#COVID19 Rais Samia azindua Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya COVID-19 Jijini Dodoma

#COVID19 Rais Samia azindua Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya COVID-19 Jijini Dodoma

Hiyo ni kampeni ya chanjo, sasa wataushangaza vipi ulimwengu? Au watachanja nchi nzima siku 1

Mie nasubiria mengineyo, yatokanayo na hotuba ya Mheshimiwa, kuna vitu anaweza kuvisema vinavyogusa maslahi mapana ya taifa.

Hilo ulilolisema hakuna maajabu hapo.
 
Naona sasa tv stion zinakazi sawa na Haji Manara wakati yupo Simba
 
Walishaanza kutapanya pesa za msaada toka kwa Mabeberu kuhusu korona, Naona wameanzisha tamasha ili kuwahadaa mabeberu kuwa pesa walizopata za IMF wanachukua hatua

Danganya toto Jinga


Sasa mbona jambo la kitaifa na la kiserikali limegeuzwa la chama

Haya mambo yanachekesha sana na yanarudisha nyuma sana hamasa na maendeleo

Meza zimewekwa bendera ya CCM na baadhi ya watu wamevaa sare za ccm

Kuna watu wakisikia neno ccm wanazima TV na kuondoka, Hawaitaji porojo na uwongo wa ccm

Unapohimiza mambo ya kitaifa kama chanjo, Kampeni za malaria, Kampeni za watu kuwa matajiri, Au kampeni za elimu yakupasa kusimamia Sera za Taifa

Watu ambao hawana chama ni wengi kuliko wana ccm au Chadema


CCM walisema tuchape kazi Corona hakuna na waliwacheka Chadema waliohimiza kuwa corona ipo na itaondoka na watu ikiwemo viongozi


Leo ccm inapiga kampeni ya chanjo ni wajinga waliopindukia na watu wasiojitambua wanaweza Sikiliza ujinga huu


Nashauri viongozi waombe radhi wananchi kwa kuwajaza upepo kuwa korona hakuna na ni kama mafua ya ndege


Humprey Polepole bado anahubiri hakuna korona na amesimama na msimamo wa ccm


Sasa Je Pesa za IMF zimetumikaje?

Mtuambie pesa mlizopata za IMF mmeajiri madaktari wangapi kama mkataba unavyotaka


CCM wanahubiri mapambano ya corona, Pathetic

CCM mlikuwa wapi mmesubiri mpaka watu wameondoka, Mlihimiza Bunge liendeleee na waliotoka bungeni wakatwe pesa
Binafsi nimezima tv .
Huo ndiyo ukweli
 
Kuna utekelezaji wa ilani. Pia Rais ni Mwenyekiti wa CCM.
Kumbukeni kuwa hao mabeberu waliotoa fungu la mapambano ya covd wana mabalozi wao hapa nchini wanajua kipi kikao cha chama na ipi ni kampeini tokomeza janga
 
Suala hili ni la kitaifa ni kampeni ya maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO - 19.
Sasa mabendera ya CCM yanafanya nini hapo?

Hicho kikao kinaongozwa na rais wa JMT au mwenyekiti wa chama?
 
Back
Top Bottom