Rais Samia: Dereva aliyeamua kuliingiza lorry kwenye korongo kwa kukwepa utelezi

Rais Samia: Dereva aliyeamua kuliingiza lorry kwenye korongo kwa kukwepa utelezi

Hamieni Bujumbura
Huko mtaenda msiokuwa na nchi. Sisi Watanganyika, tukitoka nchini mwetu tunaenda nje kutembea tu, lakini hapa ni kwetu. Hakuna wa kututoa.

Warundi waliopo Tanganyika wanaweza kurudi kwao Burundi, Wazanzibari wanaweza kurudi kwao Zanzibar, Wamalawi wanaweza kurudi kwao Malawi LAKINI Mtanganyika ambaye yupo Tanganyika, hakuna wa kumtoa maana yupo nyumbani kwake.
 
Hakuna kazi hata moja iliyowahi kukosa changamoto. Iwe ni Urais, Uwalimu, Udaktari, Ukulima, Biashara na Uwekezaji, Udereva, Uhandisi, Uchungaji au Ushekhe, Uwanafunzi, au nyingine yoyote, isiyo na changamoto, japo uwingi na uzito wa changamoto hutofautiana.

Na wanaofanikiwa, siyo watu wanaokosa changamoto, bali ni watu wenye kutafuta majibu sahihi ya changamoto zinazowakumba.

Kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoanguka, ni uwezo wa kutafuta majibu ya changamoto, zinapojitokeza. Kwenye utatuzi wa changamoto, kuna makundi matatu:

1) Wapo ambao wakipata tu changamoto, hawatafuti majibu ya changamoto, hunyosha mikono na huishia hapo hapo. Hawa huwa wafu wa mafanikio.

2) Wapo wanaotafuta suluhu za mkato, wakakosa hekima, maarifa, ujuzi na tafakari, huishia kutafuta suluhu za changamoto ambazo huleta madhara mabaya zaidi hata kuzidi changamoto walizotaka kuzitatua.

3) Wapo wanaotafuta suluhisho la changamoto zinazowakumba, hutafuta suluhisho sahihi, huzivuka changamoto, na huibuka wakiwa washindi. Hawa ndio watu wenye mafanikio siku zote.

Bahati Mbaya, Rais wetu Samia Suluhu Hassan, anaangukia kwenye kundi ka pili. Yaani mtu anayetafuta suluhisho la matatizo kwa kuzalisha matatizo makubwa zaidi maradufu ya tatizo analotaka kulitatua. Amekuwa kama dereva wa lorry lililobeba shehena kubwa ya mzigo wenye thamani kubwa, linalopanda mlima wenye utelezi ambao upande mmoja wa barabara ni mlima mrefu, na upande wa pili ni gema refu kuelekea korongoni (sawa na yale makorongo ya milima ya Lukumburu, kama unaelekea Songea). Mlima una utelezi, dereva anawaomba watu walisukumie lorry kwenye korongo refu ili kuukwepa utelezi. Na kwa kufanya hivyo anaamini ametatua tatulizo la kuupanda mlima wenye utelezi, asijue kuwa kwa kusukumia lorry korongoni, ameliua lorry, ameteketeza shehena yenye thamani, na lorry halitaweza kuendelea na safari.

Kuna tatizo kubwa kwenye mkataba wa bandari wa DP, ambalo ni uhovyo na ushenzi wa mkataba. Rais Samia haumizwi na ubovu wa mkataba, anaumizwa na sauti za wanaolalamikia uhovyo wa mkataba. Hahangaiki na kutatua uhovyo wa mkataba, bali anahangaika kuzima sauti za wanaolalamikia mkataba wa hovyo. Kwake kuwakamata Dr. Slaa, Mwambukusi na Mdude na kuwabambikia kesi za uhaini anaona ametatua tatizo la kusikia kelele zinazokosoa uhovyo wa mkataba. Hajui wala hatambui kuwa kwa kufanya hivyo anatengeneza matatizo makubwa zaidi dhidi yake na Serikali yaje kuliko hata uhovyo wa mkataba. Sasa afahamu kuwa:

1. Kelele dhidi ya mkataba wa kishenzi wa DP, zitaongezeka kutoka ndani ya nchi.

2) Kelele dhidi ya udikteta wa utawala wake zimeanza kutoka ndani ya nchi na jamii ya kimataifa. Tayari Amnesty International wamelaani maamuzi yake, Human Rights Watch wamepaza sauti dhidi ya utawala wake. Siku si nyingi kutakuwa na kauli toka Jumuiya ya Ulaya na Marekani.

