Rais Samia elewa wapiga kura wa nchi hii wanahitaji nini kwa sasa

Kwa hiyo wewe haya mawazo ya unaowaita "wananchi" umeyatoa wapi?
 
Hilo neno "wapiga kura" ni la hovyo sana bahati mbaya wananchi wenzangu tunaliendekeza, ni vyema litumike kipindi muafaka si kila wakati kulitumia kana kwamba ni sifa, ni kutiana unnyonge tu' japo andiko lako lina Dasperado
 
Which will be directed by Party Cocus
That's why the astute people demand for constitutional reform so as to plug all the loopholes that allow one party members to dominate the parliament.
 
Wapiga kura wa sasa wanahitaji Tume HURU na Katiba bora mpya.
 
Pamoja na katiba mpya, tume mpya ya uchaguzi, mabadiliko ya sheria, ...
Ni muhimu kushughulika na wahalifu (wezi wa kura na wanaopindisha sheria). Katiba na sheria zilizopo hairuhusu wizi wa kura.
Kuwaza kumuondoa Mama Samia hakuondoi tatizo, yeye mwenyewe anaweza kutumia mfumo huo huo wa wizi kujirudisha madarakani.
Hasira zisielekezwa kwa mama tu, ziende kwa wote walio katika mfumo uliosababisha hali hii, lakini lengo likiwa ni kurekebishwa ili tuaminiane na tuishi kwa Umoja, Amani na Upendo kitaifa.
 
Katiba Mpya na Tume Huru itarudisha fedha zilizoibwa au tutasamehe na tuanze moja?
Sasa kama mtu anajua hamuwezi kumtoa madarakani kupitia Sanduku la kura unadhani atachukulia hatua mafisadi kwa faida ya nani? Hata JPM kuwa mkali mkali vile ni sababu alijua moto wa 2015 ungejirudia 2020 so hakutaka kudhalilika Tena!!

Demokrasia inaleta uwajibikaji.... Sasa nyie mnataka eti Rais asikilize wananchi wanataka Nini? Kwani akikataa mtafanyaje? Jibu HAKUNA then Uzi wako unakosa relevance maana sijaona ulipo propose tume huru au katiba mpya Ili mumuadhibu 2025.
 
Katiba na sheria zilizopo hairuhusu wizi wa kura.
Zinaruhusu ndio maana inakataza kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani. Yaani hata kama umeibiwa na una ushahidi huna pa kuupeleka!! Kma sio mwanya wa kuruhusu wizi ni Nini?
Ni muhimu kushughulika na wahalifu
Kivipi Sasa wakati bunge lililopewa kazi ya kuchambua ripoti ya CAG na kuleta mapendekezo ya kuwanyoosha mafisadi kikatiba linaweza vunjwa na Rais!! Yaani hata bajeti zikiwa za kifisadi lazma mzipitishe tu otherwise bunge linavunjwa na uchaguzi mpya unaitishwa!!
Kuwaza kumuondoa Mama Samia hakuondoi tatizo,
Nani anataka kumuondoa? Nilichosema kama wanataka mama Samia afanye kazi ni lazima kuwepo na tume huru plus katiba mpya, Ile hofu ya kwamba wananchi ndio wanaamua nani awe Rais inatosha kumfanya achape kazi. Ila kwa Sasa hiyo motivation haipo maana Rais anaamuliwa na kamati kuu ya CCM full stop na sio wananchi so hawawezi kuwa na leverage ya kumpangia Rais chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…