Rais Samia: Haikuwa na maana kuchoma vifaranga wa kuku mpakani

Rais Samia: Haikuwa na maana kuchoma vifaranga wa kuku mpakani

Daktari gani atapima kitu ambacho kimeingia kimagendo nchini? Manake walikuja kupimwa baada ya kukamatwa ili nchi ijiridhirishe kulikuwa attempt gani kutoka kwa jirani zetu. Utaratibu wa custom unajulikana, vipimo vinachuliwa custom, sasa wale walipimwaje halafu wakose permits?
Mbona Kenya hawakuiteketeza dhahabu ya Tanzania iliyokuwa imeingia kwa magendo? Wakairudisha Tanzania.

Mbona hawakutaifisha ng'ombe 9,000 waliokuwa wameingia Kenya, wakati sisi tulitaifisha ng'ombe 4,000 walioingia Tanzania?

Sisi tulikosa tu uongozi wa hekima.
 
Sisi tulimkemea Luhaga Mpina waziwazi kwa ile misifa yake aliyofanya kuchoma vifaranga mbele ya makamera. Yani wasukuma mlichotufanyia mmejichumia laana kubwa sana!
Ndio maama mvua zimegoma😅😅
 
Walikuwa marehemu?
Magu kabla hajafa alikuwa yupo tayari kusemwa na kukosolewa?

Umesahau yaliyowapata waliojifanya majasiri kumkosoa.

Tundu lissu mpaka leo ana ulemavu.

Ben sa nane yuko wapi?

Kwa vile alikataa kusemwa akiwa hai watu tutamsema akiwa amekufa.
 
"wenzake tayari wanatumikia sentence zao, yeye kakimbilia Nairobi nadhani ni calculation tu". Hapa siyo dhambi, dhambi ni kuchoma kuku wenye magonjwa waliokuwa wanaingia nchi bila kujali sheria transboundary movement of live animal. Kama nchi tupo tayari kuingiza magonjwa nchini kudhuru afya ya walaji almradi kufurahisha majirani? Tufuate sheria zilizopo.

Yote ni dhambi tu. Ndio hasara ya kuingiza jazba katika majukumu ya kiserikali.

Rais kusema visivyo kuhusu Mbowe katika chombo kikuu cha media kama BBC huku akiwa macho makavu ni adha ya kitaifa isiyoelezeka kirahisi. Hapa ndipo waswahili tunasema: aibu naona mimi.

Vifaranga vingezuiwa pale pale mpakani visiingie nchini. Kama ni magonjwa yangebakia huko huko Kenya. Kuvichukua kisha kununua petroli na kuvichoma moto vikiwa hai mbele ya kamera za tv ni kielelezo cha matatizo ya kisaikolojia. Ask the honest opinion of any reputable psychiatrist.

Inabidi tujiongeze kama taifa. We really need to be beyond these despicable acts. No defense can exonerate our leaders from suspicion of insanity - beyond malice, that is.
 
Katika kongamano la biashara lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam ambalo limehusisha viongozi wawili wakubwa ambao ni Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Rais wa Tanzania Samia Hassan Suluhu.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu amesema kwamba hakukuwa na haja ya kuchoma vifaranga waliokamatwa nchini Tanzania kutoka nchi jirani.

Amesema pia kuna kipindi ilitokea pia Sukari kutoka nchi ya Uganda iligomewa na wafanya biashara kutoka Tanzania, hivyo amemueleza Rais Museven kwamba hivi sasa Sukari kutoka Uganda itanunuliwa na wafanyabiashara wa Tanzania!

Amehimiza pia kwamba vikwazo vya kibiashara kati ya nchi hizi mbili viondolewe!

Hayo yamesemwa wakati Kongamano hilo likifungwa.
Wanafiki hawawezi kwisha duniani. Amalizie ungwe yake atoke.
 

Na ile kauli dhidi ya waziri wa Kilimo Bwana Mkenda imekaaje?
Mkenda aachie tu ngazi, mama amuweke mtu wake(Nape Mosses Nauye) pale.
 
Kama elimu yako ni ya ubabaishaji na walimu wako wa kitanzania ni vilaza ni bora walimu wa Kenya waje watufaulishie watoto wetu.

Wewe kaa unainba kiswahili hadi unapandisha jaji cheo kwa hukumu ya kiswahili.