3) Taasisi zote ambazo hutoa misaada na mikopo kwa sharti nchi iwe na mfumo wa utawala unaoheshima demokrasia, uhuru wa maoni na haki za binadamu, hazitatoa msaada wala mkopo kwa Serikali ya Samia. Ni suala la wakati tu.

4) Hata ambao hawakuwahi kujua uhovyo wa mkataba wa DP, watafahamu sasa kutokana na hizo kesi za kubambikia watu, na matamko ya taasisi za jamii ya kimataifa.

5. Uchumi ambao tayari ni legelege utalegea zaidi kwa sababu hakuna mwekezaji makini anayeweza kwenda kuwekeza mahali ambapo unaweza kubambikiwa kesi na Serikali wakati wowote.

Rais Samia badala ya kutafuta msaada wa kusukuma gari liupite utelezi, ametafuta watu wa kumsaidia kulisukumiza lorry korongoni.
Huyu mama kuna jambo analificha ile mikataba aliyosaini utadhani anauza nguo zake kalikosea sana taifa huyu mzanzibar.
 
Andiko lako na mifano yako haina uhalisia wala hauendani na kile ulichotaka kukiwasilisha hapa jukwaani,umeongea uongo na upotoshaji mtupu.

Habari za kusema uchumi wetu ni dhaifu hapa naona aidha huna takwimu sahihi au umeamua kujipa upofu wa akili na macho,kwa kuwa ukuaji wa uchumi wetu ni mzuri sana na unaendelea kufanya vizuri sana mpaka Taasisi kama IMF na WB zilitupongeza waziwazi kama nchi, tumeshuhudia miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikifanyika nchini, wawekezaji waliongezeka kila siku, mzunguko wa fedha Mitaani ukiwa ni wenye afya, shughuli za kiuchumi na kibiashara zikiongezeka kila iitwayo leo ,jambo lililopelekea kuongezeka kwa fursa za ajira kwa vijana pamoja na kuongezeka kwa mapato ya kikodi kufikia Trilioni mbili kwa mwezi.

Kwa Taarifa yako hakuna Taifa lolote linaloweza kuvumilia wala kuwavumilia wahuni na watu aina ya akina Mdude,hakuna Taifa hilo la kijinga hapa Duniani ambalo linaweza kuwafumbia macho watu wanaofanya matendo ya kihaini kwa kupanga , kuchochea, kuhamasisha na kushawishi watu waipindue serikali halali iliyopo madarakani.Hao wababaishaji wataendelea kusota ndani ili wajibu vizuri juu ya matamko yao ya kijinga.

Habari za matamko au nyaraka kutoka Taasisi au nchi au jumuiya yoyote ile hayawezi iteteresha wala itetemesha serikali yetu wakati inajuwa hatari ya maneno ambayo yanatolewa na wahuni wachache wanaotaka kuleta machafuko nchini,.yeyote atakaye kwenda kinyume na sheria zetu atawajibishwa kwa mujibu wa sheria .Hakuna aliye juu ya sheria na hakuna atakaye achwa pasipo kuchukuliwa hatua.Nchi yetu ni huru na ina sheria zake na haihitaji kuomba ruhusa kutoka popote pale au kufundishwa namna ya kuongaza Taifa letu.suala la usalama na maslahi ya Taifa letu lipo mikononi mwetu kama Taifa na hivyo yeyote yule kutoka nje ya nchi yetu hawezi kuibabaisha serikali yetu.

Kama mnatoa lugha za kichochezi ili mje mtetewe na hao mnao waabudu basi mjue ya kuwa serikali yetu ni imara, madhubuti na shupavu,ambapo haitamuonea mtu haya katika kumuwajibisha na kumchukulia hatua kali za kisheria .wahuni kama akina Mdude lazima wafundishwe adabu na namna ya kutii sheria zetu.
 
