Rais Samia: Haikuwa na maana kuchoma vifaranga wa kuku mpakani

Rais Samia: Haikuwa na maana kuchoma vifaranga wa kuku mpakani

Naona genge flani linatoa povu Kwa Bibi Hangaya eti ni mnafiki yeye alikua part ipi kipindi ule upuuzi wa kuchoma vifaranga unafanyika huko wakisahau utawala wa Mwendawazimu jiwe,mtu mwenye faili lake Milembe alikua anakuja na maamuzi inategemeana ameamkaje!
Mnajisahaulisha ya kwamba yule bwana alikua na kichaa Cha mbwa Koko hataki kushaurika plus ujuaji wa kishamba na ukizingatia bi Hangaya ni mwanamke na yule bwana ni mhutu na mwanaume wa kihutu hua hawasikilizi ushauri wa wanawake wakiamini ya kwamba Hana alijualo!
Hahahahahaha!
 
Utalindaje wazalishaji wa ndani, bei za bidhaa nchi jirani ziko chini na mipaka ya nchi ipo wazi kila pembe kupitisha magendo, Tunaenda kuua viwanda vya ndani
Unataka wananchi tuumie kisa tunalinda viwanda vya ndani?
 
Wasipokee kwa sababu gani? Si vimetoka kwao? Mliwarudishia wakavikataa? Au shobo zenu tu kuwahi kuvipigq kiberiti kwa chuki mlizojijengea awamu ile.
Zitapokewa vipi kama hakuwa na nyaraka zinazoonesha kwamba wametoka Huko
 
Rais wa JMT mh Samia Suluhu Hassan amesifu ushirikiano wa nchi za Afrika mashariki na kusema tulikuwa tunachomeana kuku mipakani, dhambi tupu viumbe wa Mungu tunamwaga petrol kuwachoma haikuwa na maana.

Rais Samia amesema hayo katika kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda.

Source: Swahili times
Mbona hakuthubutu kuongea kipingi dikteta yupo hai?
 
Mbona machinga nao mmewabomolea na kuharibu mali zao nini tofauti na kuchoma vifaranga?
Mlishindwa nini wasimamia watoe vibanda vyao.
 
Sheria inayoongoza masuala haya ilitungwa wakati gani? Ni nani walibuni sheria ile na nina walipitisha sheria hiyo itumike. Tuanzie kwenye kiini. Wenzetu Kenya sheria zao zipoje?
 
Sheria inayoongoza masuala haya ilitungwa wakati gani? Ni nani walibuni sheria ile na nina walipitisha sheria hiyo itumike. Tuanzie kwenye kiini cha tatizo
Mbona machinga nao mmewabomolea na kuharibu mali zao nini tofauti na kuchoma vifaranga?
Mlishindwa nini wasimamia watoe vibanda vyao.
Asante mkuu kwa maswali mazuri. Nasubiri mabijibu, ingawa johnthebaptist anasema vibanda siyo viumbe hai.
 
Praise team watakuwa wameinuka na kushangilia [emoji122] kana kwamba sio wao walioshangilia uchomaji wa vifaranga uliofanywa na wasaidizi wa bwana yule.
Hata Yeye Alisema kuwa ni kitu kimoja na Mwendazake[emoji1787][emoji1787][emoji1787] hakuona kama ni dhambi kipindi hiko akemee
 
pia mahindi ya Tanzania sumu yake iliondoka baada ya yeye kwenda Kenya
 
walikua wapi kuongea haya mambo, siwalitakiwa wamshauri mwendazake katika masuala kama haya? imagine wanachofanya sasa ni kinyume kabisaaaa na aliyekua kiongozi wao na malaika wao mkuu, ambaye ilifika kipindi akaitwa Yesu mwana wa Mungu aliye hai, wakaenda mbali zaidi wakamwita Mungu, hii dunia ina unafiki wa hali ya juu sana , yaani watu wale wale huwezi kuamini, kuna kina ndalichakoo , kuna kina dorotheeeeeee gwajifix yaani ni aibu sana , na bado wapo tu kwenye ma STK na bendera wanapeperusha kabisaaa mchana kweupe
 
Rais wa JMT mh Samia Suluhu Hassan amesifu ushirikiano wa nchi za Afrika mashariki na kusema tulikuwa tunachomeana kuku mipakani, dhambi tupu viumbe wa Mungu tunamwaga petrol kuwachoma haikuwa na maana.

Rais Samia amesema hayo katika kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda.

Source: Swahili times
Huyu mama inatakiwa awe na governor ya matamshi yake. Hayo yamefanywa na serikali aliyokuwa akiiongoza. Yeye kama makamu wa Rais alichukua hatua gani?

Anajifanya kumtupia Zigo MAREHEMU wakati mda wote wa uhai wa JPM amekuwa akisimama majukwaani akimsifia JPM. Ina maana alikuwa akimsifia kinafiki?

Wakenye siyo watu wa kuonea huruma. Ole wako ukamatwe na bidhaa ya Tanzania huko Kenya utajuta kuzaliwa. Sema wao wanatunyong'onyeza kimya kimya sisi tuna publish kwenye vyombo vya habari. Mkenya ni jilani mnafiki. Hivyo mama usijpendekeze kwake.

Kwa mda mrefu sana sisi tumekuwa soka lao la bidhaa za viwandani vyao. JPM kukata soko lao .hilo hawakufurahi. Kumbuka Duniani walikuwa ni wa pili kwa mauzo ya Tanzanite. Kwa sasa hawana hata kipande cha Tanzanite. Hiyo nayo iliwajengea chuki kwa nchi yetu.

MAMA TAFAKALI KABLA YA KUTAMKA. WEWE NI RAISI WA NCHI.
 
Back
Top Bottom