Nani mbishi ?? au huelewi kitu gani tunachosema??--- bidhaa yoyote yenye madhara au hatarishi ni lazima iangamizwe, sasa inaangamizwaje??!!, hapo ndipo mjadala ulipo, je viumbe hai wenye madhara nao waangamizwe kama sub standard goods from China??!!, wala haiingii akilini Kuua kwa kuchoma moto viumbe hai wenye madhara kama jinsi vipodozi vyenye madhara vinavyochomwa moto, kumbuka wewe ni kiumbe hai kama hao vifaranga, tofauti kati yako na kuku/kifaranga ni moja tu kwamba wewe unajitambua na yeye hajitambui lakini mambo mengine yote kimsingi mnafanana, na hata hao EU na Marekani huwa hawaangamizi kwa MOTO mifugo yenye madhara.
Sisi au mimi ninapinga kuangamiza viumbe hai kwa moto, itumike njia zingine Soft izilizopo na sio kuangamiza kwa MOTO kwani lengo la kuangamiza sio adhabu na mateso kwa hicho kiumbe bali ni sisi kujiepusha na madhara yatokanayo na hao viumbe.