Rais Samia, hata siku moja mwekezaji habembelezwi kuja kuwekeza nchini, tafadhali zingatia yafuatayo watakuja wenyewe

Huwa naziona jitihada nyingi za raisi Samia kubembeleza wawekezaji kuja kuwekeza nchini, hadi namuonea huruma kwa sababu naelewa anapigia debe kitu ambacho sio rahisi kufanikiwa. Napenda kumwambia Raisi Samia kwamba wawekezaji hawavutwi au kushawishiwa kwenda kuwekeza kwenye nchi fulani, huwa ni nguvu ya soko (market forces) na mazingira ya uwekezaji katika uchumi huria vitakavyoamua kama wawekezaji watakuja au la.

Raisi Samia unaweza ukaenda Marekani na kwingineko hata kuwatumbuiza wawekezaji kwa taarabu ukipenda, lakini kama Tanzania haina conducive investment environment hawaji ng'o! Uwe unajiuliza, nini kitamfanya mwekezaji aje Tanzania badala ya kwenda nchi nyingine? Namna gani tunaifanya Tanzania kuwa na comparative advantage katika kuvutia wawekezaji? Kumbuka chema chajiuza, kibaya chajitembeza!

Sasa baadhi ya mambo wawekezaji wanayoangalia kuleta investment ni haya hapa, na kwa kweli nimejaribu kutaja karibu yote;
  1. Upatikanaji wa umeme wa uhakika
  2. Upatikanaji wa maji wa uhakika
  3. Soko la uhakika la kile wanachotaka kuwekeza (local na Tanzania as an exporter to regional markets)
  4. Sera za uwekezaji zilizo wazi (transparent) na zilizohakikishwa (policy certainty)
  5. Kutokuwepo ukiritimba (red-tape au bureaucracy)
  6. Urahisi wa kuishi Tanzania (residency permits)
  7. Kutokuwepo kwa rushwa (level of corruption in the country)
  8. Uaminifu na uchapakazi wa wafanyakazi (trustworthy and hardworking labor force, sio wadokozi ofisini laptop zikipotea hovyo nk)
  9. Urahisi wa kutoka na kuingia Tanzania (kupata visa, urahisi wa flights kuja nchini nk)
  10. Miundo mbinu ya barabara, airports, majengo ya ofisi nk
  11. Ubora na uhodari (efficiency) na cost za bandari katika kutoa huduma
  12. Kodi rafiki za TRA kwa wawekezaji ambazo zinajulikana kwa kanuni sio za kubambikiana
  13. Sheria za kazi zilizo rafiki (labour laws nchini)
  14. Sheria za utoaji faida (laws and regulations of repatriation of profits)
  15. Usalama katika nchi pamoja na kutokuwapo uhalifu
  16. Utulivu na amani katika siasa za ndani (CCM Vs vyama vya upinzani)
  17. Huduma za afya (matibabu)
  18. Mazingira stareheshe (uzuri wa hoteli na vivutio nk)
Sasa niambie Raisi Samia, kama ungetakiwa kutoa marks kwa kila kipengele hapo juu, ungetoa ngapi? Sasa ukifanyia kazi hayo juu, wala huhitaji kupiga vuvuzela kuita wawekezaji, watakuja wenyewe!

Mfano, ni miaka mingapi wawekezaji wanalia na usumbufu wa residency permits? Kwanza serikali haitoi hata kile kitu kinaitwa permanent residency kwa wawekezaji hata wale wakubwa hata waliooa Watanzania! Wanasumbuliwa sana na uhamiaji ku-renew permits.

Pili, Watanzania wanajulikana duniani kama wafanyakazi wavivu na wezi! Watu wanaisema nchi yetu vibaya sana katika udokozi ofisini nk. Watu wanaiba hadi stapple pins, sukari, vijiko vya chai vya ofisi! Bosi akisahau laptop mahali imekwenda! Wizi wa mitaani ndio usiseme. Wewe unajua ukiwa uarabuni huko ukasahau kufunga vioo vya gari, bado utaikuta laptop yako na simu kwenye gari, lakini sio hapa kwetu - kwanza wanavunja gari wakiona laptop kwenye gari.

Haya, upatikanaji wa umeme na maji je, ninahitaji kusema hapo kweli? Unamwambia mwekezaji aje kuja kukabiliana na matatizo ya umeme na maji nchi atakuja kufanya nini, kwa sababu anatupenda sana Watanzania au wewe raisi?