Magufur ndiyo kiboko ya wakenya maana wakenya walitutesa Sana miaka 30 walikuwa wanaingia Tanzania bila viba wanafanya kaz za ualimu bila kibali cha kaz wa uhamiaji sasa wataanza kutamba tena
 
Utalindaje wazalishaji wa ndani, bei za bidhaa nchi jirani ziko chini na mipaka ya nchi ipo wazi kila pembe kupitisha magendo, Tunaenda kuua viwanda vya ndani
Acha vife. Kama kulinda viwanda vya ndani ni kununua na kuuziana bidhaa kwa bei ghali kuliko nchi nyingine, acha hivyo viwanda vife kabisaaaaa!!!! Mfano sukari ikiingizwa kutoka nje itauzwa kg 2000 halafu sukari ya ndani inauzwa kg @ 3000[emoji3064] Acha vife maana sukari ya nje plus usafiri lakini bado bei iko chini lakini hii ya ngani ambayo usafiri ni wa ndani humu humu lakini bado iko juu [emoji119][emoji119][emoji119]
 
Hiyo nchi itakubali kuwapokea tena wakati lab test kwa upande wetu imeshadhihirisha kuwa vifaranga vile vina infestation of quarantine importance? Kenya wenyewe wapo tayari kupeleka mlipuko wa magonjwa kwao? Kupiga kiberiti ilikuwa ni suluhusho ili kuzuia magonjwa ya mifugo kuingia nchini. Ndo utaratibu wa quarantine duniani.
Ukumbuke vifaranga vile siyo vya nchi ni vya individual mfugaji, shipping ilifanyika kinyemela kati Wafanyabiashara wa pande mbili bila kufuata utaratibu. Imekuja kubainika kwamba vifaranga vina shida, Kenya itawapokea?! Never on earth. Watakwambia infestation ilitokea at the point of entry kwa bakini na mzigo wenu huko.
Hayo majibu ya kuwa hao vifaranga wana ugonjwa yalitolewa na tapeli yule yule aliyepima covid kwenye mapapai na diseli. Halafu akasema tumepiga maombi kisha Corona ikaondoka!
 
Rais amesema, "tulikuwa tunachomeana" then wehu kadhaa wanakuja na mapovu useless kabisa kumtuhumu Rais Samia kuwa anamsaliti Magufuli!. Baadhi ya mitanzania mivivu kusoma na hivyo miakili yao imevilia tu. Hakuna mahali Rais amejitoa kwenye kadhia ya vifaranga!. Kama mtu amemsikiliza vizuri Rais, ameonesha kujihusisha katika hilo na hivyo kujilaumu kwa makosa ambayo waliyafanya kama serikali awamu iliyopita.
 
View attachment 2026534
Na ile kauli dhidi ya waziri wa Kilimo Bwana Mkenda imekaaje?
Mkenda aachie tu ngazi, mama amuweke mtu wake(Nape Mosses Nauye) pale.
View attachment 2026531

Tanzania kununua sukari Uganda ni ujinga kupitiliza .

Wakati mwingine nchi yetu kama nchi inakosa thinktank kila kitu tunamwachia Rais atuamulie hata kama kina madhara kwa taifa.

Tanzania haiwezi kuwa nchi ya kununua tu hata pale tunapoweza kama nchi.Uganda inaingia mara nne au zaidi iweje Rais ashabikie tununue sukari badala ya kuweka mikakati ya kuzalisha sukari ya kutosha hapa nchini.
 
Hayo majibu ya kuwa hao vifaranga wana ugonjwa yalitolewa na tapeli yule yule aliyepima covid kwenye mapapai na diseli. Halafu akasema tumepiga maombi kisha Corona ikaondoka!
Hahahahaha .......corona haikuondoka Ila waliipa masharti kupitia Polepole kwamba " aidha iondoke au ituogope ikubali kuishi nasi". Mara moja Makonda akapewa jukumu la kusherekea corona kukubali kwishuishi Na na sisi. Ogopa watu wenye uwezo wa kutoa amri kwa virus. Hii nchi kiboko sana.
 
Katika kongamano la biashara lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam ambalo limehusisha viongozi wawili wakubwa ambao ni Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Rais wa Tanzania Samia Hassan Suluhu.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu amesema kwamba hakukuwa na haja ya kuchoma vifaranga waliokamatwa nchini Tanzania kutoka nchi jirani.

Amesema pia kuna kipindi ilitokea pia Sukari kutoka nchi ya Uganda iligomewa na wafanya biashara kutoka Tanzania, hivyo amemueleza Rais Museven kwamba hivi sasa Sukari kutoka Uganda itanunuliwa na wafanyabiashara wa Tanzania!

Amehimiza pia kwamba vikwazo vya kibiashara kati ya nchi hizi mbili viondolewe!

Hayo yamesemwa wakati Kongamano hilo likifungwa.
Mara nyingi mtu husema kwakuwa mdomo ni mali yake ila siku hazigandi kama nikwahisia au nikwa maono ya mtu binafsi time will tell us. Marehem hasemwi. End
 
Back
Top Bottom