Naunga mkono hoja! Kama ameshauriwa hili hakika walimshauri hawamtakii mema wala hawamtakii safari njema ya siasa za hapa nchini.
Sio ajabu safari yake ikaishia hapa, very sad!
 
Kwa kifupi mtoa mada anasema Rais ana elements za ukilaza, Mimi ni nani nipinge?
 
Naunga mkono hoja! Kama ameshauriwa hili hakika walimshauri hawamtakii mema wala hawamtakii safari njema ya siasa za hapa nchini.
Sio ajabu safari yake ikaishia hapa, very sad!
Watanzania wana imani kubwa sana na mh Rais wetu mpendwa mama samia,wana matarajio makubwa sana kutoka kwake na wanaamini Rasilimali zetu ni salama mikononi mwake.ndio maana ukipita mitaani unaona namna kulivyo Tamalaki kwa amani na utulivu.ndio maana unaona watanzania wamefurahishwa sana na uamuzi na hatua ya jeshi la polisi kuwazoa wachochezi na wahamasisha vurugu na machafuko hapa nchini
 
Rais wa hovyo kuwahi kutokea sio Afrika tu huenda dunia nzima.
Sikiliza wewe uliyekosa adabu na akili.kwa Taarifa yako ni kuwa Rais samia ndiye Rais bora kabisa tuliye naye kwa sasa katika Bara hili la Afrika kwa sasa ni kiongozi wa mfano na kuigwa ,ni kiongozi anayeishi mbele ya wakati na mwenye maono ya mbali. Ni kwa ushujaa wake na upeo wake mkubwa wa kimaono na kiuongozi ndiyo maana ametuvusha kama Taifa katika nyakati zote ngumu ambazo Dunia imezipitia na kutetemeshwa ,lakini Rais samia alisimama imara na kutuvusha
 
Hakuna kazi hata moja iliyowahi kukosa changamoto. Iwe ni Urais, Uwalimu, Udaktari, Ukulima, Biashara na Uwekezaji, Udereva, Uhandisi, Uchungaji au Ushekhe, Uwanafunzi, au nyingine yoyote, isiyo na changamoto, japo uwingi na uzito wa changamoto hutofautiana.

Na wanaofanikiwa, siyo watu wanaokosa changamoto, bali ni watu wenye kutafuta majibu sahihi ya changamoto zinazowakumba.

Kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoanguka, ni uwezo wa kutafuta majibu ya changamoto, zinapojitokeza. Kwenye utatuzi wa changamoto, kuna makundi matatu:

1) Wapo ambao wakipata tu changamoto, hawatafuti majibu ya changamoto, hunyosha mikono na huishia hapo hapo. Hawa huwa wafu wa mafanikio.

2) Wapo wanaotafuta suluhu za mkato, wakakosa hekima, maarifa, ujuzi na tafakari, huishia kutafuta suluhu za changamoto ambazo huleta madhara mabaya zaidi hata kuzidi changamoto walizotaka kuzitatua.

3) Wapo wanaotafuta suluhisho la changamoto zinazowakumba, hutafuta suluhisho sahihi, huzivuka changamoto, na huibuka wakiwa washindi. Hawa ndio watu wenye mafanikio siku zote.

Bahati Mbaya, Rais wetu Samia Suluhu Hassan, anaangukia kwenye kundi ka pili. Yaani mtu anayetafuta suluhisho la matatizo kwa kuzalisha matatizo makubwa zaidi maradufu ya tatizo analotaka kulitatua. Amekuwa kama dereva wa lorry lililobeba shehena kubwa ya mzigo wenye thamani kubwa, linalopanda mlima wenye utelezi ambao upande mmoja wa barabara ni mlima mrefu, na upande wa pili ni gema refu kuelekea korongoni (sawa na yale makorongo ya milima ya Lukumburu, kama unaelekea Songea). Mlima una utelezi, dereva anawaomba watu walisukumie lorry kwenye korongo refu ili kuukwepa utelezi. Na kwa kufanya hivyo anaamini ametatua tatulizo la kuupanda mlima wenye utelezi, asijue kuwa kwa kusukumia lorry korongoni, ameliua lorry, ameteketeza shehena yenye thamani, na lorry halitaweza kuendelea na safari.