Kuna wawekezaji wamelalamika viongozi wa serikali hawapatikaniki, ni rahisi kufanya appointment na raisi wa USA kuliko waziri au katibu mkuu Tanzania. Kwa nini? Kwa nini hawa wateule wako wanajifanya miungu watu hard to get? Wawekezaji wanakuambia ilituchukua miezi sita kumwona waziri! Waambie watu wako hawa waache kujifanya miungu watu, wawe na open door policy katika kuhudumia watu, watanzania na wawekezaji.

Vipi urahisi wa kuja au kutoka Tanzania? Achana na sera za visa arrangement reciprocation, yamepitwa na wakati. Kama Marekani wanatusumbua kutupa visa, wewe waambie Wamarekani wakija watapata visa airport kirahisi kabisa. Scrap visa requirements kwa nchi ambazo zina potential za wafanyabiashara kuwekeza nchini. Ifanye Tanzania kuwa the easiest country to fly to, itasaidia kuleta wewekezaji na watalii. Mara nyingi watalii wanazalisha wawekezaji. Kumbuka hilo.

Halafu kumbuka huu ugomvi wenu CCM na vyama vya upinzani una athari kubwa sana katika kuvutia wawekezaji. Hawapendi kusikia sijui Mbowe kafunguliwa kesi za uhaini, Lissu kaomba hifadhi Ubelgiji - unahitaji kuwa concerned na hayo mambo, usieme hayakuhusu! Wawekezaji siku zote wanapenda strong political opposition kama check na control dhidi ya chama tawala, hawapendi upinzani dhaifu katika nchi wanazowekeza. Hivyo kuwa na upinzani ulio strong is a good thing for investments - waambie watu wako wa CCM pamoja na viongozi wako wa Bunge. Wasibeze hoja za upinzani Bungeni hasa zenye mshiko, wawekezaji wanasikia!

Una kitu kinaitwa Tanzania Investment Centre, hivi wanafanya kazi gani? Waulize katika hayo hapo juu wana mkakati wowote? Mara ngapi wamekuja kuku-consult kwamba Mheshimiwa raisi hili na hili vinatukwamisha tunaomba uingilie kati? Wapowapo tu wanasubiri mtu agonge hodi waanze kumsumbua badala ya kumsaidia. Wanahitaji kuwa pro-active, waendane na vision yako, sio wakae ofisini wasubiri wewe ukapige debe Marekani ili waje kugongewa hodi.
True badala yake atapata kwa mgonngo wa uwekezaji
 
  1. Upatikanaji wa umeme wa uhakika ......40-50%
  2. Upatikanaji wa maji wa uhakika................40-50%
  3. Soko la uhakika la kile wanachotaka kuwekeza (local na Tanzania as an exporter to regional markets)..80-100%
  4. Sera za uwekezaji zilizo wazi (transparent) na zilizohakikishwa (policy certainty).....50% kwatika makaratasi tu si utendaji
  5. Kutokuwepo ukiritimba (red-tape au bureaucracy).....red tape 90%
  6. Urahisi wa kuishi Tanzania (residency permits)......20%
  7. Kutokuwepo kwa rushwa (level of corruption in the country)....0% rushwa is the game of the day, kwa wengine is a means of income, hata kwa wanasiasa.
  8. Uaminifu na uchapakazi wa wafanyakazi (trustworthy and hardworking labor force, sio wadokozi ofisini laptop zikipotea hovyo nk).......60%(Mlimani Game experience)
  9. Urahisi wa kutoka na kuingia Tanzania (kupata visa, urahisi wa flights kuja nchini nk)...60%
  10. Miundo mbinu ya barabara, airports, majengo ya ofisi nk....70%
  11. Ubora na uhodari (efficiency) na cost za bandari katika kutoa huduma....60%
  12. Kodi rafiki za TRA kwa wawekezaji ambazo zinajulikana kwa kanuni sio za kubambikiana......30% worst experience
  13. Sheria za kazi zilizo rafiki (labour laws nchini).......60%
  14. Sheria za utoaji faida (laws and regulations of repatriation of profits).....50%
  15. Usalama katika nchi pamoja na kutokuwapo uhalifu.........70%
  16. Utulivu na amani katika siasa za ndani (CCM Vs vyama vya upinzani).......75%
  17. Huduma za afya (matibabu)...50%
  18. Mazingira stareheshe (uzuri wa hoteli na vivutio nk)...75%

Mzizi wa fitna upo katika mambo hayo yaliyotajwa, na marks ambazo mimi naona zinafaa kutolewa kwa huduma ya serikali.
Pamoja na maneno mengi ya kukaribisha uwekezaji, utendaji kiserikali katika eneo hilo ni sawa na hakuna.
Idara karibu zote za serikali hazijui zinafanya nini kuhusiana na uwekezaji.
Maafisa wanaweka vikwazo vingi ili kujinufaisha(rushwa).
Mimi ni mjasiria mali, ningetaja majina na vyeo vya maafisa wizara ya Ardhi, TIC, Uhamiaji na sehemu nyingi tu wanaofanya kazi ili kujinufaisha zaidi kuliko kukaribisha uwekezaji wa ndani na nje.
 
