Rais Samia chagua upande wa Haki au Dhuluma, huwezi kwenda na vyote

Rais Samia chagua upande wa Haki au Dhuluma, huwezi kwenda na vyote

Si ndio waliochagua CCM ikashinda law kishundu au??

Pamoja na wananchi wengine lakini wana CCM ndio walioiachagua ilani ya CCM na kupenda sera zao na ndio maana ikashinda na sasa mama ndio anafanyia kazi ilani hiyo
Ccm ilishinda wapi wakati walifukuza wote uwanjani wakabaki peke yao na bila hata watazamaji. Chama kiko madarakani kwa zaidi ya nusu karne lakini kinaogopa uchaguzi balaa. Very hopeless indeed.
 
Mhe. Rais, uliupata Urais kwa kurithi kulingana na matakwa ya Katiba na sheria za nchi yetu. Embu fikiria wasingefuata katiba na sheria kwenye eneo hilo, labda sasa hivi usingekuwa rais.
Kweli kabisa mkuu. Kwa mfano jeshi lingeamua kutofuata katiba ingekuwaje?
Kufuata katiba lisiwe takwa la mtu, kwamba leo sawa kesho hapana, au hili sawa lile hapana
 
Kuhusu Katiba na Tume huru ya uchaguzi Mama kaa chini utafakari upya.

Watanzania wana njaa...sasa wewe umelishikilia bakuli la pilau hutaki kulitenga chini...

Sidhani kutakuwa na utulivu unaouhitaji wewe kama utaendelea kulikumbatia bakuli hilo.
 
Yaani ni ajabu mtu anaapa kuitunza,kuilinda na kuheshimu katiba ambayo hata yeye ndo ilimpa madaraka baada ya JPM ila anakuwa wa kwanza kuivunja hiki sio kitu kizuri kwa taifa
 
Mama ajue kuwa katiba mpya ni haki ya wananchi na Tumehuru ya uchaguzi is a must kama anapenda kweli haki!! La sivyo anatudanganya kwa kutamka haki!!
 
Viongozi wetu wawe mfano kwa watoto na wajukuu zetu kwa kyonyesha imtegrity! Kuwa mtu wa haki, mzalendo kwa nchi yake, mfuata sheria, mwiko kuiba kura, msema kweli, na mpemda watu wote kwa usawa!! La sivyo tunajenga nchi isiyo na maadili!!
 
Back
Top Bottom