Rais Samia azindua ugawaji wa vitendea kazi kwa maafisa ugani kilimo. Asema Serikali imeongeza bajeti ya utafiti kutoka Tsh 7.35bn hadi 11bn

Huu mtindo wa ugani haufai, niwa ghali sana na hauleti tija...Wagani walitakiwa kuwa sehemu ya uzalishaki kwenye kilimo hii tumepigwa Africa na kitu kizito ili tusitoke kwenyw hii small holder farming
 
Aache porojo za kiwaki,mfuko wa mbolea 150,000 bado buster na dawa hazishikiki...hui uharo akaongee na ccm wenzake
 
Watu hata hawahitaji hizo ruzuku. Na jambo hilo lilifanyika na kufeli. Wakulima wanataka uhuru zaidi wa kuuza mazao yao. Mapinduzi ya kilimo China yalifikiwa baada ya serikari kuwaruhusu wananchi wao wauze mazao yao kokote watakako.
 
Alisikika mkulima mmoja baada ya kuuza kangomba na kununua heness
Hatutaki ruzuku tunataka mtutolee kodi kwenye kilimo pia mtu achie tuuze kwa uhuru pia samia ajiuzuru atufufulie,jembe letu ,,.
 
Serikali itafute namna ya kuzalisha mbolea ya kutosha tunapoteza pesa nyingi sana kuagiza, sio lazima kiwe kiwanda cha serikali lakini wanaweza kutoa security/dhamana na subsidies nyingine ili watu binafsi wajenge viwanda vya mbolea, ni muhimu sana kwa food safety ya nchi, tunatumia billions kuagiza mchele,ngano , mafuta ya kula etc vitu ambavyo tungeviweza wenyewe ndani ya nchi
 
Kwa hiyo bashe anatembelea nyota ya Mkenda?
 
Per diem ya watu wote walioenda kwenye hii "circus" , petrol, na lost labour, pesa yote hii ingeweza kununua zaidi ya mara mbili ya hivyo vitenda kazi walivyogawa.

Ongezeko la 3.6bn kwa ajili ya research ni pesa ndogo sana kuleta impact kwenye kilimo.

Huyu waziri wa kilimo hana mikakati yoyote ya kukuza kilimo zaidi ya kutafuta kiki aka msanii
 
Kilichofanyika ni sawa na kuajiri mwalimu kwenye eneo lisilo n shule.

Unaboreshaje maisha ya afisa mmoja huku ukiwakandamiza wakulima ambao ni zaidi ya 60% ya watanzania wote? Huyo mgani anaenda kufanya nini
 
Asante kwa kunifumbua macho. Toka jana najiuliza hawa maafisa ugni ni watu gani hasa... Kumbe ni extension officers! Now I can happily contribute.
 
Mkulima atafaifika kwa kuhodhi soko? Kuwe na soko huru. Serkali afanye monitoring
 
Ila watanzania mna PhD ya kulalamika na kulaumu asee. Kwanini hamna Jambo jema kwenu?
1. Maafisa ugani wamewezeshwa usafiri na vipima uongo.
2. Mbegu ya alizeti na miche milioni 20 ya parachichi subsidized na hivyo kutolewa bure.
3. Kila Halmashauri kuwa na ofisi ya umwagiliaji inayopimwa performance yake kwa idadi ya ekari za umwagiliaji.
4. Kila afisa ugani lazima awe na shamba lake.
5. Kuanzia mwakani mbolea kupewa ruzuku na kutolewa kwa mkopo kama ilivyo kwenye korosho.
6. Ofisi ya Rais utumishi kupitia muundo Ili kuwezesha kuajiri mtaalam wa umwagiliaji kila halmashauri.
7. Benki zote zote mikopo ya single digit kwenye kilimo ambapo Benki ya CRDB na NMB tayari zimefikia hatua hiyo.
8. Serikali imetafuta masoko kwenye nchi zaidi ya 10 Ulaya na Asia na Afrika.
9. Hakuna mkulima amayepangiwa akauze wapi mazao yake kwa kipindi hiki;
10. Mabwawa kwa ajili ya umwagiliaji kuchimbwa kila Halmashauri yenye uhitaji na inayozalisha;
11. Kuanzisha mfuko wa maendeleo ya kilimo Ili kuwezesha utoaji wa ruzuku kwa mbolea pindi bei ikipanda;
12. Mashamba makubwa yaliyo chini ya msajili wa hazina sasa yazalishe kwa kuyakodisha kea sekta binafsi.
13. Eneo lote baada ya Bwawa la umeme lipimwe mashamba na yagaiwe kwa wawekezaji wakubwa Ili yazalishe kwani maji kwa ajili ya umwagiliaji tayari yatakuwepo.
14. Eneo la bonde la RUBADA lianze uzalishaji kwa njia ya ubia na sekta binafsi.

Pamoja na initiatives nyingi na nyingi. Sasa nyie mlitaka watu wafanye kitu hasa ili msilalsmike?
 
Ndugu maandishi mazuri. Kufikirika! Hadithi za Akajasembamba! Bibi kizee akamlamba matongotongo hahaha!
Miche ya korosho ilikuwa hivyo hivyo, na ulikuwa utawala wa Simba wa Yuda!
4. Nyerere alijaribu Sana, kuhakikisha Hilo likafeli, watu wamesoma wapate ajira siyo walime!
Kulikuwa na benki ya wakulima, benki mikopo ya wakulima wanakuambia hatukopesheki, BIMA premium Kali!

YOTE HAYO YANAENDESHWA KISIASA SIYO KIMFUMO, na ni marudio tu ya Sera za awamu zilizopita,

Watu wameshakula per Diem kazi iendelee, kilimo hakihitaji maonyesho Ka vifaa vya kijeshi!

KILIMO NI KIGUMU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…