwanza lilipojitokeza hakuna hatua zozote za zuio zilizochukuliwa, barakoa zilipuuzwa, kilichofanyika ni kushauri watu kutumia vitakasa mikono, na kuwahimiza wengine kutumia tiba ya kujifukiza iliyopewa jina la “kupiga nyungu”, na baadaye ilizuia kutoa takwimu za idadi ya watu walioambukizwa na wanaokufa kwa COVID-19, na kuitangazia dunia kuwa Mungu ameondoa virusi vya Corona Tanzania.

Hata hivyo Sayansi ni sayansi, ukweli ni kwamba watanzania waliendelea kuambukizwa na kufa. Baada ya Bw. Magufuli kuaga dunia, serikali ya Rais Samia Suluhu ilijikuta njia panda. Kwanza iliendelea kulaumiwa vikali na jumuiya ya kimataifa kwa kutofuata mbinu za kisayansi zinazotambuliwa na Shirika la Afya Duniani WHO na ambazo hata wataalamu wa afya wa Tanzania na wanasayansi wa Tanzania wanazikubali. Kwa upande mwingine, kutokana na mtangulizi wake kuwaaminisha watanzania wengine kuwa barakoa si salama na chanjo si nzuri, watanzania wengine wanaendelea kutokuwa na imani hadi sasa na chanjo.

Hata Tanzania ilipojiunga na mpango wa COVAX Juni 15, kulikuwa na mjadala na hofu miongoni mwa watanzania. Waziri wa Afya wa Tanzania Bibi Doroth Gwajima, alisema Tanzania inatakiwa kuchukua hatua polepole kwa kutangulia na kuwaelimisha wananchi. Kwani bado kuna ushawishi mkubwa wa watu wanaopinga njia za kisayansi, ikiwa ni pamoja baadhi ya wanasiasa, watu wa dini, na wengine walioamua kuwa wabishi.

Ni bahati mbaya kuwa maisha ya watanzania yamepotea kutokana na msimamo usio na ushahidi wa kisayansi kuhusu COVID-19. Jambo la kutia moyo ni kuwa sauti za wataalam sasa zimeanza kusikika, na hata mitandao ya kijamii ya Tanzania inaonyesha wanasiasa na wahubiri wanaopotosha wananchi, wakikosolewa.
 
Mama kasema hawezi kujipeleka kwenye kifo hilo tumemwelewa hakuna Shaka.
 
Habari wadau,

Nilikuwa nimelala nimestuka usingizini nasikia chanjo imeingia nchini.

Je, Rais amechanjwa chanjo ipi na wananchi watachanjwa chanjo ipi?

Isije kukawa kuna madaraja au matabaka (classes )katika utoaji chanjo.

IMG_20210730_110054.jpg
 
Back
Top Bottom