Wale wenye uwezo wa kuufikisha ujumbe huu kwa Samia, tafadhali mfikishieni. Anahitaji kuelewa haya mambo yanavyoenda
Umetoa mada yenye siha hasa.

Nami nitajitahidi kurudi hapa niisome tena, na pengine tena zaidi.

Pamoja na kuunga mkono mada yako, lakini ninahakika kuna upande mwingine ambao hukuugusia, na mara nyingi huwa hauguswi; hii dhana ya kudhani "Uwekezaji ndiyo mwarobaini wa maendeleo ya nchi", kiasi kwamba watu husahau hata kudadisi athari za kutegemea uwekezaji toka nje kuwa ndiyo dawa yetu ya kupata maendeleo.

Nisieleweke vibaya, sisemi uwekezaji ni mbaya na kwamba hautakiwi, la hasha; kwa maoni yangu uwekezaji ni muhimu katika kuunga na kuchochea juhudi zetu katika kutafuta maendeleo yetu.

Mengi ya hayo uliyoyataja kuwa mahitaji ya kuvuta wawekezaji kuja hapa, kiukweli yote hayo ni kwa manufaa yetu sisi wenyewe, kwa sababu yanatufaidisha kufanikisha juhudi zetu. Tukiwa na umeme wa kutosha na wenye kutegemewa, hivyo hivyo na maji, n.k., si ndiyo maendeleo hayo!

Sasa nisiandike gazeti, huku nikiwa nimeeleza kuwa nitarudi nisome kwa utulivu zaidi, mada hii muhimu kabisa, ili nipate kuchangia kwa uhakika.
 
Umeona basi hiyo Mkuu? Yaani tuna kazi kweli kweli!
 
Mzizi wa fitna upo katika mambo hayo yaliyotajwa, na marks ambazo mimi naona zinafaa kutolewa kwa huduma ya serikali.
Duh!

Mkuu 'Jidu'

Sijakusoma, lakini kwa kuangalia tu alama zilizomo kwenye haya uliyoweka hapa, bila shaka umetumia sayansi hasa kuchangia mada hii muhimu.
Kwa mwendo huu hii mada inaweza kuvunja rekodi ya uchangiaji wa umakini mkubwa, jambo ambalo linafurahisha sana.
Navutiwa sana kurudi, nikusome vizuri.
 
Huwa naziona jitihada nyingi za raisi Samia kubembeleza wawekezaji kuja kuwekeza nchini, hadi namuonea huruma kwa sababu naelewa anapigia debe kitu ambacho sio rahisi kufanikiwa. Napenda kumwambia Raisi Samia kwamba wawekezaji hawavutwi au kushawishiwa kwenda kuwekeza kwenye nchi fulani, huwa ni nguvu ya soko (market forces) na mazingira ya uwekezaji katika uchumi huria vitakavyoamua kama wawekezaji watakuja au la.

Raisi Samia unaweza ukaenda Marekani na kwingineko hata kuwatumbuiza wawekezaji kwa taarabu ukipenda, lakini kama Tanzania haina conducive investment environment hawaji ng'o! Uwe unajiuliza, nini kitamfanya mwekezaji aje Tanzania badala ya kwenda nchi nyingine? Namna gani tunaifanya Tanzania kuwa na comparative advantage katika kuvutia wawekezaji? Kumbuka chema chajiuza, kibaya chajitembeza!

