Rais Samia: Hakuna atakayeuza Tanzania. Sitaki Shida nataka Watanzania Waishi Maisha mazuri

Rais Samia: Hakuna atakayeuza Tanzania. Sitaki Shida nataka Watanzania Waishi Maisha mazuri

Ujue kwa Africa ni mamiunguwatu. Tofauti sana na huko ulipo.
Hapa ndiyo kama hivyo bandari zinaenda kwa mikataba mibovu. Na wanaohoji wanapewa uhaini na kuwindwa kama ndege pori.

Kwani kwanini asione umuhimu wa ku review hivyo vinavyolalamikiwa ?!. Kwanini aone solution ni kuwapa watu uhaini !!.
Ndugu itabidi muwe wakimbizi kama sie tuliomkimbia Magufuli na alipoondoka tukambiwa nchi imetulia ameanza maridhiano wanasiasa wakaitwa lakini hakuna hata mwanasiasa mmoja aliesema kwenye maridhiano jamani kwani ndio sisi tu tuliokuwa wakimbizi??!!Wengine je wafanyabiashara vipi wawekezaji vipi na kadhalika.Hilo ndio tatizo la Tanzania kila mtu anapambana na matatizo yake huku ulaya ukiwa na shida atakaekusaidia ni mtu wa huku ulaya sio ubalozi wako wa Tanzania au Mtanzania mwenzako kwa hiyo ndio ukweli wa Watanzania pambaneni tu mkiungana labda mtafanikiwa
 
Mkataba tayari umeshatugawa., wapo wanaouona hauna tatizo, na wapo wanaouona unatatizo. Ndio maana wanaouona unatatizo tunataka tuwafungulie mashtaka ya Uhain kama aliyekuwa Rais wa Niger.
 
Rais Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi pamoja na baadhi ya Wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) pamoja na Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

Akizungumza katika mkutano huo Rais Samia amekumbusha juu ya wajibu wa TLS na ZLS kusimamia utawala wa sheria kwa mujibu wa Katiba ya nchi kwa kuzingatia weledi na uadilifu huku akiwataka pia kumsaidia kusimamia misingi ya "R" nne katika kujenga umoja wa nchi na kuleta maendeleo

"Nimekuja na R zangu nne, sitaki shida nataka Watanzania waishi vizuri, nisaidieni huko. Kwa karne tuliyonayo hapa hakuna Mtanzania atakayeuza Tazania hii wala atakayegawa Tanzania hii, na sisi serikali, vyama vya siasa tukianza fukunyuku Wananchi watatusuta, nendeni kanisaidieni hizo R nne." Ameeleza Rais Samia

Chanzo: Clouds Media
Bring it on mama
Sema mimi naimani haya yote yatakuwa sawa tu
 
Nadhani mama pengine hajausoma ule mkataba vizuri na akauelewa ama wanasheria aliowaamini sana wamempotosha ndio maana akaja na maneno kama hayo
Cha pili nadhani angevunja ukimya na kujitokeza kwenye presidential press conference aongee na taifa kwa mamlaka kama kiongozi mkuu, awape watu confidence na kuamrisha wanasheria kupitia upya mkataba (hata kwa kuzuga) tu ili at least a win public trust kwa muda
Kuwaendea TLS na kuwataka wamasaidie bado kunatengeneza ama kunazidi kutengeneza ombwe na hisia hasi kama kiongozi mkuu kati yake na wananchi wake

Kingine kibaya zaidi ni kuwakabidhi TLS hati ya kiwanja katika mazingira kama haya.. Hli halijajenga bali limezidi kuharibu.. Ni kama vile TLS wamefungwa mikono rasmi..!

Mama apunguze kuwaamini watu maana wameshamharibia vya kutosha sana sasa anahangaika pekeyake huku wao wakiwa nyuma ya pazia wanamcheka View attachment 2717731

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuuh hati ya kiwanja.., hapo nahis kawaziba kiaina. Na hautawasikia wakikosoa tena hiyo kitu watabaki wananong'ona pemben tu.
 
Rais Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi pamoja na baadhi ya Wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) pamoja na Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

Akizungumza katika mkutano huo Rais Samia amekumbusha juu ya wajibu wa TLS na ZLS kusimamia utawala wa sheria kwa mujibu wa Katiba ya nchi kwa kuzingatia weledi na uadilifu huku akiwataka pia kumsaidia kusimamia misingi ya "R" nne katika kujenga umoja wa nchi na kuleta maendeleo

"Nimekuja na R zangu nne, sitaki shida nataka Watanzania waishi vizuri, nisaidieni huko. Kwa karne tuliyonayo hapa hakuna Mtanzania atakayeuza Tazania hii wala atakayegawa Tanzania hii, na sisi serikali, vyama vya siasa tukianza fukunyuku Wananchi watatusuta, nendeni kanisaidieni hizo R nne." Ameeleza Rais Samia

Chanzo: Clouds Media
Maneno yake na matendo yake ni vitu viwili tofauti mnafiq mkubwa huyu yalimoyo kifuani mwake ni tofauti na ayatendayo!!....MwenyeziMungu atuondolee huu mkosi!!
 
Maneno yake na matendo yake ni vitu viwili tofauti mnafiq mkubwa huyu yalimoyo kifuani mwake ni tofauti na ayatendayo!!....MwenyeziMungu atuondolee huu mkosi!!
Magufuli alikuwa hivyo hivyo
 
Back
Top Bottom