Kuna tatizo kubwa kwenye mkataba wa bandari wa DP, ambalo ni uhovyo na ushenzi wa mkataba. Rais Samia haumizwi na ubovu wa mkataba, anaumizwa na sauti za wanaolalamikia uhovyo wa mkataba. Hahangaiki na kutatua uhovyo wa mkataba, bali anahangaika kuzima sauti za wanaolalamikia mkataba wa hovyo. Kwake kuwakamata Dr. Slaa, Mwambukusi na Mdude na kuwabambikia kesi za uhaini anaona ametatua tatizo la kusikia kelele zinazokosoa uhovyo wa mkataba. Hajui wala hatambui kuwa kwa kufanya hivyo anatengeneza matatizo makubwa zaidi dhidi yake na Serikali yaje kuliko hata uhovyo wa mkataba. Sasa afahamu kuwa:

1. Kelele dhidi ya mkataba wa kishenzi wa DP, zitaongezeka kutoka ndani ya nchi.

2) Kelele dhidi ya udikteta wa utawala wake zimeanza kutoka ndani ya nchi na jamii ya kimataifa. Tayari Amnesty International wamelaani maamuzi yake, Human Rights Watch wamepaza sauti dhidi ya utawala wake. Siku si nyingi kutakuwa na kauli toka Jumuiya ya Ulaya na Marekani.

3) Taasisi zote ambazo hutoa misaada na mikopo kwa sharti nchi iwe na mfumo wa utawala unaoheshima demokrasia, uhuru wa maoni na haki za binadamu, hazitatoa msaada wala mkopo kwa Serikali ya Samia. Ni suala la wakati tu.

4) Hata ambao hawakuwahi kujua uhovyo wa mkataba wa DP, watafahamu sasa kutokana na hizo kesi za kubambikia watu, na matamko ya taasisi za jamii ya kimataifa.

5. Uchumi ambao tayari ni legelege utalegea zaidi kwa sababu hakuna mwekezaji makini anayeweza kwenda kuwekeza mahali ambapo unaweza kubambikiwa kesi na Serikali wakati wowote.

Rais Samia badala ya kutafuta msaada wa kusukuma gari liupite utelezi, ametafuta watu wa kumsaidia kulisukumiza lorry korongoni.
Umenikumbusha kipindi nasomea udereva mwalimu wetu alitufundisha namna ya kulisaidia gari likianguka.
Yaani wakati unaendesha labda ukaona kabisa gari pale mbele litaanguka wee endesha alafu ukifika pale ulipohisi likunjie hapo lianguke vizuri ili lisiumie.
 
Naunga mkono hoja yako, Binafsi najiuliza hivyo huyu ndiye yule yule Samia aliyeanzisha mahusiano mema na kutatua changamoto kadhaa ktk kuleta demokrasia? Bila shaka kuna kundi linalomshauri vibaya wakiwa na dhamira yao makhususi.
Kundi linalomshauri vibaya linajulikana, ni lile linalochochea mauaji ya kimbari kwa kuchochea ghasia, kuhamasisha lila aina ya vurugu kwa kuwa tu wametolewa kwmy ulaji
 
Kuna watu inaonekana wamedhamiria sana kuhakikisha Samia anakuwa Rais wa nusu mhula tu. Na hao wamekazana sana kuhakikisha kila siku idadi ya wanaomchukia Rais inaongezeka.
Rais samia ndio chaguo la mamilioni ya watanzania,ndio kiu ya watanzania,ndio hitaji la wengi katika kutuongoza na kutufikisha mpaka 2030.kinachosubiliwa kwa sasa ni kumuapisha tu kwa ajili ya muhula wa pili maana kwa sasa hana mpinzani wala mwenye ubavu wa kushindana naye katika sanduku la kura.
 
sio kweli!
ndo angepewa u-Dr?
Kwani Dr. Kasheku a.k.a King Musukuma mjumbe amaalum ambae aliongoza wajumbe kwenye mkataba wa bandari huko Dubai mbona nae ni lasaba failure?
 
Wewe punguani, endelea kujidanganya. Kichaa anaweza kunyanyua fimbo akamtisha mtu mwenye akili timamu, na mwenye akili timamu akakimbia, lakini haimaanishi kuwa kichaa kashinda.
Nimecheka sana.
 
Back
Top Bottom