Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acha nao hao huyo BASHE NAE MZINGUAJI HANA LOLOTE WOTE CCM WATOTO WA PANYA HANA JIPYANisiwaze vipi wakati msimu umeanza bei tz mbolea mfuko 160k lakini malawi mfuko wa mbolea 55k
Huu mtindo wa ugani haufai, niwa ghali sana na hauleti tija...Wagani walitakiwa kuwa sehemu ya uzalishaki kwenye kilimo hii tumepigwa Africa na kitu kizito ili tusitoke kwenyw hii small holder farmingMaafisa ugani ni watu muhimu katika kupeleka na kutafsiri matokeo ya tafiti mbalimbali kwa wakulima, wanasayansi tunapofanya tafiti mara nyingi zinabaki kwenye machapisho ambayo yanaishia kusomwa na watafiti wengine, badala ya mapendekezo kupelekwa kwa maafisa ugani wakawaelimishe wakulima. Wizara ya TAMISEMI inatakiwa kuwa na dawati la kupokea mapendekezo mbalimbali ya watafiti yaliyotokana na tafiti zao ili wazisambaze kwa wagani waliopo halmashauri na kuweza kuwaelimisha wakulima.
Aache porojo za kiwaki,mfuko wa mbolea 150,000 bado buster na dawa hazishikiki...hui uharo akaongee na ccm wenzakeDodoma.
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumpatia Sh150 bilioni ili aziweke katika benki za biashara kama dhamana (security), hatua itakayowezesha wakulima nchini kuanza kupata ruzuku ya mbolea katika msimu wa kilimo ujayo.
Bashe ameomba fedha hizo leo Jumatatu Aprili 4, 2022 wakati wa hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa vitendea kazi kwa maofisa ugani nchini.
Bashe amesema bei ya mbolea katika soko la dunia imepanda kwa zaidi asilimia 300.
Amesema Rais Samia aliielekeza Benki Kuu (BoT) kutenga Sh1 trilioni kwa ajili ya sekta ya kilimo na kumuomba Sh150 bilioni kwa ajili ya kuweka katika benki za biashara kama security.
Amesema hatua hiyo itawezesha kuaanza kutoa ruzuku ya mbolea katika msimu ujao wa kilimo.
“Nakuhakikishia mheshimiwa Rais fedha hii haitapotea. Tumeshafanya hivi katika korosho kwa kugawa ruzuku ya pembeje na tumeongeza uzalishaji tani 40,000,”amesema.
Aidha, Bashe amesema jumla ya maofisa ugani 7,000 watagawiwa pikipiki na vifaa vya kupimia udongo.
“Tumeanza kuwapa elimu maofisa ugani kulingana ekolojia ya maeneo na mazao yanayozalishwa na tutawapa ekari moja kwa kila ofisa ugani, atapewa mbegu bora na mbolea ili akiwafundisha awapeleke shambani,”amesema.
Amesema kuwa majaribio yameanza katika mikoa mitatu ya Dodoma, Singida na Simiyu kwa kutenga mashamba 600 ambapo kila kijiji kitakuwa na shamba darasa ili wakulima wapate elimu stahiki.
Pia amesema maofisa ugani hao watapatiwa vifaa vya kupimia udongo na kwamba hapo mwanzo taarifa za udongo zilikuwa zinapatikana kama za uganga wa kienyeji.
Bashe amesema lengo hadi kufikia mwaka 2025 kila kata iwe na kipimia udongo chake ambapo mkulima atapimiwa udongo na kupewa cheti ambacho kitakuwa na taarifa zote za afya ya udongo wake na aina ya virutubisho vinavyotakiwa.
View attachment 2175655
Mzalishaji mkuu mbolea ni RussiaHebu hayo mapinduzi yaanze kwenye bei ya mbolea
Mimi nimeanza kukubali baada ya kuona mabomba ya kutoa maji victory yashaanza kuwekwa singida , maana yake maji ya victory yatatinga dodoma ndani ya miaka miwiliMtakubali tuu kadiri ya mda unavyoenda.
