Rais Samia hajaonekana kwenye Sherehe za Mei Mosi, yuko wapi?

Sio kila mwaka ahudhirie, kuna miaka hatakiwi kuhudhuria wafanyakazi wasimzoee sana. Atahudhuria mei mosi ijayo kama kutakuwa na jambo muhimu la kuzungumzia.
 
Ndugu zangu hivi hadi leo mnaamini hawa watu hushinda kwa kura?
Ni bora usijiumize moyo kwa matarajio hewa.
Kura hazipigwi,zinachukuliwa zinawekwa - waa
 
Hili ni tukio kubwa na yeye ndio muhusika mkuu na ndio mwajiri mkuu kama sikosei kwa watumishi wa umma.

Swali ni je, yuko wapi na anafanya nini au nini kimemsibu?

Lissu kapiga chini ya mkanda. Mama kaumia sana na ukweli aliosema Lissu kuhusu ubaguzi wa kikatiba wa Wabara ukilinganisha na Wanzanzibari. Mama anahitaji muda kufikiria vizuri badala ya kwenda kwenye mkutano na huzuni usoni. Pamoja na ukali wa maneno Lissu kasemea wengi kwenye huu muungano hasa kwa watu wa Arusha waliofukuzwa na kuhamishwa.
 
TUCTA pamoja ya kuwa ni Jumuiya Mojawapo ya chama kongwe dola CCM kama ilivyo UVCCM, WAZAZI n.k leo hawakupata ugeni mzito waliotarajia na kujitayarisha kwa siku kibao kumpokea

TUCTA (soma historia zamani JUWATA ilivyojigeuza kuwa TUCTA www.tucta.or.tz ) pamoja ya kuwa ni Jumuiya Mojawapo ya chama kongwe dola CCM leo hawakupata ugeni mzito waliotarajia na kujitayarisha kwa siku kibao kumpokea
 
Uwanja wa Gombani Pemba.

SIKU YA WAFANYAKAZI / LABOUR DAY ZANZIBAR 2024

SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI ILIVYOADHIMISHWA PEMBA 2024


View: https://m.youtube.com/watch?v=zdeBODYgD6k
Rais Dkt. Hussein Mwinyi amezitaka taasisi mbili yaani Vyama vya Wafanyakazi na ile taasisi ya Waajiri kukutana mara nne kwa mwaka yaani kila robo mwaka ili ikifika Mei Mosi Siku ya Wafanyakazi Duniani / Labour Day kuwepo lugha moja ya walivyofanikiwa kuboresha mazingira ya wafanyakazi ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…