Rais Samia chagua upande wa Haki au Dhuluma, huwezi kwenda na vyote

Rais Samia chagua upande wa Haki au Dhuluma, huwezi kwenda na vyote

JERUSALEM 2006

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
527
Reaction score
596
Haujambo mwana JF mwenzangu wa jukwaa letu pendwa la siasa. Ni matumaini yangu unaendelea kupigana vizuri na changamoto za maisha hasa kwenye uchumi huu ulio dorora kutokana na changamoto za UVIKO. Pambana mwana jamvi, usikate tamaa, maisha ni kuishi kwa matumaini kila iitwayo leo mpaka pale pumzi zetu zitakapo katika.

Nianze kwa kumpongeza Mhe. Rais SSH kwa kufikisha siku 100 akiwa kama rais wa kwanza mwanamke kuongoza taifa letu. Pongezi zangu pia zielekezwe kwenye utendaji wa serikali yake kwa siku hizi za awali, amejipambanunua kama mtu wa haki na anayechukia dhuluma kwa matendo. Wote ni mashahidi, kesi mbalimbali zilizokosa ushahidi zimefutwa, wafungwa kadhaa wameachiwa huru, wafanya biashara wako huru, wanasiasa kwa sehemu wanapumua na zaidi uchumu bado umetengamaa japo sio kwa ubora sana.

Tar. 28/06/2021 wakati anasheherekea siku 100, Mhe. Rais SSH alitumia mwanya huu kuongea na wahariri na waandishi wa vyombo vya habari. Mhe. Rais alipokea maswali na maoni kutoka upande wa waandishi, baadae akapata wasaa wa kujibu maswali hayo na kutoa neno kwenye baadhi ya maoni. Kwa kweli alijitahidi sana kuwa muungwana na kuongea ukweli katika mambo mengi. Naomba nijikite kumshauri Mhe. Rais Katika hoja mbili tu, nazo ni katiba mpya na mikutano ya kisiasa ya hadhara.

Kuhusu katiba mpya
, Mhe. Rais hili ni hitaji la kisheria. Mwaka 2012, ilitungwa sheria na Bunge la JMT kuruhusu mchakato wa katiba mpya kuanza mpaka ukamilifu wake. Bahati mbaya mchakato huo uliishia njiani bila mwafaka wala consensus ya kisiasa. Hakuna sheria mpya iliyotungwa kubatilisha sheria hii ya mwaka 2012, hivyo sheria hii bado iko valid mpaka sasa.

Mhe. Rais, Hoja zako za kuweka pending mchakato wa katiba mpya ni kuhusu utengamavu wa uchumi na utulivu wa kisiasa ili kuvutia uwekezaji.

Mosi, mchakato wa katiba mpya kama utafanywa kwa matakwa ya sheria bila kubakwa na wanasiasa, utakuwa bora sana na kufanya hali ya siasa nchini kutengamaa hivyo kuvutia wawekezaji (kulingana na hoja zako).

Pili, katiba mpya ni hitaji la watanzania, sio hitaji la wawekezaji. CCM imekuwa madarakani kwa miaka 60 mpaka leo bado mnahitaji muda kuboresha uchumi? Nadhani ni wakati muafaka sasa kama taifa tukatunga katiba ya wananchi, katiba itakayo ungwa mkono na walio wengi. Hivyo basi kama wawekezaji hawawezi kuwekeza kwa sababu ya mchakato wa katiba mpya, and so be it.

Kenya matharani, wanatuzidi kwa uwekezaji na wawekezaji nchini kwao, mwaka 2011 walifanikiwa kupata katiba mpya, hatukuona mahala popote uchumi wao ukiteteleka wala uwekezaji kushuka kwa sababu ya mchakato ule.

Mhe. Rais, kuepusha lawama na masimango kwa viongozi wanaojifanya miungu watu pindi waingiapo madarakani, na ili kuleta utengamano wa kisiasa katiba mpya haikwepeki.

Kuhusu Mikutano ya Kisiasa,
Mhe. Rais, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 18, 20 na 21 zinatoa uhuru wa watu kukutana na kutoa maoni yao bila kuingiliwa na mtu yeyote ila kwa kufuata sheria za JMT. Pia, sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, inavipa haki vyama vya siasa vilivyosajiliwa au vilivyo kwenye mchakato wa kusajiliwa kufanya mikutano ya hadhara mahali popote ndani ya JMT.