Mara ngapi ?Inambidi Hamis Kigwa nae atafute Mganga wa kusafisha Nyota.
Kwa hiyo bashe anatembelea nyota ya Mkenda?"Kwa sasa idadi ya maafisa ugani tulionao nchini ni 6,704, idadi hii ni ndogo ukilinganisha na mahitaji yetu ya maafisa ugani 20,538 nchini, pamoja na idadi hii ndogo, pia kuna changamoto ya ukosefu wa vitendea kazi na mafunzo rejea kwa maafisa ugani nchini"
🎤 Waziri Mkenda
#BajetiYaKilimo2021
Taarifa za vita vya ukrain na Russia hazijawafikia.Ninaomba kufahamu, ni kwanini bei ya pembejeo Msumbiji na Malawi iko chini kuliko hapa kwetu?
Asante kwa kunifumbua macho. Toka jana najiuliza hawa maafisa ugni ni watu gani hasa... Kumbe ni extension officers! Now I can happily contribute.Leo maafisa ugani (extension officers) wanakabidhiwa Pikipiki, vipima udongo na simu janja (smart phone) ili viwawezeshe kutekeleza majukumu yao.
Hii fani ya maafisa ugani ilipoteza umuhimu kuanzia miaka ya 1980s. Hongera Samia kwa kumfanya Hussein Bashe kuwa Waziri kamili wa kilimo.
Kabla hata hiyo vita haijaanza mbolea bei imepaa sana kulinganisha na nchi za jirani.Mzalishaji mkuu mbolea ni Russia
Ndugu maandishi mazuri. Kufikirika! Hadithi za Akajasembamba! Bibi kizee akamlamba matongotongo hahaha!Ila watanzania mna PhD ya kulalamika na kulaumu asee. Kwanini hamna Jambo jema kwenu?
1. Maafisa ugani wamewezeshwa usafiri na vipima uongo.
2. Mbegu ya alizeti na miche milioni 20 ya parachichi subsidized na hivyo kutolewa bure.
3. Kila Halmashauri kuwa na ofisi ya umwagiliaji inayopimwa performance yake kwa idadi ya ekari za umwagiliaji.
4. Kila afisa ugani lazima awe na shamba lake.
5. Kuanzia mwakani mbolea kupewa ruzuku na kutolewa kwa mkopo kama ilivyo kwenye korosho.
6. Ofisi ya Rais utumishi kupitia muundo Ili kuwezesha kuajiri mtaalam wa umwagiliaji kila halmashauri.
7. Benki zote zote mikopo ya single digit kwenye kilimo ambapo Benki ya CRDB na NMB tayari zimefikia hatua hiyo.
8. Serikali imetafuta masoko kwenye nchi zaidi ya 10 Ulaya na Asia na Afrika.
9. Hakuna mkulima amayepangiwa akauze wapi mazao take kwa kipindi hiki;
10. Mabwawa kwa ajili ya umwagiliaji kuchimbwa kila Halmashauri yenye uhitaji na inayozalisha;
11. Kuanzisha mfuko wa maendeleo ya kilimo Ili kuwezesha utoaji wa ruzuku kwa mbolea pindi bei ikipanda;
12. Mashamba makubwa yaliyo chini ya mfuko wa hazina sasa yazalishe kwa kuyakodisha kea sekta binafsi.
13. Eneo lote baada ya Bwawa la umeme lipimwe mashamba na yagaiwe kwa wawekezaji wakubwa Ili yazalishe kwani maji kwa ajili ya umwagiliaji tayari yatakuwepo.
14. Eneo la bonde la RUBADA lianze uzalishaji kwa njia ya ubia na sekta binafsi.
Pamoja na initiatives nyingi na nyingi. Sasa nyie mlitaka watu wafanye kitu hasa ili msilalsmike?