Sasa baadhi ya mambo wawekezaji wanayoangalia kuleta investment ni haya hapa, na kwa kweli nimejaribu kutaja karibu yote;
  1. Upatikanaji wa umeme wa uhakika
  2. Upatikanaji wa maji wa uhakika
  3. Soko la uhakika la kile wanachotaka kuwekeza (local na Tanzania as an exporter to regional markets)
  4. Sera za uwekezaji zilizo wazi (transparent) na zilizohakikishwa (policy certainty)
  5. Kutokuwepo ukiritimba (red-tape au bureaucracy)
  6. Urahisi wa kuishi Tanzania (residency permits)
  7. Kutokuwepo kwa rushwa (level of corruption in the country)
  8. Uaminifu na uchapakazi wa wafanyakazi (trustworthy and hardworking labor force, sio wadokozi ofisini laptop zikipotea hovyo nk)
  9. Urahisi wa kutoka na kuingia Tanzania (kupata visa, urahisi wa flights kuja nchini nk)
  10. Miundo mbinu ya barabara, airports, majengo ya ofisi nk
  11. Ubora na uhodari (efficiency) na cost za bandari katika kutoa huduma
  12. Kodi rafiki za TRA kwa wawekezaji ambazo zinajulikana kwa kanuni sio za kubambikiana
  13. Sheria za kazi zilizo rafiki (labour laws nchini)
  14. Sheria za utoaji faida (laws and regulations of repatriation of profits)
  15. Usalama katika nchi pamoja na kutokuwapo uhalifu
  16. Utulivu na amani katika siasa za ndani (CCM Vs vyama vya upinzani)
  17. Huduma za afya (matibabu)
  18. Mazingira stareheshe (uzuri wa hoteli na vivutio nk)
Sasa niambie Raisi Samia, kama ungetakiwa kutoa marks kwa kila kipengele hapo juu, ungetoa ngapi? Sasa ukifanyia kazi hayo juu, wala huhitaji kupiga vuvuzela kuita wawekezaji, watakuja wenyewe!

Mfano, ni miaka mingapi wawekezaji wanalia na usumbufu wa residency permits? Kwanza serikali haitoi hata kile kitu kinaitwa permanent residency kwa wawekezaji hata wale wakubwa hata waliooa Watanzania! Wanasumbuliwa sana na uhamiaji ku-renew permits.

Pili, Watanzania wanajulikana duniani kama wafanyakazi wavivu na wezi! Watu wanaisema nchi yetu vibaya sana katika udokozi ofisini nk. Watu wanaiba hadi stapple pins, sukari, vijiko vya chai vya ofisi! Bosi akisahau laptop mahali imekwenda! Wizi wa mitaani ndio usiseme. Wewe unajua ukiwa uarabuni huko ukasahau kufunga vioo vya gari, bado utaikuta laptop yako na simu kwenye gari, lakini sio hapa kwetu - kwanza wanavunja gari wakiona laptop kwenye gari.

Haya, upatikanaji wa umeme na maji je, ninahitaji kusema hapo kweli? Unamwambia mwekezaji aje kuja kukabiliana na matatizo ya umeme na maji nchi atakuja kufanya nini, kwa sababu anatupenda sana Watanzania au wewe raisi?

Kuna wawekezaji wamelalamika viongozi wa serikali hawapatikaniki, ni rahisi kufanya appointment na raisi wa USA kuliko waziri au katibu mkuu Tanzania. Kwa nini? Kwa nini hawa wateule wako wanajifanya miungu watu hard to get? Wawekezaji wanakuambia ilituchukua miezi sita kumwona waziri! Waambie watu wako hawa waache kujifanya miungu watu, wawe na open door policy katika kuhudumia watu, watanzania na wawekezaji.

Vipi urahisi wa kuja au kutoka Tanzania? Achana na sera za visa arrangement reciprocation, yamepitwa na wakati. Kama Marekani wanatusumbua kutupa visa, wewe waambie Wamarekani wakija watapata visa airport kirahisi kabisa. Scrap visa requirements kwa nchi ambazo zina potential za wafanyabiashara kuwekeza nchini. Ifanye Tanzania kuwa the easiest country to fly to, itasaidia kuleta wewekezaji na watalii. Mara nyingi watalii wanazalisha wawekezaji. Kumbuka hilo.

Halafu kumbuka huu ugomvi wenu CCM na vyama vya upinzani una athari kubwa sana katika kuvutia wawekezaji. Hawapendi kusikia sijui Mbowe kafunguliwa kesi za uhaini, Lissu kaomba hifadhi Ubelgiji - unahitaji kuwa concerned na hayo mambo, usieme hayakuhusu! Wawekezaji siku zote wanapenda strong political opposition kama check na control dhidi ya chama tawala, hawapendi upinzani dhaifu katika nchi wanazowekeza. Hivyo kuwa na upinzani ulio strong is a good thing for investments - waambie watu wako wa CCM pamoja na viongozi wako wa Bunge. Wasibeze hoja za upinzani Bungeni hasa zenye mshiko, wawekezaji wanasikia!

