Rais Samia: Hakuna anayependa Jeshi lake lichafuke. Nimewalinda ndio maana nimewabadilisha

Daah!

Nchi inapitia kipindi kigumu sana.

JK alikuwa dhaifu na Rais wa hovyo sana lakini hakuthubutu kuongea upuuzi kama huu.

Huyu mama sijui hata kama anaelewa matokeo ya anachokiongea.

"Kuleni kwa urefu wa kamba zenu msiingiliane"

"Mafisadi watajeni tuwazomee waone aibu"

"Nimewahamisha ili kuwalinda na mnayolalamikiwa"

Ni upuuuzi juu ya upuuzi.

😂😂😂😂
 
Na ww si wamekuweka hapo ulipo. Kwa ufupi mnalipana.
Kazi ni kipimo cha utu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewataka wakuu wa mikoa walioteuliwa na kubadilishwa vituo vya kazi kwenda kujirekebisha na kuwatumikia wananchi ipasavyo. Akizungumza Septemba 2, 2026, katika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar, wakati akiwaapisha Wakuu wa Mikoa na Katibu Tawala wa Mkoa, Rais Samia amewakumbusha viongozi hao kuwa wao ndio "jeshi lake" na asingependa kuona jeshi lake likichafuka au kuharibu kazi nzuri iliyokwisha fanyika.

"Nilisema kuwa wakuu wa mikoa nyie ndio jeshi langu. Sasa hakuna anayependa jeshi lake lichafuke"-Amesema Rais Samia

Rais Samia amebainisha kuwa uamuzi wa kuwabadilisha vituo vya kazi badala ya kuwaondoa umelenga kuwalinda na kuwaondosha katika matatizo na tuhuma mbalimbali alizokuwa akipokea kutoka katika maeneo yao ya awali. Amesisitiza kuwa vituo vipya walivyopangiwa vinatoa fursa mpya ya kujirekebisha na kuacha tabia mbaya au kuingilia majukumu yasiyowahusu, ili wajikite kikamilifu katika kuwahudumia wananchi.

"Sasa kama ulikuwa unajijua unatabia mbaya au yoyote kule ulikotoka, kupya unakokwenda ni nafasi mpya kajirekebishe. Kajirekebishe tumikieni wananchi kama inavyotakiwa. Ni kuwasevu au kuwalinda, kuwahami na yale ambayo nimekuwa nikipokea. Kwa hiyo nenda kajirekebishe."-Amesema Rais Samia

Form IV alitaga huyu tusimlaumu sana tuwalaumu waliomuweka hapo
 
Hivi kwanini tunaongeza gharama za uendeshaji wa serikali?
Kuna Ikulu Dar, Dodoma na sasa Tunguu. Hawa wakuu wa mikoa ni wa Tanganyika, nani analipa gharama za usafiri na malazi kwenda Unguja! Na kwanini isiwe Dar au Dodoma ili kupunguza gharama kwa mlipa kodi

JokaKuu
Duh!..

Hizi Ikulu zipo kila mkoa ?
 
..hili suala ni la Tanganyika halikupaswa kufanyika Zanzibar.
Nadhani kuna namna ya kupeleka 'pesa' kwa kualika wageni ili Hoteli na huduma zinufaike
Hili suala la Tanganyika linafanyika Tunguu! Tuna Ikulu Dar na Dodoma

Viongozo wajali gharama zinazombebesha mlipa kodi mzigo mkubwa.
 
"Amesisitiza kuwa vituo vipya walivyopangiwa vinatoa fursa mpya ya kujirekebisha na kuacha tabia mbaya au kuingilia majukumu yasiyowahusu, ili wajikite kikamilifu katika kuwahudumia wananchi."

JE NI UJUMBE KWA RC wa DAR?
~ Cc : Albert Chalamila?
 
Watanzania, amkeni na kujiuliza maswali haya matatu !

1. Mkuu wa Mkoa ni Mwakilishi wa Rais kwenye mkoa husika! Kama Rais anatokana na Kura za wananchi, kwanini Mkuu wa Mkoa hatokani na kupigiwa kura na wananchi?

2. Mkuu wa Wilaya ni Mwakilishi wa Rais kwenye wilaya husika! Kama Rais anatokana na Kura za wananchi, kwanini Mkuu wa wilaya hatokani na kupigiwa kura na wananchi?

3. 1&2 Wote ni wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM ,Kwanini ni wajumbe wa vyama vya siasa na kwanini wajihusishe na siasa?,na hupeleka kwenye kikao hicho taarifa zipi? Tujiulize!

Bila Katiba,mpya ya kuondoa au kuboresha 1,2 & 3 hapo Juu,CCM itatawala milele kwa Mabavu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewataka wakuu wa mikoa walioteuliwa na kubadilishwa vituo vya kazi kwenda kujirekebisha na kuwatumikia wananchi ipasavyo. Akizungumza Septemba 2, 2026, katika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar, wakati akiwaapisha Wakuu wa Mikoa na Katibu Tawala wa Mkoa, Rais Samia amewakumbusha viongozi hao kuwa wao ndio "jeshi lake" na asingependa kuona jeshi lake likichafuka au kuharibu kazi nzuri iliyokwisha fanyika.

"Nilisema kuwa wakuu wa mikoa nyie ndio jeshi langu. Sasa hakuna anayependa jeshi lake lichafuke"-Amesema Rais Samia

Rais Samia amebainisha kuwa uamuzi wa kuwabadilisha vituo vya kazi badala ya kuwaondoa umelenga kuwalinda na kuwaondosha katika matatizo na tuhuma mbalimbali alizokuwa akipokea kutoka katika maeneo yao ya awali. Amesisitiza kuwa vituo vipya walivyopangiwa vinatoa fursa mpya ya kujirekebisha na kuacha tabia mbaya au kuingilia majukumu yasiyowahusu, ili wajikite kikamilifu katika kuwahudumia wananchi.

"Sasa kama ulikuwa unajijua unatabia mbaya au yoyote kule ulikotoka, kupya unakokwenda ni nafasi mpya kajirekebishe. Kajirekebishe tumikieni wananchi kama inavyotakiwa. Ni kuwasevu au kuwalinda, kuwahami na yale ambayo nimekuwa nikipokea. Kwa hiyo nenda kajirekebishe."-Amesema Rais Samia

Hivi Makongoro Bado yuko kwenye hilo jeshi...!?
 
Watanzania, amkeni na kujiuliza maswali haya matatu !

1. Mkuu wa Mkoa ni Mwakilishi wa Rais kwenye mkoa husika! Kama Rais anatokana na Kura za wananchi, kwanini Mkuu wa Mkoa hatokani na kupigiwa kura na wananchi?

2. Mkuu wa Wilaya ni Mwakilishi wa Rais kwenye wilaya husika! Kama Rais anatokana na Kura za wananchi, kwanini Mkuu wa wilaya hatokani na kupigiwa kura na wananchi?

3. 1&2 Wote ni wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM ,Kwanini ni wajumbe wa vyama vya siasa na kwanini wajihusishe na siasa?,na hupeleka kwenye kikao hicho taarifa zipi? Tujiulize!

Bila Katiba,mpya ya kuondoa au kuboresha 1,2 & 3 hapo Juu,CCM itatawala milele kwa Mabavu.

Ndiyo maana hata number 2 wake alituambia tupambambane tupate katiba mpya. Hii katiba ni ya Chama Kimeshika UTAMU.
 
Hakika huyo ni mama kweli kweli wana raha sana wanaofanya. Nae kazi kwa karibu
 
Back
Top Bottom