Rais Samia hajaonekana kwenye Sherehe za Mei Mosi, yuko wapi?

Rais Samia hajaonekana kwenye Sherehe za Mei Mosi, yuko wapi?

Sio kila mwaka ahudhirie, kuna miaka hatakiwi kuhudhuria wafanyakazi wasimzoee sana. Atahudhuria mei mosi ijayo kama kutakuwa na jambo muhimu la kuzungumzia.
 
Mimi nilivyoona Hadi WADUDU ni wageni rasmi nilijua Tu hapa hakuna nyongeza ya mshahara
1713332931003.jpg

Mimi nilipoona futuhi mkuu anasherehesha nikajua hamna kitu
 
Hili ni tukio kubwa na yeye ndio muhusika mkuu na ndio mwajiri mkuu kama sikosei kwa watumishi wa umma.

Swali ni je, yuko wapi na anafanya nini au nini kimemsibu?

Lissu kapiga chini ya mkanda. Mama kaumia sana na ukweli aliosema Lissu kuhusu ubaguzi wa kikatiba wa Wabara ukilinganisha na Wanzanzibari. Mama anahitaji muda kufikiria vizuri badala ya kwenda kwenye mkutano na huzuni usoni. Pamoja na ukali wa maneno Lissu kasemea wengi kwenye huu muungano hasa kwa watu wa Arusha waliofukuzwa na kuhamishwa.
 
TUCTA pamoja ya kuwa ni Jumuiya Mojawapo ya chama kongwe dola CCM kama ilivyo UVCCM, WAZAZI n.k leo hawakupata ugeni mzito waliotarajia na kujitayarisha kwa siku kibao kumpokea
TOKA MAKTABA

SOLIDARITY FOREVER

Newsroom​

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI APRIL 2024

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI APRIL 2024


18 April 2024

Rais Samia mgeni rasmi Mei Mosi, kufanyika kitaifa Arusha​


View: https://m.youtube.com/watch?v=hQpvPpGFbYo
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Dunia (Mei Mosi) yatakayofanyika kitaifa mkoani Arusha.

Maadhimisho hayo yanatajwa pamoja na mambo mengine, kujadili masuala yanayohusu haki za wafanyakazi ikiwa ni pamoja kupinga ukiukwaji wa sheria na taratibu mahala pa kazi.


View attachment 2978103

Kikao cha Maandalizi ya Mei Mosi Arusha: Nyongeza ya Mishara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga dhidi ya hali ngumu ya maisha.​

WhatsApp-Image-2024-04-09-at-12.01.34_cd6dcbdd-1024x683.jpg

Arusha, Tanzania – Tarehe 6 Aprili, 2024, kikao muhimu kilifanyika Arusha huku wadau wakijiandaa kwa kikao cha maandalizi ya Mei Mosi.

Mkutano huu, uliofanyika kwa lugha ya Kiswahili, ulihamaisha na kauli mbiu isemayo: “Nyongeza ya mishahara ni msingi wa mafao bora na kinga dhidi ya hali ngumu ya maisha.”

Wawakilishi kutoka vyama vya wafanyakazi mbalimbali, maafisa wa serikali, na mashirika ya kiraia walikusanyika, wakianzisha jitihada za pamoja kabla ya Siku ya Wafanyakazi Duniani tarehe 1 Mei.

Majadiliano yenye msisimko yaligusa masuala muhimu kama haki za wafanyakazi, mishahara ya haki, na ulinzi wa kijamii.

Maafisa wa serikali walisisitiza umuhimu wa kuwatambua wafanyakazi kwa michango yao na kuelezea juhudi zilizopo za kuboresha mazingira ya kazi na kuchochea ukuaji wa kiuchumi unaowajumuisha wote.

Wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi walishirikisha ufahamu kutoka sekta mbalimbali, wakipendekeza mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili wafanyakazi. Majadiliano yao yalilenga katika kudai mazingira bora ya kazi, kukuza usawa wa kijinsia kazini, na kuboresha mipango ya maendeleo ya stadi.

Mashirika ya kiraia yalithibitisha ushirikiano wao kwa haki za wafanyakazi, wakiahidi kushirikiana na wadau katika kutatua masuala kama ajira ya watoto, ubaguzi, na upatikanaji wa huduma muhimu kama afya na elimu.

Mkutano ukifikia kikomo, hisia za umoja na azma zilionekana kila mahali, zikionyesha azma ya pamoja ya kujenga jamii yenye haki na usawa kwa wafanyakazi wote. Huku roho ya uwezeshaji ikiendelea kusikika Arusha, maandalizi ya sherehe za Mei Mosi yanaendelea, yakiongozwa na kauli mbiu ya pamoja inayothibitisha umuhimu wa nyongeza ya mishahara kama msingi wa kuhakikisha mafao bora na ulinzi dhidi ya changamoto za maisha.

TUCTA


TUCTA (soma historia zamani JUWATA ilivyojigeuza kuwa TUCTA www.tucta.or.tz ) pamoja ya kuwa ni Jumuiya Mojawapo ya chama kongwe dola CCM leo hawakupata ugeni mzito waliotarajia na kujitayarisha kwa siku kibao kumpokea
 
Uwanja wa Gombani Pemba.

SIKU YA WAFANYAKAZI / LABOUR DAY ZANZIBAR 2024

SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI ILIVYOADHIMISHWA PEMBA 2024


View: https://m.youtube.com/watch?v=zdeBODYgD6k

Rais Dkt. Hussein Mwinyi amezitaka taasisi mbili yaani Vyama vya Wafanyakazi na ile taasisi ya Waajiri kukutana mara nne kwa mwaka yaani kila robo mwaka ili ikifika Mei Mosi Siku ya Wafanyakazi Duniani / Labour Day kuwepo lugha moja ya walivyofanikiwa kuboresha mazingira ya wafanyakazi ....
 
Back
Top Bottom