Una kitu kinaitwa Tanzania Investment Centre, hivi wanafanya kazi gani? Waulize katika hayo hapo juu wana mkakati wowote? Mara ngapi wamekuja kuku-consult kwamba Mheshimiwa raisi hili na hili vinatukwamisha tunaomba uingilie kati? Wapowapo tu wanasubiri mtu agonge hodi waanze kumsumbua badala ya kumsaidia. Wanahitaji kuwa pro-active, waendane na vision yako, sio wakae ofisini wasubiri wewe ukapige debe Marekani ili waje kugongewa hodi.
Elimu nzuri sana, ila kabla haijafanyiwa kazi lazima waulize kwanza kuwa wewe ni chama gani
 
Umetoa mada yenye siha hasa.

Nami nitajitahidi kurudi hapa niisome tena, na pengine tena zaidi.

Pamoja na kuunga mkono mada yako, lakini ninahakika kuna upande mwingine ambao hukuugusia, na mara nyingi huwa hauguswi; hii dhana ya kudhani "Uwekezaji ndiyo mwarobaini wa maendeleo ya nchi", kiasi kwamba watu husahau hata kudadisi athari za kutegemea uwekezaji toka nje kuwa ndiyo dawa yetu ya kupata maendeleo.

Nisieleweke vibaya, sisemi uwekezaji ni mbaya na kwamba hautakiwi, la hasha; kwa maoni yangu uwekezaji ni muhimu katika kuunga na kuchochea juhudi zetu katika kutafuta maendeleo yetu.

Mengi ya hayo uliyoyataja kuwa mahitaji ya kuvuta wawekezaji kuja hapa, kiukweli yote hayo ni kwa manufaa yetu sisi wenyewe, kwa sababu yanatufaidisha kufanikisha juhudi zetu. Tukiwa na umeme wa kutosha na wenye kutegemewa, hivyo hivyo na maji, n.k., si ndiyo maendeleo hayo!

Sasa nisiandike gazeti, huku nikiwa nimeeleza kuwa nitarudi nisome kwa utulivu zaidi, mada hii muhimu kabisa, ili nipate kuchangia kwa uhakika.
Mkuu Kalamu, unaonyesha una uzalendo wa moyoni/

Labda pengine tume focus katika uwekezaji wa mitaji kutoka nje, na hatujasema ni nini kinakwamisha uwekezaji wa ndani. Lakini unachosema kwamba kusema uwekezaji ndio msingi wa maendeleo, hilo halipingiki, ila sasa labda tuseme tuna balance vipi kati ya uwekezaji wa nje na wa ndani. Kumbuka kwamba serikali katika uchumi wa leo, zinajiepusha kujihusisha na biashara, na hata Wachina wamechagua kufuata mwelekeo huu, ambao mwasisi wake alikuwa Margareth Thatcher.

Hivyo basi, kama tunataka uwekezaji wa ndani nao ukue, ni vipi tutawawezesha wawekezaji wa ndani? Kumbuka kuna siku Prof. Muhongo alsem hakuna mwekezaji wa ndani anaweza kuwekeza kwenye mafuta, wao wanaweza biashara za machungwa tu. Japo aliweka kauli amba ni extreme, alikuwa anaongea kweli.

Kwa sasa mwekezaji mkubwa wa ndani hapa kwetu bado ni serikali - katika barabaram ndege, uzalishaji umeme, nk. Fikria wa mfano Nyerere Hydro, nani mwekezaji wa ndani anaweza kubeba ule mradi?

Hata cement ambayo ina soko kubwa sana Tanzania, ilibidi aje Dangote.

Hivyo kwa sasa labda to focus kwenye wawekezaji wa nje
 
Ubarikiwe Mkuu.

Nashangaa Kuna lijamaa limoja la CCM humu, Kila siku linaandika machapisho ya kumsifia Samia.

Badala ya Kuandika vitu kama hivi
Huenda anataka uongozi maana kwa serikali ya sasa ukitaka cheo piga debe 4 nothing,
 
Mkuu Kalamu, unaonyesha una uzalendo wa moyoni/

Labda pengine tume focus katika uwekezaji wa mitaji kutoka nje, na hatujasema ni nini kinakwamisha uwekezaji wa ndani. Lakini unachosema kwamba kusema uwekezaji ndio msingi wa maendeleo, hilo halipingiki, ila sasa labda tuseme tuna balance vipi kati ya uwekezaji wa nje na wa ndani. Kumbuka kwamba serikali katika uchumi wa leo, zinajiepusha kujihusisha na biashara, na hata Wachina wamechagua kufuata mwelekeo huu, ambao mwasisi wake alikuwa Margareth Thatcher.

