Rais Samia, fikiria hatua sahihi kwa maslahi ya Taifa na familia yako

Samia kaisha jiweka katika point of no return ni ngumu kufanya hayo maana amesha jifunga... njia pekee aliyo ichagua ni kufanya umafia kubaki madarakani akiamini kuwa akisha baki madarakani ataweza kutumia fedha na nguvu za dola kupangua maadui zake na kubaki salama
 
Asante kwa bandiko lako, yeye kama yeye, anapajua pa kuchomokea... ningependa sana awaachie wengine nao waendeleze atakapo ishia hasa ukizingatia kwamba yeye alikuwa ni Raisi wa mpito na aliyepatikana kwa mujibu wa katiba... Ya nini kungangania? Nina hakika, hata akishindwa, watakao mfuata hawatafungua makaburi yake kwa kuogopa ya kwao nao kufunguliwa siku wakiachia... hivyo hana cha kupoteza wala kuogopa kama akiachia ngazi sasa.
 
CCM waweke mtu strong katika nafasi ya kugombea urais si kuchaguliana wao ndani kwa ndani wafanye Kama CDM hii kuweka transparency miaka 5 iliyobaki mama akiendelea na urais akitoka deni la TAIFA litakuwa si chini ya 220 tilion maana Nchi anaiendesha kwa mikopo kwa kila kitu kuanzia ujenzi wa mawizara,shule,miradi mikubwa eg.SGR,Barbara etc tutajuta
 
Njia pekee ya nchi kukombolewa ni wananchi kuamka na kutumia nguvu. Namshauri Samia aendelee kuuza kila kitu mpaka machawa watakapoanza kutekwa na kupotea. CCM pigeni hela mpaka watu waanze kuandamana na kupambana na polisi. Samia ukiachia nchi sasa hivi watakaoingia wataendeleza uliyoyafanya. Ili tupige hatua endeleeni kupiga hela. Wananchi wanadiscuss Simba na Yanga wakati Lissu yupo ndani. Bado wana uwezo wa kuvumilia shida kwa kigezo cha uzalendo.
 
Shida hii hapa sasa;"...ukizingatia kwamba yeye alikuwa ni Rais wa mpito....". Hilo mnamkumbusha sasa apate akili maana huenda kile kikao cha siri atakuja ulizwa Majaliwa alikuwa PM wa awamu ya ngapi? Akijibu ya sita, naamini ataulizwa ulimuapisha? Jibu hapana. Swali kwahiyo aliendelea na kiapo cha awamu ipi? Jibu ya tano, ataambiwa ya sita ilikuwepo? Amua mwenyewe unaenda ukawe ya sita mpya au ipi?
Mkumbusheni tu huenda atarudiwa na ile hali njema.
 
Anachonikera Samia ni kitu kimoja tu, kulipa nguvu na ushawishi mkubwa kundi la JK, huko kuna watu hatari sana kibiashara ambao wanazo hulka za Ngamia kwamba akiruhusiwa kuingiza shingo hemani lazima mwili mzima uingie.

Katika miaka minne ya SSH wafanya biashara wamekuwa na nguvu sana na tayari wameshajiona wana uhalali kwa sababu ya michango yao ya nyuma ya pazia ndani ya CCM.

Pole Pole akiwa mtoto wa hayati JPM kifikra kwanza kabisa mtihani wake mgumu ni hao watu dhalimu wanaotembea nyuma ya pazia wakiongozwa na JK.

Kwa bahati mbaya ni kwamba mkwere haamini katika falsafa za kijamaa lakini kakuzwa kisiasa na anazungukwa na wajamaa wengi.
 

Tamaa ya pesa na uchu wa madaraka haviwezi mwachia,na kama akiamua kuachia ngazi basi atakua ameangalia zaidi usalama wa maisha yake kama kiongozi asiekubalika na raia pia raia wa chama chake,
 
Mungu anailinda nchi hii, baada ya kufariki JPM malaika Mabeyo akamuongoza Samia kwa kumshika mkono na kuiweka nchi mahali salama.

JK na kundi lake limefaidika na uwepo wa Mabeyo kama malaika mlinzi mkuu imekuwa ni faida njema kwa Taifa.

Hatufahamu hao wengine iwapo wangeichukua ikulu kwa kumuweka pembeni SSH leo hii tungekuwa katika hali gani.

Tatizo la uongozi ni kwamba hakuna anayeweza kuwaridhisha watanzania wote milioni 65, hata huyo hayati JPM aliumiza wafanya biashara wengi sana kwa kiburi tu cha kipuuzi.

Hakuna afadhali ya wote inakuwepo kwa wachache tu ndio maana hakuna rais mwema tangu awamu ya Julius Nyerere.
 
well said mkuu, sina cha kuongeza
 
Tamaa ya pesa na uchu wa madaraka haviwezi mwachia,na kama akiamua kuachia ngazi basi atakua ameangalia zaidi usalama wa maisha yake kama kiongozi asiekubalika na raia pia raia wa chama chake,
sasa suluhisho la haya yote yanayoendela ni nini ?
 
Ujumbe bora kabisa wa kuanzia wiki.
Mwenye masikio na asikie neno hili.
Kongole kwako mleta uzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…