Rais Samia elewa wapiga kura wa nchi hii wanahitaji nini kwa sasa

Rais Samia elewa wapiga kura wa nchi hii wanahitaji nini kwa sasa

Nimesoma kitabu cha "Will Propaganda Work in Modern World?" Mwandishi pamoja na mambo yote anasema, "moja ya sifa chanya na bora kwa kiongozi makini ni kujua watu wake wanahitaji nini kwa wakati gani na kwa sababu gani naye huenda na matakwa yao ili kukidhi na kukata kiu yao. Anasema kiongozi asiye na maono ya mbali hukinzana na matakwa ya umma na hata kusuguana nao kwa hila jambo ambalo hufanya mwisho wa kiongozi huyo kuwa mbaya au nzuri lakini uzuri wa mashaka.

Ukisoma nyuso za Watanzania, ukisikia kauli zao rasmi na zisizo rasmi kwa ujumla wao utagundua kuwa ni kikundi kidogo mno tena wa kuhesabu hata na mtoto wa darasa la pili ndio wanafurahia na kushangilia ufisadi maana wananufaika na ufisadi huo.

Kundi kubwa na hasa wenye maisha dhalili nyoyo zao zimevimba kwa hasira wanapoona hawasikilizwi wanataka nini kwa SASA sio kesho. Ukweli ni kwamba Ripoti ya CAG imeamsha hasira za wananchi walio wengi na hasa baada ya Spika kudai ripoti hiyo itajadiliwa Novemba.

Wananchi wanahoji kwa nini kama ni sheria inataka hivyo ni matukio mangapi mabadiliko ya sheria yalifanywa kwa hati ya Dharura? Wananchi hawana shida na mambo mengine yooooote. Sijui SGR, ndege Mpya, Busisi Bridge, maji asilimia 78 mijini, sijui akaunti za wasambaza ushoga kufungiwa nk. Hilo hawalijadili huku "site". Wao wanataka mjadala huru wa Ripoti hii na hatua kuchukuliwa kwa wezi wote na waziridishe pesa zao. Basi! Hayo mengine mnajifurahisha tu.

Na mimi naungana nao, wananchi wenzangu tuwaache wao wajadili ya kwao sisi tu-deal na wezi wetu na ikiwezekana tuwahukumu wenyewe.

Narudia, Samia achana na wapambe, sikiliza sauti za waajiri wako wanahitaji nini kwa sasa si November? Uchaguzi ni wako, uamuzi ni wetu. Ahsante.
Kwa hiyo wewe haya mawazo ya unaowaita "wananchi" umeyatoa wapi?
 
Hilo neno "wapiga kura" ni la hovyo sana bahati mbaya wananchi wenzangu tunaliendekeza, ni vyema litumike kipindi muafaka si kila wakati kulitumia kana kwamba ni sifa, ni kutiana unnyonge tu' japo andiko lako lina Dasperado
 
Wapiga kura wa sasa wanahitaji Tume HURU na Katiba bora mpya.
 
Hayo yote uliyoandika kama hakuna tume huru ama katiba mpya ni takataka tu. Kwani asipofuata matakwa ya wananchi watamfanyeje? Anajua kura ataiba tu, ndio maana mkiambiwa tume huru na katiba mpya ni kwa faida ya raia wote muwe mnaelewa.

Ndio maana 2020 wapinzani tulipiga kelele sababu ime set precedence mbaya sana. 2025 anajua akiamua anaweza komba majimbo na kata zote na yeye kubeba Urais kwa 90% ya kura na anajua hakuna kitu wananchi mtafanya.

Tuwe serious sote tudai katiba mpya whether ni Sukuma Gang, Chadema au CCM mwenye nia ya kumuondoa Mama Samia 2025.
Pamoja na katiba mpya, tume mpya ya uchaguzi, mabadiliko ya sheria, ...
Ni muhimu kushughulika na wahalifu (wezi wa kura na wanaopindisha sheria). Katiba na sheria zilizopo hairuhusu wizi wa kura.
Kuwaza kumuondoa Mama Samia hakuondoi tatizo, yeye mwenyewe anaweza kutumia mfumo huo huo wa wizi kujirudisha madarakani.
Hasira zisielekezwa kwa mama tu, ziende kwa wote walio katika mfumo uliosababisha hali hii, lakini lengo likiwa ni kurekebishwa ili tuaminiane na tuishi kwa Umoja, Amani na Upendo kitaifa.
 
Katiba Mpya na Tume Huru itarudisha fedha zilizoibwa au tutasamehe na tuanze moja?
Sasa kama mtu anajua hamuwezi kumtoa madarakani kupitia Sanduku la kura unadhani atachukulia hatua mafisadi kwa faida ya nani? Hata JPM kuwa mkali mkali vile ni sababu alijua moto wa 2015 ungejirudia 2020 so hakutaka kudhalilika Tena!!

Demokrasia inaleta uwajibikaji.... Sasa nyie mnataka eti Rais asikilize wananchi wanataka Nini? Kwani akikataa mtafanyaje? Jibu HAKUNA then Uzi wako unakosa relevance maana sijaona ulipo propose tume huru au katiba mpya Ili mumuadhibu 2025.
 
Katiba na sheria zilizopo hairuhusu wizi wa kura.
Zinaruhusu ndio maana inakataza kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani. Yaani hata kama umeibiwa na una ushahidi huna pa kuupeleka!! Kma sio mwanya wa kuruhusu wizi ni Nini?
Ni muhimu kushughulika na wahalifu
Kivipi Sasa wakati bunge lililopewa kazi ya kuchambua ripoti ya CAG na kuleta mapendekezo ya kuwanyoosha mafisadi kikatiba linaweza vunjwa na Rais!! Yaani hata bajeti zikiwa za kifisadi lazma mzipitishe tu otherwise bunge linavunjwa na uchaguzi mpya unaitishwa!!
Kuwaza kumuondoa Mama Samia hakuondoi tatizo,
Nani anataka kumuondoa? Nilichosema kama wanataka mama Samia afanye kazi ni lazima kuwepo na tume huru plus katiba mpya, Ile hofu ya kwamba wananchi ndio wanaamua nani awe Rais inatosha kumfanya achape kazi. Ila kwa Sasa hiyo motivation haipo maana Rais anaamuliwa na kamati kuu ya CCM full stop na sio wananchi so hawawezi kuwa na leverage ya kumpangia Rais chochote.
 
Back
Top Bottom