Hivyo basi, kama tunataka uwekezaji wa ndani nao ukue, ni vipi tutawawezesha wawekezaji wa ndani? Kumbuka kuna siku Prof. Muhongo alsem hakuna mwekezaji wa ndani anaweza kuwekeza kwenye mafuta, wao wanaweza biashara za machungwa tu. Japo aliweka kauli amba ni extreme, alikuwa anaongea kweli.

Kwa sasa mwekezaji mkubwa wa ndani hapa kwetu bado ni serikali - katika barabaram ndege, uzalishaji umeme, nk. Fikria wa mfano Nyerere Hydro, nani mwekezaji wa ndani anaweza kubeba ule mradi?

Hata cement ambayo ina soko kubwa sana Tanzania, ilibidi aje Dangote.

Hivyo kwa sasa labda to focus kwenye wawekezaji wa nje
Inawezekana kuna mkanganyiko katika niliyoeleza kwa harakaharaka hapo juu.
Sikuwa na maana ya "serikali kufanya biashara", kama wengi wanavyopenda kuliweka hilo kwa maksudi tu ya kuvuta hisia, lakini ni wazi kwamba kuna mambo ambayo ni lazima serikali iyafanye au iyasimamie, hili siyo jambo baya, na kutofanikiwa kama historia inaonyesha hivyo, hiyo haina maana hakuna lisiloweza kufanikiwa kwa serikali kulisimamia.

Sijasema, ni wazi kabisa, msisitizo wangu mkubwa ni uwekezaji wa ndani, wa waTanzania kuwezeshwa kufanya hivyo. Huu ndio msingi wa maendeleo wa nchi zote duniani. Hakuna nchi iliyopelekewa maendeleo toka nje.

Samia na viongozi wengine wanachokosea ni kudhani kwamba kazi yao kubwa ni kuvutia wawekezaji, toka nje, kumbe kazi yao kubwa ni kuhakikisha kwamba hao wanaokuja kuvuna hapa ni lazima kuvuna kwao pia kuwe kwa manufaa yetu wenyewe, siyo kwa vimishahara tu, bali unufaikaji wenye tija zaidi, kama kutuwezesha watu wetu kupata ujuzi na kujifunza mbinu zinazotumika katika nyanja hizo, ili hiyo kazi tuifanye wenyewe mbele ya safari.

Haitoshi kabisa kuvutia na kupata wawekezaji wengi toka nje, halafu ukajihesabu umefanikiwa, kama hukuweka mikakati madhubuti ya kunufaika na uwekezaji huo. Kunufaika, siyo sawa na kupata vimishahara tu kwa wafanyakazi, bila ya kuhakikisha kwamba thamani kubwa ya uwekezaji ni kukuza uwezo wetu.

Hiyo China uliyoitolea mfano, hawakufungua tu milango na madirisha ili takataka zote ziingie. Waliweka masharti, tena magumu sana, kiasi cha kwamba hata 'inteleectual property' za hayo makampuni yaliyolazimika kuingia yalijua hawana njia ya kuzuia kuchukuliwa kwa hizo 'intellectual property'.

Hapa kwetu Samia anahaha kutafuta wawekezaji, lakini hahahi kuhakikisha anaweka kinga madhubuti za kuzuia kuwa 'taken advantage of., na hao wawekezaji. Analegeza kila kitu, hata kuhakikisha tu kwamba baada ya miaka mitatu, watu wetu wae wamefundishwa kazi ili kushika nafasi za hao wageni!

Uwekezaji wa aina hiyo ni uwekezaji wa kipuuzi.

Msisitizo wangu: Juhudi za serikali yetu zielekezwe katika kujenga uwezo wa wananchi wetu kuwa wawekezaji katika nchi yetu. Hii ndiyo njia sahihi ya kujikwamua kimaendeleo.
Ndiyo, hao wanaokuja hapa kutoka nje wakaribishwe kwa mikono miwili, lakini lengo letu ni kuunga juhudi tunazofanya sisi wenyewe kuleta maendeleo yetu.
 
Hivi ni mwekezaji gani mjinga aneweza kuja kuwekeza kwenye nchi ambayo akilipa Kodi zote Halali Bado anakatwa Kodi ya wizi iitwayo tozo? Wazungu pesa yao inamahesabu labda awe mbumbumbu ndio anaweza kuja tanzania
 
Elimu nzuri sana, ila kabla haijafanyiwa kazi lazima waulize kwanza kuwa wewe ni chama gani
Ndio mambo ya kipuuzi haya yanatukwamisha sana. Upinzani wakisema hata jambo la maana sana, CCM wanazomea, CCM wakisema jambo la maana upinzani wanapinga. Sijui tunataka nini.
 
