Rais Samia: Bei ya mafuta Tanzania ni rahisi kuliko Marekani

Rais Samia: Bei ya mafuta Tanzania ni rahisi kuliko Marekani

Rais Samia katika kuwajibu wale wanaolalamika kua bei ya mafuta ni kubwa sana amesema hiyo bei ni ndogo sana hasa ukilinganisha na bei ya mafuta Marekani.

Rais anasema juzi alikua Marekani akakuta bei ya mafuta iko juu sana kuliko Tanzania.

Hayo Rais ameyasema leo hii kwenye kipindi cha mahojiano na Tido Mhando.

Juzi pia Rais akiwa Arusha alisema kua watu wanapenda kulalamika umeme ukikatika kidogo tu wakati hata New York umeme unakatika tu hata kuliko Tanzania.

Nimeisikiliza hii Intvw daah kweli kazi ipo ,hii awamu yaani naiona ndefu, eeh Mungu tusaidie hapa mpaka mwishoni mwa mwaka ngoma itakuwa 4000+ per litre,tukiingia mwakani sitoshangaa kufika 5000+ per litre.

Kweli mwingi unapigwa na sukari inalambwa.
 
Rais Samia katika kuwajibu wale wanaolalamika kua bei ya mafuta ni kubwa sana amesema hiyo bei ni ndogo sana hasa ukilinganisha na bei ya mafuta Marekani.

Rais anasema juzi alikua Marekani akakuta bei ya mafuta iko juu sana kuliko Tanzania.

Hayo Rais ameyasema leo hii kwenye kipindi cha mahojiano na Tido Mhando.

Juzi pia Rais akiwa Arusha alisema kua watu wanapenda kulalamika umeme ukikatika kidogo tu wakati hata New York umeme unakatika tu hata kuliko Tanzania.

Huyu bibi, aende TU akaishi huko Marekani maana imemjaa akilini mwake! Hovyo kabisa!
Tunaongelea gharama za maisha kupanda tangu awe rais, anaongelea Marekani 🤔!
 
Huyu Rais huyu nahisi kuna kitu hakiko sawa....
So what?...yaani hii ndio justification..aisee
Ok yeye anasaidiaje katika hili?....
Kuwa kiongozi sio lelemama....
Hatari sana

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
Tuwe wapole, hata marekani umeme huwa unakatika!
===

Huyu mama huyu !!!! ??????

Nimeishi UK, kule kila kitu gharama nguo, viatu kodi ya pango n.k. , Ila kipato changu nilichokuwa napata kule kwa wiki kwa kazi hio huku hata kwa mwaka huenda nisingepata..., (yaani hapo naongelea unskilled labor bado sijaongelea professional jobs)

Hivi haya anayasema kama siasa, kukosa uelewa au anatudharau (insulting our intelligence)

Hii ni kukosa uelewa aisee. Ni hatari kua na raisi mwenye uwezo huu wa kufikiri.
 
Wastani wa kipato cha Mtanzania mmoja kwa mwezi 500K na litre ya mafuta ni Tzs 3,184 wakati wastani wa kipato cha Mmarekani wa hali ya chini ni 11M kwa mwezi wakati gallon ya mafuta ambayo ni sawa na litre 3.4 ni USD 5.

Sasa hapo nani mwenye nafuu?
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. 😁
 
Sasa purchasing power ya mwananchi wa Tanzania ni sawa na Marekani,yani kipato cha mtu unskilled labour kipo juu sana kuliko hata hapa bongo kwa upande wa skilled ..kwel kunasehemu tumekosea kama nchi.Magufuri lala salama baba..
REASONING ABILITY yake ndo inaniacha na maswali, juzi tu hapa alisema hata MAREKANI umeme unakatika kwahiyo Wadanganyika tusimsumbe Waziri Makamba...
 
Rais Samia katika kuwajibu wale wanaolalamika kua bei ya mafuta ni kubwa sana amesema hiyo bei ni ndogo sana hasa ukilinganisha na bei ya mafuta Marekani.

Rais anasema juzi alikua Marekani akakuta bei ya mafuta iko juu sana kuliko Tanzania.

Hayo Rais ameyasema leo hii kwenye kipindi cha mahojiano na Tido Mhando.

Juzi pia Rais akiwa Arusha alisema kua watu wanapenda kulalamika umeme ukikatika kidogo tu wakati hata New York umeme unakatika tu hata kuliko Tanzania.

Kwahiyo pia Mishahara ya Wafanyakazi wa Tanzania ni mikubwa kuliko Mishahara ya Wafanyakazi wa Marekani!
Marais Wetu wanavyopenda Kurongopa kwa kujilinganisha na nchi zingine! Akili ya Watanzania tunajijua Wenyewe!
 
Iko juu kivipi?
Screenshot_20220504-130957.jpg
 
Back
Top Bottom