Rais Samia: Hakuna atakayeuza Tanzania. Sitaki Shida nataka Watanzania Waishi Maisha mazuri

Rais Samia: Hakuna atakayeuza Tanzania. Sitaki Shida nataka Watanzania Waishi Maisha mazuri

Jibuni hoja hizi, sisi tunaangalia mkataba unasema nini, sio Rais anasema nini...

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Rais Samia, umefeli sana sana sana, unajiwekea record mbaya sana, dalili zinaonyesha kuwa ukombozi wa Tanzania na hasa Tanganyika utakuja chini ya utawala wako. Huwezi ukaanza kufunga watu na kuwabambikizia kesi ukabaki salama, haiwezekani labda Mungu hayupo.
 
Acha kuota wewe!! Ukombozi gani?
 
Rais Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi pamoja na baadhi ya Wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) pamoja na Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

Akizungumza katika mkutano huo Rais Samia amekumbusha juu ya wajibu wa TLS na ZLS kusimamia utawala wa sheria kwa mujibu wa Katiba ya nchi kwa kuzingatia weledi na uadilifu huku akiwataka pia kumsaidia kusimamia misingi ya "R" nne katika kujenga umoja wa nchi na kuleta maendeleo

"Nimekuja na R zangu nne, sitaki shida nataka Watanzania waishi vizuri, nisaidieni huko. Kwa karne tuliyonayo hapa hakuna Mtanzania atakayeuza Tazania hii wala atakayegawa Tanzania hii, na sisi serikali, vyama vya siasa tukianza fukunyuku Wananchi watatusuta, nendeni kanisaidieni hizo R nne." Ameeleza Rais Samia

Chanzo: Clouds Media
Madam president! Withdraw (ondoa) huo mkataba kabla ya utekelezaji! Huo mkataba haurekebishiki! Mkiwachekea DP WORLD wakaanza utekelezaji alafu mambo yakaanza kutubana itakuwa ngumu kujiondoa! Hatutaki huo mkataba!
 
Ajibu ule mkataba kifungu kwa kifungu. Au amwambie mwanasheria wake ajibu na siwabambikie watu wanaohoji mkataba kesi ya uhaini. Yeye ndiye mhaini na alitakiwa ashitakiwe yeye.
Mkataba umeshafafanuliwa kifungu kwa kifungu tena na Hamza Johari aliyeshiriki kuuandika akiwa na wanasheria wa Dubai.

Kusema Rais aufafanue wakati ufafanuzi ulishafanyika ni vurugu na ni ukosefu wa adabu wa kwa Rais.
 
Rais Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi pamoja na baadhi ya Wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) pamoja na Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

Akizungumza katika mkutano huo Rais Samia amekumbusha juu ya wajibu wa TLS na ZLS kusimamia utawala wa sheria kwa mujibu wa Katiba ya nchi kwa kuzingatia weledi na uadilifu huku akiwataka pia kumsaidia kusimamia misingi ya "R" nne katika kujenga umoja wa nchi na kuleta maendeleo

"Nimekuja na R zangu nne, sitaki shida nataka Watanzania waishi vizuri, nisaidieni huko. Kwa karne tuliyonayo hapa hakuna Mtanzania atakayeuza Tazania hii wala atakayegawa Tanzania hii, na sisi serikali, vyama vya siasa tukianza fukunyuku Wananchi watatusuta, nendeni kanisaidieni hizo R nne." Ameeleza Rais Samia

Chanzo: Clouds Media
Hivi Mama anafahamu kama Mkataba tunao?
 
The Commander in Chief has spoken!

JamiiForums934640752.jpeg
 
Back
Top Bottom