#COVID19 Rais Samia azindua Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya COVID-19 Jijini Dodoma

#COVID19 Rais Samia azindua Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya COVID-19 Jijini Dodoma

CT scan moja inauzwa dukani dola za kimarekani 1,000,000-7,000,000.....

Leo serikali yetu sikivu inatuletea CT SCAN 72.......

Iko hivi.......

Kila siku kunatokea ajali za PIKIPIKI-BODABODA........vijana wenzetu wanavunjika MIKONO NA MIGUU...mbaya zaidi MAJERAHA VICHWANI(head injuries)....

Sasa unampeleka majeruhi mwenye "HEAD INJURY" na kuambiwa hawana CT-SCAN mpaka MKOANI....😳😳😳

Haya ni MAPINDUZI MAKUBWA 💪🙏👏👏👊👊😍

SIEMPRE JMT
SIEMPRE CCM
 
Hakuna pesa ya bure,fanya Kazi omba tenda utoe jasho ndio upate pesa..Mimi Mgao wangu ni huduma bora..

Imagine ukiwa Nyanda za Juu mkoa wowote ukitaka MRI na CT scan lazima uende Dom au Dar ,,sasa huu upuuzi unakwenda kuisha
😍
 
CT scan moja inauzwa dukani dola za kimarekani 1,000,000-7,000,000.....

Leo serikali yetu sikivu inatuletea CT SCAN 72.......

Iko hivi.......

Kila siku kunatokea ajali za PIKIPIKI-BODABODA........vijana wenzetu wanavunjika MIKONO NA MIGUU...mbaya zaidi MAJERAHA VICHWANI(head injuries)....

Sasa unampeleka majeruhi mwenye "HEAD INJURY" na kuambiwa hawana CT-SCAN mpaka MKOANI....😳😳😳

Haya ni MAPINDUZI MAKUBWA 💪🙏👏👏👊👊😍

SIEMPRE JMT
SIEMPRE CCM
Bila kusahau centers za kufanya communication Ili kusaidiana kusoma vipimo in case hakuna wataalamu wa ku interprete
 
Nice, lakini ungeinvest kwenye kilimo utoe ajira kwa graduates.
Kuna mipango ya mda mfupi,Kati,dharura na mda mrefu..

Tija ya kuanza kuwekeza kwenye kilimo bila kujiandaa ni sawa na kukurupuka na kupoteza pesa.

Afya kwanza ndio msingi wa vyote,kote huko mama atafika ila kwa sasa tuanze na afya kwanza
 
Kuna mipango ya mda mfupi,Kati,dharura na mda mrefu..

Tija ya kuanza kuwekeza kwenye kilimo bila kujiandaa ni sawa na kukurupuka na kupoteza pesa.

Afya kwanza ndio msingi wa vyote,kote huko mama atafika ila kwa sasa tuanze na afya kwanza
mnhh kama kaweza kujiandaa kwa hili why not kilimo?
 
Bora hata angepeleka sasa hakuna hata hospital alikamilisha zaidi ya kujijengea mahekalu na airport awe anashuka ..

Eti alijenga mahakama kubwa,TRA kubwa,Tanesco kubwa na upuuzi mwingine huku watu hawana maji wala shule vituo vya afya vya kutosha
Mungu fundi bhanaa..
 
Hongera Sana mama,.ombi langu Mimi ni kua,kwa kua mpango ni endelevu basi usiishie tu kwenye sekta ya afya ,mwakani wawafikie na wakulima pia.

Kila mtanzania afaidi keki ya taifa
 
Kama umewahi kufanya kazi taasisi za kimataifa
Inauguration ni kitu kinachopewa kipaumbeke na huwa na bajeti yake
Kinachofanyika ni public advocacy ambacho ni kitu muhimu sana
Kila activity huwa na budget cost kwaio wako ndani ya bajeti
Siyo kufanyia vikao vya chama kama wafanyavyo.
 
Inapelekea huu mkutano wa Leo uzinduzi wa kampeni ya maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya uviko 19 umetumia fedha nyingi sana. Nikifuatilia utangulizi wake utangamua Hilo kwa idadi kubwa ya waalikwa
Njia ya upigaji hiyo
 
Hivi kweli cccm wanadhani watanzania vyote vichwa vyetu ni urembo tu si vya kufikiri? Punguzeni huo ujinga wenu japo kdg jamani.
Waache waendelee kujidanganya siku watastuka wapo nje ya jukwaa
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Ndg. Samia Suluhu Hassan akizindua kampeni ya maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO - 19 katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma leo 10 Oktoba 2021.​

