Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema chakula ni siasa na kwamba kukiwa hakuna chakula au sukari ikipanda bei Vijana wa Gen Z hawatotulia bali wataingia barabarani (kuandamana) na kwa kulitambua hilo Serikali inaendelea kulinda maslahi ya makundi yote ikiwemo maslahi ya Wananchi bila kuathiri maslahi ya uwekezaji na viwanda.
Rais Samia amesema hayo leo August 03,2024 baada ya kuzindua Bwawa la Umwagiliaji la Kiwanda cha Sukari Mtibwa Mkoani Morogoro.
“Serikali inatambua umuhimu wa viwanda vya sukari Nchini tunalenga kufika masoko makubwa ikiwemo DRC ambako ni soko kubwa mno, kwahiyo sukari yote itakayozalishwa Tanzania italiwa ndani lakini tutauza Burundi DRC na Nchi nyingine zitakazotaka sukari yetu”
“Jukumu la Serikali ni kulinda na kutetea maslahi ya makundi yote katika Jamii, hivyo inapotokea Serikali inasimamia upande wa kundi lisilo na nguvu ni katika kutimiza jukumu hilo na kutetea maslahi ya makundi yote katika Jamii, hivyo Serikali inaposimama upande wa Wananchi wanaotaka sukari ya uhakika kwa bei himilivu inafanya hivyo kwa msingi huo na sio vingine vyovyote, sio kwamba tuna shida na viwanda au vyovyote vile, tunalinda uwekezaji, tunalinda viwanda lakini lazima tulinde na Wananchi wetu”
“Wanasema chakula ni siasa kukiwa hakuna chakula hapa ile Gen Z haitokaa kitako itaingia barabarani, au ukiwapandishia sukari ikifika kilo elfu 7, elfu 8, elfu 9 hawatotulia wengine wote hawa hawatotulia kwahiyo lazima tulinde maslahi ya kotekote”