Huwa naziona jitihada nyingi za raisi Samia kubembeleza wawekezaji kuja kuwekeza nchini, hadi namuonea huruma kwa sababu naelewa anapigia debe kitu ambacho sio rahisi kufanikiwa. Napenda kumwambia Raisi Samia kwamba wawekezaji hawavutwi au kushawishiwa kwenda kuwekeza kwenye nchi fulani, huwa ni nguvu ya soko (market forces) na mazingira ya uwekezaji katika uchumi huria vitakavyoamua kama wawekezaji watakuja au la.

Raisi Samia unaweza ukaenda Marekani na kwingineko hata kuwatumbuiza wawekezaji kwa taarabu ukipenda, lakini kama Tanzania haina conducive investment environment hawaji ng'o! Uwe unajiuliza, nini kitamfanya mwekezaji aje Tanzania badala ya kwenda nchi nyingine? Namna gani tunaifanya Tanzania kuwa na comparative advantage katika kuvutia wawekezaji? Kumbuka chema chajiuza, kibaya chajitembeza!

Sasa baadhi ya mambo wawekezaji wanayoangalia kuleta investment ni haya hapa, na kwa kweli nimejaribu kutaja karibu yote;
  1. Upatikanaji wa umeme wa uhakika
  2. Upatikanaji wa maji wa uhakika
  3. Soko la uhakika la kile wanachotaka kuwekeza (local na Tanzania as an exporter to regional markets)
  4. Sera za uwekezaji zilizo wazi (policy transparency) na zilizohakikishwa (policy certainty)
  5. Kutokuwepo ukiritimba (red-tape au bureaucracy)
  6. Urahisi wa kuishi Tanzania (residency permits)
  7. Kutokuwepo kwa rushwa (level of corruption in the country)
  8. Uaminifu na uchapakazi wa wafanyakazi (trustworthy and hardworking labor force, sio wadokozi ofisini laptop zikipotea hovyo nk)
  9. Urahisi wa kutoka na kuingia Tanzania (kupata visa, urahisi wa flights kuja nchini nk)
  10. Miundo mbinu ya barabara, airports, majengo ya ofisi nk
  11. Ubora na uhodari (efficiency) na cost za bandari katika kutoa huduma
  12. Kodi rafiki za TRA kwa wawekezaji ambazo zinajulikana kwa kanuni sio za kubambikiana
  13. Sheria za kazi zilizo rafiki (labour laws nchini)
  14. Sheria za utoaji faida (laws and regulations for repatriation of profits)
  15. Usalama katika nchi pamoja na kutokuwapo uhalifu
  16. Utulivu na amani katika siasa za ndani (CCM Vs vyama vya upinzani)
  17. Huduma za afya (matibabu)
  18. Mazingira stareheshe (uzuri wa hoteli na vivutio nk)
Sasa niambie Raisi Samia, kama ungetakiwa kutoa marks kwa kila kipengele hapo juu, ungetoa ngapi? Sasa ukifanyia kazi hayo juu, wala huhitaji kupiga vuvuzela kuita wawekezaji, watakuja wenyewe!

Mfano, ni miaka mingapi wawekezaji wanalia na usumbufu wa residency permits hapa Tanania? Kwa nini hili halijaangaliwa? Kwanza serikali haitoi hata kile kitu kinaitwa permanent residency permit kwa wawekezaji hata wale wakubwa na waliooa Watanzania! Wanasumbuliwa sana na uhamiaji ku-renew permits.

Pili, Watanzania wanajulikana duniani kama wafanyakazi wavivu na wezi! Watu wanaisema nchi yetu vibaya sana katika udokozi ofisini nk. Watu wanaiba hadi stapple pins, sukari, vijiko vya chai vya ofisi! Bosi akisahau laptop mahali imekwenda! Wizi wa mitaani ndio usiseme. Wewe unajua ukiwa uarabuni huko ukasahau kufunga vioo vya gari, bado utaikuta laptop yako na simu kwenye gari, lakini sio hapa kwetu - kwanza wanavunja gari wakiona laptop kwenye gari.

Haya, upatikanaji wa umeme na maji je, ninahitaji kusema hapo kweli? Unamwambia mwekezaji aje kuja kukabiliana na matatizo ya umeme na maji nchi atakuja kufanya nini, kwa sababu anatupenda sana Watanzania au wewe raisi?

