Rais Samia: CCM inawachama milioni 13 yoyote anayefikiria kukipasua chama hiki ajifikirie mara mbili mbili

Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amewashukuru Watanzania Kwa kuendelea kuiamini na kuiunga mkono CCM.
Kinara wa "kukipasua chama" ni yeye mwenyewe.
Inashangaza kuona kuwa bado anamtafuta mchawi mwingine.
 
Chama kina wanachama wote hao halafu kinaogopa UCHAGUZI HURU, WA HAKI NA WAKUAMINIKA?
Huyu Samia ni DR . Wa nn sasa! Hawezi kufanya analysis?
Huyo huyo Samia anayejigamba chama chake kuwa na wanachama wote hao, bado haamini kuwa wanachama wenzake kwenye mkutano watampitisha kuwa mgombea wa nafasi ya Rais!

Inabidi afanye mbinu za kuwaepuka wenzake wasimpe taabu.

Je, huko kwenye uchaguzi mkuu nako hataweza kuwategemea hawa mamilioni kumchagua yeye kwa kura halali, hadi ibidi kufanyike hujuma kwenye uchaguzi huo?

Hii ina maana gani na kujigamba kuwa na wana chama milioni kumi na tatu!
 
Unacho eleza hapa bila ya aibu ni mpango wa wizi wa kura wakati wa uchaguzi.
Hao waTanzania wengine ambao hawataki hizo kura zenu hawana haki ya kuchagua viongozi wa kuwaongoza?

Sasa ielewe vizuri maana ya "NO REFORM, NO ELECTION".

hao mnaotafuta kuwanyang'anya HAKI yao hawatakubali ushenzi huu.
 
 
..akawaombe msamaha GenZ wa Kenya.

..Watanzania tumechoka mitandao kufungiwa wakati ugomvi hatukuuanzisha sisi.
Maana yake, sisi sote ni "MATEKA" wao. waweza kufanya chochote bila ya kuhojiwa na yeyote.
 
Kqtiba yq nchi imetoa uhuru anayetaka kupiga kura ruksa na asiyetaka ruksa asiende kupiga kura

Katiba inachojataza ni mtu mwingine kuzuia nwingine anayetaka kwenda kupiga kura asiende Huo ni uhaini

Huwezi zuia mtu mwingine asitumie haki yake ya kikatiba kwenda kupiga kura yake kama anataka .
 
Hiyo katiba CCM wanaikumbuka tu inapowafaa wao, na wanaitupilia mbali inapokataa ujinga wao?

Basi subiri safari hii hiyo katiba iwe kweli "vipande vya karatasi "tu, kama alivyosema Samia.

Nyinyi watu wa CCM mmejitoa akili vichwani mwenu kiasi cha kuonekana kuwa majuha kabisa!
 
Kama mpo wengi hivyo, mnaogopaje tume huru ya uchaguzi?
Kwa nini mnahangaika kuengua wapinzani wenu kwenye chaguzi au kuwateka na kuwaua?
Hofu yenu nini?
 
Kadi za CCM zilikuwa zinatolewa kwa wenye kadi za kupiga kura tu muongo wewe

Hao milioni 13 ni wenye kadi za kupiga kura.Haiwezekani ukawa na kadi ya CCM halafu huna kadi ya kupiga kura
Sasa hofu ya uchaguzi huru na haki mnaitoa wapi?
Hizo takwimu fake
 
Chama kinachojiamini kwa sera nzuri na kimefanya mengi katika kuleta maendeleo kwenye nchi hii ila ishu ya tume huru ya uchaguzi hawataki hata kuisikia.

Wasomi,wanachama,makada,vijana wa Lumumba naombeni majibu yenye maana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…