Rais Samia: Hakuna atakayeuza Tanzania. Sitaki Shida nataka Watanzania Waishi Maisha mazuri

Rais Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi pamoja na baadhi ya Wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) pamoja na Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

Akizungumza katika mkutano huo Rais Samia amekumbusha juu ya wajibu wa TLS na ZLS kusimamia utawala wa sheria kwa mujibu wa Katiba ya nchi kwa kuzingatia weledi na uadilifu huku akiwataka pia kumsaidia kusimamia misingi ya "R" nne katika kujenga umoja wa nchi na kuleta maendeleo

"Nimekuja na R zangu nne, sitaki shida nataka Watanzania waishi vizuri, nisaidieni huko. Kwa karne tuliyonayo hapa hakuna Mtanzania atakayeuza Tazania hii wala atakayegawa Tanzania hii, na sisi serikali, vyama vya siasa tukianza fukunyuku Wananchi watatusuta, nendeni kanisaidieni hizo R nne." Ameeleza Rais Samia

Chanzo: Clouds Media
Hao TLS walimwonyesha matobo ya mkataba, sasa kama hataki yazibwe ana lengo gani.
Kuna msemo unasema, the road to hell is paved by good intentions. Inawezekana ana nia njema, ila asikilize watu pia wanaomkosoa arekebishe. Akiishia sikiliza wapambe tu watampoteza
 
Rais Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi pamoja na baadhi ya Wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) pamoja na Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

Akizungumza katika mkutano huo Rais Samia amekumbusha juu ya wajibu wa TLS na ZLS kusimamia utawala wa sheria kwa mujibu wa Katiba ya nchi kwa kuzingatia weledi na uadilifu huku akiwataka pia kumsaidia kusimamia misingi ya "R" nne katika kujenga umoja wa nchi na kuleta maendeleo

"Nimekuja na R zangu nne, sitaki shida nataka Watanzania waishi vizuri, nisaidieni huko. Kwa karne tuliyonayo hapa hakuna Mtanzania atakayeuza Tazania hii wala atakayegawa Tanzania hii, na sisi serikali, vyama vya siasa tukianza fukunyuku Wananchi watatusuta, nendeni kanisaidieni hizo R nne." Ameeleza Rais Samia

Chanzo: Clouds Media
Huyu mama ni Delila wa kwenye bibilia.
 
Tuna wanasheria wa ajabu sana kuwahi kutokea katika nchi hii.
Hii TLS ni tawi la mawakili wa CCM.
Haiwezekani wakati kama huu ambao wanasheria na wanachama wenzao wa TLS wakifunguliwa kesi za bandia na hata kutishiwa maisha na serikali hiyo hiyo na kulazimika kuikimbia nchi...

Haya mengine yako pale yakienezewa ujinga huku wakikenua kuusaka ujaji na teuzi zingine.

Shame on them!
Unawapangia wenzako maisha? Mbona mjinga sana wewe?
 
Haya
 
Attachments

  • F36CA164-BADC-4A1E-B90D-D4EE98D9D166.jpeg
    F36CA164-BADC-4A1E-B90D-D4EE98D9D166.jpeg
    54.2 KB · Views: 3
Back
Top Bottom