Mwaka 2023 Vijana wa kitanzania kwa umoja wao walishindwa kuunga mkono maandamano ya kupinga mali zetu za taifa kupigwa mbana, ila pengine mwaka huu 2024 tutakuwa tumejifunza ya GEN-Z ya Kenya.
Pengine tahadhari ya mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huko Morogoro kuwa maandamano yanaweza kutokea ya viiana ni kweli kwa kuwa ana utitiri wa vyombo vya Dola vinavyompa
taarifa ya hali ya kisiasa na kijamii mtaani na vijijini Tanzania
TOKA Maktaba:
19 June 2023
Dar es Salaam, Tanzania
MAANDAMANO YA MWAKA 2023, ILIKUWA GEN-Z ILIYOSHINDWA KUUNGWA MKONO
View: https://m.youtube.com/watch?v=ewNw5e22LWY
Jeshi la Polisi limewatawanya na kuwakamata baadhi ya waandamanaji wanaopinga mkataba wa uwekezaji katika bandari Tanzania.Maandamano hayo yaliitishwa na Deusdedith Soka Juni 15, 2023 kwa ajili ya kupinga mkataba huo wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.Hata hivyo Juni 17, 2023 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilipiga marufuku maandamano hayo na kueleza kuwa, mtu aliyeandaa maaandamano hayo ameshajibiwa kwa barua.