Rais Samia, fikiria hatua sahihi kwa maslahi ya Taifa na familia yako

Tunasemaga Locuta causa finita !
Hata Polepole analijua hilo !
Wabishi wakae kwa kutulia tu!
Hakuna mahali Katiba imevunjwa !
Kwa maana Katiba hiyo hiyo ndio iliyompa Mkuu Madaraka yote hayo makubwa na hao wabishi wanaolalama kwa sasa hawakuwahi kulalamika kuhusu hiyo Katiba !

WHY NOW ! ? Big question mark ⁉️
 
Mwaka 1985 Mwinyi alipita kwenye mchakato kwa kumshinda Salim..hivyo hivyo Mkapa,Kikwete,Magufuli wate walishindanishwa ndani ya Chama huyu Samia ni Rais kujiteua bila kupita kwenye mchakato..
Unajua kusoma kweli? Nauliza tena, hao wote kwenye awamu yao ya pili walishindanishwa na nani?
 
Bila shaka utakua kamanda mwenzetu wa CHADEMA.. maana bila kutukana kamwe utaweza kuendelea kuitwa kamanda.
Huyo Mama yako hapendwi ila analazimisha kupendwa, mngempambania na matusi waliyomporoshea Wakenya !
 
Ni mawazo yangu maana nimepima upepo kitambo sana humu tangu mwaka 2008, sijui wewe ulijiunga lini ndugu yangu? umepima upepo? tunakoelea Panya road watatamalaki...
Mkuu nimekuelewa sana. Kumbe haya ni mawazo yako na wala wewe si Mjumbe aliyetumwa kutuletea ujumbe husika. Kama ulivyosema awali, Mjumbe hauwawi. Hivyo kwa uhai wako katika Jukwaa hili utakuwa umejiandaa vizuri sana kwa vipigo kutoka pande zote. Kila la kheri.
 
....Wakati wafuatao wanatafuta kugombea nafasi au awamu yao ya pili walishindanishwa na akina nani?
Aiseeee!
Unajua kusoma kweli? Nauliza tena ,awamu zao za pili walishindanishwa na nani?
Sasa na mimi na kuuliza unajua kuandika na kusoma kweli? Ama hilo neno 'au' ulikosea kuandika 'ua' . Ukiujua huu wengine wanaujua ule. JF hapa, nyata taratibu.
 
Inashangaza sana, Samia anavunja katiba ya CCM kwa kujiteua mwenyewe na Nchimbi wake huku wanaCCM wanaangalia kama kwamba hakuna wanaume wenye uwezo wa kuongoza nchi .... 😲
shithole countries. wezi na mafisadi wanataka waendelee na yao
 
Wavilete tu... kelele zimezidi sana humu nchini, kila sehemu moto, moto, moto, mara Polepole na sukuma gang, mara Mpango kajiuzuru, mara Kasim Majaliwa.. kuna tatizo mahali fulani. ktk timu ya mpira, mara nyingi ni kocha anatakiwa kujiudhuru na si vinginevyo , hata kama amefanya usajili wa akina Messi, Ronadinho , na wengineo. Wasipo funga , lawama zote ni kwake na lazima ateme bungo.. Ndio maana ya bandiko langu.
 
Naunga mkono hoja.
Mzalendo wa kweli hawezi kuona mambo yanaharibika kwa kuangalia maslahi ya tumbo lake na familia yake tu.
Hivyo kama na yeye pia ana punje ya uzalendo, kwa hapa tulipofikia, busara kwake ni kuachia ngazi.

Sisi Watanzania wa kawaida hatutaki tena kuongozwa na wale ambao wanatuongoza bila ridhaa yetu maana wengi wao huwa wanaongoza kwa nyodo sana na hawajali maslahi ya watu wa hali ya chini.

Nakumbuka zile kauli zake kwa wajane za kusema " hebu mwondosheni huyo maana anashughulisha watu hapa!"

Sidhani kama itakuwa busara kuendelea kuongozwa na yule ambaye anatanguliza maslahi ya wenye nacho na kuwaacha wengi wapambane na hali zao.

Busara na hekima ni kuachia ngazi kama alivyofanya Joe Biden.
 
Huu ujumbe umfikie SAMIA SULUHU HASSAN kupitia watu wake wa karibu. Chawa hakikisheni ujumbe huu anausoma mama yenu, asipoelewa basi atakua na "kishimbe".
 
Mheshimiwa sana,

Rais Samia, fikiria hatua sahihi kwa maslahi ya Taifa na familia yako- Achia ngazi kama Biden alivyo fanya- hupungukiwi na kitu... waachie pia wafungwa wa kisiasa wakiwemo pia wale ulio watembelea Nairobi- Mungu wa Mbinguni atakubariki sana.​

 
Polepole atalindaje mkataba wa kinyonyaji wa DP WORLD, na waarabu walionunua hifadhi ya ngoro ngoro na kuwafukuza wamasai?
Fanya utafiti kidogo kuhusu Ngorongoro..ni dude kubwa kuliko unavyodhani ..
 
Bandiko hili Bado lina dumu kwa Muheshimiwa sana mama Rais wetu - Samia Suluhu Hassan...
 
Mheshimiwa sana,

Rais Samia, fikiria hatua sahihi kwa maslahi ya Taifa na familia yako- Achia ngazi kama Biden alivyo fanya- hupungukiwi na kitu... waachie pia wafungwa wa kisiasa wakiwemo pia wale ulio watembelea Nairobi- Mungu wa Mbinguni atakubariki sana.​

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…