Rais Samia: Hakuna anayependa Jeshi lake lichafuke. Nimewalinda ndio maana nimewabadilisha

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewataka wakuu wa mikoa walioteuliwa na kubadilishwa vituo vya kazi kwenda kujirekebisha na kuwatumikia wananchi ipasavyo. Akizungumza Septemba 2, 2026, katika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar, wakati akiwaapisha Wakuu wa Mikoa na Katibu Tawala wa Mkoa, Rais Samia amewakumbusha viongozi hao kuwa wao ndio "jeshi lake" na asingependa kuona jeshi lake likichafuka au kuharibu kazi nzuri iliyokwisha fanyika.

"Nilisema kuwa wakuu wa mikoa nyie ndio jeshi langu. Sasa hakuna anayependa jeshi lake lichafuke"-Amesema Rais Samia

Rais Samia amebainisha kuwa uamuzi wa kuwabadilisha vituo vya kazi badala ya kuwaondoa umelenga kuwalinda na kuwaondosha katika matatizo na tuhuma mbalimbali alizokuwa akipokea kutoka katika maeneo yao ya awali. Amesisitiza kuwa vituo vipya walivyopangiwa vinatoa fursa mpya ya kujirekebisha na kuacha tabia mbaya au kuingilia majukumu yasiyowahusu, ili wajikite kikamilifu katika kuwahudumia wananchi.

"Sasa kama ulikuwa unajijua unatabia mbaya au yoyote kule ulikotoka, kupya unakokwenda ni nafasi mpya kajirekebishe. Kajirekebishe tumikieni wananchi kama inavyotakiwa. Ni kuwasevu au kuwalinda, kuwahami na yale ambayo nimekuwa nikipokea. Kwa hiyo nenda kajirekebishe."-Amesema Rais Samia

Kuna RC Babu anakula na DED wa manispaa yake!
Matokeo huyo ded, anatukana na kumdharau kila aliyeko mbele yake!
 
Daah!

Nchi inapitia kipindi kigumu sana.

JK alikuwa dhaifu na Rais wa hovyo sana lakini hakuthubutu kuongea upuuzi kama huu.

Huyu mama sijui hata kama anaelewa matokeo ya anachokiongea.

"Kuleni kwa urefu wa kamba zenu msiingiliane"

"Mafisadi watajeni tuwazomee waone aibu"

"Nimewahamisha ili kuwalinda na mnayolalamikiwa"

Ni upuuuzi juu ya upuuzi.
 
Ni kwamba Katika Raia Million 60 usheee, hamna mtu wakufaa zaidi ya hao wanafanya maovu, wakatihumiwa , kwamba sasa anawabadili waendelee pengine, huko wakaanze Upya !!!.

Kwamba Ana guarantee hawatofanya yake waloyafanya.

Sisi kama Wananchi tunawaambia, NYOOSHENI NJIA ZENU, SIKU YAJA AMBAYO TUTAFUKUA MAKABURI HASWAA, ULIKUA DAS, RAS, DC, RC , KATIBU WIZARA, WAZIRI, RAIS .

Hamtalindwa na yeyote !!.
 
Back
Top Bottom