Fuatilia matangazo hapa




Dondoo ujio wa Shilingi Trilioni 1.3 kutoka IMF.
1. Kujenga madarasa mapya 15,000 ya sekondari.
2. Kujenga madarasa 3,000 shule za msingi shikizi
3. Kutengeneza madawati 462,795
4. Kumalizia vyuo vya VETA 32
5. Magari 25 ya kuchimba visima vya maji.
6. Mitambo 5 ya kujenga mabwawa ya maji.
7. Kujenga ICU 72
8. Magari ya wagongwa (Ambulance) 395 na ya chanjo 214
9. Mifumo ya Oxygen hospitali 82
10. Mitungi ya gesi 4,640
11. Mitambo ya kuzalisha hewa ya Oksijeni 40.
12. Vitanda vya wagonjwa 2,700
13. Xray za kisasa 85
14. CT- Scan 29
15. MRI hospitali zote za kanda

Rais Samia Suluhu Hassan

Kwenye kipindi cha miezi sita tumeweza kutatua changamoto 11 za Muungano ikiwemo masuala ya usimamizi wa ukokotoaji na ukusanyaji wa kodi za huduma za simu unaofanywa na Mamlaka ya Mapato Zanzibar, Sheria ya Uvuvi kwenye ukanda wa uchumi wa bahari kuu pamoja na suala la ucheleweshaji wa mikataba mbalimbali ya miradi ya maendeleo

Hakuna shaka kutatuliwa changamoto hizo kumeimarisha muungano wetu.

Kwenye hotuba yangu tarehe 22 Aprili nilitaja baadhi ya hatua tulizopanga kuzichukua ili kukuza uchumi ikiwemo kuhakukisha viashiria vyote vya uchumi jumla vinabaki kuwa imara. Kutathmini mifumo, taratibu na viwango vya kodi, kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, kuimarisha ukusanyaji wa mapato. Nfarijika kuwa katika miezi 6 iliyopita, tumetekeleza hayo yote.

Uchumi umeongezeka hadi kufikia asilimia 4.3 ukilinganisha na asilimia 4 kipindi kama hicho mwaka uliopita

Tumedhibiti mfumuko wa bei ambapo umeendelea kuwa na tarakimu moja. Katika kipindi cha mnwezi Aprili hadi Septemba 2021 mfumuko wa bei ulikuwa kwa wastani wa asilimia 4. Hadi mwezi Agosti 2021 akiba ya fedha za kigeni ilifikia dola za Marekani bilioni 5.8 iliyotoshelea kuagiza bidhaa kwa kipindi cha miezi 6 ikilinganishwa na akiba ya dola za Marekani bilioni 4.9 iliyokuwa kipindi kilichopita.

Hali ya ukusanyaji wa mapato inakwenda vyema. Kuanzia Aprili mpaka Septemba tumakusanya trilioni 9, bilioni 905, na mapato yasiyokuwa ya kodi yalikuwa Tshs. Trilioni 1 bilioni 436

Tumrefanikiwa kupata mikopo ya masharti nafuu yenye thamani ya Tsh. Trilioni 1 bilioni 447.

Katika kipindi hicho tumetuliza kilio cha muda mrefu cha kufanya marejesho ya kodi ya ongezeko la thamani, yaani VAT Refund. Kiasi cha bilioni 451 na milioni 300.

Tumeendelea kulipa madeni ya ndani na je. Tumeweza kumaliza uhakiki wa madeni ya ndani yanayofikia shilingi bilioni 439 yanayotokana na madai ya watumishi, wazabuni wakubwa na wadogo, wakandarasi wakubwa, madeni ya huduma za umeme maji na simu kwa taasisi za umma

Madeni yote hayo yameanza kulipwa na yanaendelea kulipwa. Kazi ya uhakiki wa madeni yaliyobaki inaendelea.

Kuhusu uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji na biashara, hatua mbalimbali zimechukuliwa ikiwemo ikiwemo kuondoa urasimu kwenye utoaji wa vibali vya kazi ambapo tumeanzi mfumo wa kielektroniki, yaani e-permit. Mfumo huu umepunguza siku za utoaji vibali kutoka siku 14 hadi siku moja kwa sasa endapo mwombaji atakuwa amekamilisha taratibu zote.

Kama samia ataweza geuza huu mkopo wa imf wa kulazimisha kuwafaidisha mabeberu kua mkopo wa faida kwa maendeleo atakua ameepa kikombe cha uchungu alichoshindwa yesu.
Iko hivi. Imf ni wakopeshaji kwa faida kwa hivyo ni biashara. Makampuni ya magharibu wana bidhaa wameshajipanga WHO wanakwambia lazima ununue na wewe huna pesa. IMF wanakwambia tutakukopesha uende kununua pale ulaya/marekani. Bidhaa hizo wala sio lazima kwa mtazamo wako. Kama hununui utakutana na vikwazo hivi na vile. Unakopa hela zinarudi ulaya nchi inabaki na deni. Nchini kuna vigogo na wafanya biashara na wao wanafaidika kupiga hio hela ya mkopo. ndio mchezo ulivyo😂😂🤣
 
Back
Top Bottom