Rais Samia: Chalamila wewe ni mfanyakazi mzuri ila naomba ukakue

Rais Samia: Chalamila wewe ni mfanyakazi mzuri ila naomba ukakue

Nchi ina watu kibao lakini yeye kamteua mtu asiyemuamini!! amemteua wa nini?? Chalamila ameumbwa vile sasa sijui kama ataweza kuwa siriaz??
Angekuwa hamuamini asingemteua..Mnaweza kuwa watu kibao ila Wenye uwezo ni wachache..

Ndio maana hakunaga viongozi wengi huwa ni wachache na Chalamila ni miongoni mwa hao wachache..

Uteuzi sio Fadhila,Hata maofisini Huko tunaona watu ni lundo ila Wenye uwezo ni wachache wengi ni mizigi tuu.
 
Hakuna tatizo kwa Mama kumwambia mwanae ukweli.

Hii inathibitisha kuwa Mama anampenda mwanae ndio maana kamwambia ukweli maana hataki kuona mwanae anaharibikiwa tena.
naamini Mama anamwamini sana kuwa mwanae ni hodari kwa kuchapa kazi.
Kwanza ana msaidia, Chalamila anapenda kuweka masihala pasipohitaji masihala..

Mimi binafsi alipotenguliwa nilosikitika kwa sababu ni kweli kusimamia jambo anaweza ila mzaha sasa.
 
Msando si alikuwa anajifanya ana hela jumbe uzushi tu,mshahara wa RC hauzidi milioni kumi ,Kafulila alikaribia kupasuka kwa unene,watakuwa wanapiga dili na wakurugenzi wa halmashauri
Kuwa kiongozi ni heshima,pesa tuu haitoshi ndio maana hata mabwanhenye huko Ulaya wanapambana wawe viongozi..
 
Mbna wataz kibao tu wako wakupewa hizo nafasi chalimila kitu gani saasa akapotezwa mazima apewa hata mtu anaituwa mtukamanzina
 
Kwani ikiteuliwa ni lazima
ukubali, ya nini kusimangwa kama mtoto kisa ukuu wa
mkoa, mbona sie wengine
tunaishi hata ukuu wa kaya
hatuujui unafananaje
Na huyo aliyemteuwa kwani alilazimishwa kumteuwa mtu ambaye anajua ni mtundu kama hakuna watu wengine.
 
Wateuliwa wote wapelekwe seminar ya how to behave like a senior Government official

Mbona mabalozi hupewa seminar kabla kuruhusiwa kwenda ofisi ya ubalozi
Hakuna lolote ujinga mtupu!

Yaani mtu ujibane bane hata kujamba ushindwe ati kisa ni mkuu wa mkoa wa Simiyu?

Simiyu yenyewe haijulikani hata kwenye ramani ya dunia. Mwisho wa siku unakufa na ushuzi tumboni na ukuu wako wa mkoa!!

Watu wawe huru. Ni kweli nidhamu iwepo lakini watu wasiwe watumwa wa vyeo uchwara.

Wengine wanapenda maskhara. Ndio raha hiyo. Unataka kununa nuna tu muda wote kama ZIMWI??

Ati mkuu wa mkoa!!! Kheeee!!!
 
Raisi yuko Sahihi Chalamila na Makongoro Nyerere wanatakiwa kujua vyeo vikubwa kama vya kuteuliwa viwe ukuu wa mkoa etc na Raisi they need to behave themselves as senior responsible government officials not as comedians Or playboys.Nafasi hizo ni kubwa
Acha wivu wa kike
 
Nchi ina watu kibao lakini yeye kamteua mtu asiyemuamini!! amemteua wa nini?? Chalamila ameumbwa vile sasa sijui kama ataweza kuwa siriaz??
Lukuvi+ Prof+ Ndugu+ Chala+ ......... = Mshtuko!?
 
Mbona wakubwa walioishakua wapo tayari? Mpaka tumsubiri mtu mmoja akue saa ngapi?
Hata wanawake ukiwauliza wanataka nini wengi hawajui. Acha twende tu hivyo hivyo. Kuba mmoja katumbuliwa kabla ya kuapishwa, sasa na yeye akakue au Kuna sababu nyingine?
 
Anyway wakuu wa mikoa wawili wanaotakiwa kujitathimini kuwa wanaenda au la ni wawili kwa sasa Chalamila na Makongoro Nyerere

Cheo hicho wanapwaya they don't behave like senior government officers .They just behave like comedians
 
Back
Top Bottom