Mhe. Rais, hakuna sheria yoyote hapa nchini, inayoruhusu wabunge wenye majimbo tu kufanya mikutano ya hadhara, na kukataza wanasiasa wengine kufanya hivyo. Hakuna kitu kama hicho.Hayo yalikuwa maoni yako binafsi, na tunayachukua kama maoni ya rais, ila sio kama sheria za JMT.

Mhe. Rais, mikutanoo ya hadhara sio hisani kutoka kwako, na wala sio ombi. Ni jukumu lako na serikali yako kusimamia kwa ukamilifu taratibu, Katiba na sheria zote za JMT bila kujali zina kupa favor wewe au wapinzani wako.

Mhe. Rais, uliupata Urais kwa kurithi kulingana na matakwa ya Katiba na sheria za nchi yetu. Embu fikiria wasingefuata katiba na sheria kwenye eneo hilo, labda sasa hivi usingekuwa rais.

Naomba nikukumbushe, kama unachagua kuwa Rais mwema, basi kuwa mwema kwa kila kitu. Usichagua baadhi ya mambo tu ili kufurahisha kundi fulani la watu. Kama unataka kuacha legacy ya kweli katika taifa hili, anza kwa kutenda haki kwa kufuata katiba na sheria zetu.

Lakini kama utaamua kuminya katiba (dictatorship) basi fanya kweli kweli. Usiume na kupuliza, usiwe moto halafu ukawa baridi kwa wakati mmoja. hakuna vuguvugu, hakuna katikati.

Mwisho ila sio kwa umuhimu
, Mhe. Rais, washauri wako wa karibu wanaweza kukujenga au kukubomoa. Kwa sasa una mamlaka makubwa sana, kila utakalofanya utasifiwa na washauri wako. Watu wa kukwambia ukweli kuhusu taifa hili, ni wapinzani wako wa kisiasa na wananchi wasio na mamlaka ya kisiasa. Ukisahau hili na wewe utaanza kuililia hiyo katiba mpya na uhuru wa kisiasa pindi hayo mamlaka yatakapo kutoka, mimi na wewe sio Mungu, hakuna aijuaye kesho zaidi ya Mungu, tenda mema kana kwamba hakuna kesho, tenda haki ili ujipalilie maisha yako ya baadae, usifurahishe kundi dogo la walaji, furahisha umma kwa ujumla.
 
Tutambue anapozuia Katiba Mpya ni kwamba anawalinda wale wa chama chake hapo anakuwa mwema kwao, na mbaya kwa wapenda mabadiliko, kumtaka awe mwema kwa wote itakuwa ngumu sana kwake, lazima kuna kundi halitaridhika vinginevyo ajitoe mhanga hasa.
 
Kizazi cha sasa hatuwezi ongozwa na katika mfu. Mawazo ya miaka ya 77 ni mawazo yaliyokufa kwa kizazi cha sasa.
Katiba hii chakavu ndio imefanya vyeo vya uDC kukosa hadhi siku hizi yeyeto upewa tu. Eti mtu kama Nassari, lijuakali, Sabaya eti nao ni ma DC.
 
Kizazi cha sasa hatuwezi ongozwa na katika mfu. mawazo ya miaka ya 77 ni mawazo yaliyokufa kwa kizazi cha sasa.
Katiba hii chakavu ndio imefanya vyeo vya uDC kukosa hadhi siku hizi yeyeto upewa tu.Eti mtu kama nassari,lijuakali,sabaya eti nao ni ma DC.

Exactly, kwanza nina wasiwasi na waliopitiasha hiyo katiba ya 1977, Je walishirikisha wananchi?
 
Muda si mrefu na yeye atakuwa kama mtangulizi wake tu. Kwa mbaali madaraka yameshaanza kumlevya.

Ukiwa Kiongozi, halafu ukashindwa kutambua mahitaji ya wale unao waongoza kwa wakati huo, maana yake umeshakuwa failure tayari
yaani mnahaha na katiba utafikiri inamuhimu sana kama itawaletea hela wacheni uchumi ukue hayo mengine baadae sana
 
Back
Top Bottom