#COVID19 Rais Samia azindua Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya COVID-19 Jijini Dodoma

Hiyo ni kampeni ya chanjo, sasa wataushangaza vipi ulimwengu? Au watachanja nchi nzima siku 1

Mie nasubiria mengineyo, yatokanayo na hotuba ya Mheshimiwa, kuna vitu anaweza kuvisema vinavyogusa maslahi mapana ya taifa.

Hilo ulilolisema hakuna maajabu hapo.
 
Naona sasa tv stion zinakazi sawa na Haji Manara wakati yupo Simba
 
Binafsi nimezima tv .
Huo ndiyo ukweli
 
Kuna utekelezaji wa ilani. Pia Rais ni Mwenyekiti wa CCM.
Kumbukeni kuwa hao mabeberu waliotoa fungu la mapambano ya covd wana mabalozi wao hapa nchini wanajua kipi kikao cha chama na ipi ni kampeini tokomeza janga
 
Suala hili ni la kitaifa ni kampeni ya maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO - 19.
Sasa mabendera ya CCM yanafanya nini hapo?

Hicho kikao kinaongozwa na rais wa JMT au mwenyekiti wa chama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…