Kuna wawekezaji wamelalamika viongozi wa serikali hawapatikaniki, ni rahisi kufanya appointment na kukutana na raisi wa USA kuliko waziri au katibu mkuu Tanzania. Kwa nini? Kwa nini hawa wateule wako wanajifanya miungu watu hard to get? Wawekezaji wanakuambia ilituchukua miezi sita kumwona waziri! Waambie watu wako hawa waache kujifanya miungu watu, wawe na open door policy katika kuhudumia watu, watanzania na wawekezaji.

Vipi urahisi wa kuja au kutoka Tanzania? Achana na sera za visa arrangement reciprocation, yamepitwa na wakati. Kama Marekani wanatusumbua kutupa visa, wewe waambie Wamarekani wakija watapata visa airport kirahisi kabisa. Scrap visa requirements kwa nchi ambazo zina potential za wafanyabiashara kuwekeza nchini. Ifanye Tanzania kuwa the easiest country to fly to, itasaidia kuleta wewekezaji na watalii. Mara nyingi watalii wanazalisha wawekezaji. Kumbuka hilo.

Halafu kumbuka huu ugomvi wenu CCM na vyama vya upinzani una athari kubwa sana katika kuvutia wawekezaji. Hawapendi kusikia sijui Mbowe kafunguliwa kesi za uhaini, Lissu kaomba hifadhi Ubelgiji - unahitaji kuwa concerned na hayo mambo, usiseme hayakuhusu! Wawekezaji siku zote wanapenda strong political opposition kama check na control dhidi ya chama tawala, hawapendi upinzani dhaifu katika nchi wanazowekeza. Hivyo kuwa na upinzani ulio strong is a good thing for investments - waambie watu wako wa CCM pamoja na viongozi wako wa Bunge. Wasibeze hoja za upinzani Bungeni hasa zenye mshiko, wawekezaji wanasikia!

Una kitu kinaitwa Tanzania Investment Centre, hivi wanafanya kazi gani? Waulize katika hayo hapo juu wana mkakati wowote? Mara ngapi wamekuja kuku-consult kwamba Mheshimiwa raisi hili na hili vinatukwamisha tunaomba uingilie kati? Wapowapo tu wanasubiri mtu agonge hodi waanze kumsumbua badala ya kumsaidia. Wanahitaji kuwa pro-active, waendane na vision yako, sio wakae ofisini wasubiri wewe ukapige debe Marekani ili waje kugongewa hodi.
Yaani naombea kama huyu SSH angepitia hii post au mtu mwenye access nae amtumie link maana hawa jamaa wa kijani wanatumia nguvu kama greda badala ya ku operate kiakili. Enough kusema ni kikao cha familia kimejazana bungeni
 
Hivi ni mwekezaji gani mjinga aneweza kuja kuwekeza kwenye nchi ambayo akilipa Kodi zote Halali Bado anakatwa Kodi ya wizi iitwayo tozo? Wazungu pesa yao inamahesabu labda awe mbumbumbu ndio anaweza kuja tanzania
Uwekezaji wa nje ukikomaa hata hizi tozo za kubambikiana zinaondoka tu. Suala zima la kuweka tozo ni kwa sababu Tanzania haina wigo mpana wa kukusanya kodi (tax base) na hivyo serikali inakuwa tayari kufanya dhambi ya kutoza watu kodi mara mbili kwa kitu au huduma ileile.

Katika nchi makini, hili lingeenda hadi constitutional court. Huwezi ukatoza kodi mara mbili kwa kuficha neno kodi katika jina jingine na kudai hiyo sio kodi ni tozo.
 
Ndio mambo ya kipuuzi haya yanatukwamisha sana. Upinzani wakisema hata jambo la maana sana, CCM wanazomea, CCM wakisema jambo la maana upinzani wanapinga. Sijui tunataka nini.
Nakumbk hata aliyekuw MP wa Arusha mjini mhe Lema aliwah sema ushabiki ktk mambo ya msingi ndio kikwazo cha maendeleo nchini,. Yaani tunashindana kama timu za mpira
 
Sawa, "Fungua Nchi", kama unaona nchi ilifungwa.
Lakini hakikisha unapofanya hivyo umeimarisha sehemu zote za kufaidika na ufunguzi huo, siyo kuachia tu na kulegea.

Wakati wawekezaji wanapokuja hapa, unashindwa kujadiliana nao na kuelewana jinsi utakavyonufaika na uwekezaji wao, unawaachia mianya ya kukugonga katika mikataba, halafu wewe unachekelea umepata uwekezaji!
 
Ku'focus' kwa wananchi wetu kunazuiaje kuja kwa akina Angote, labda hilo ndilo swali tunalotaka ufafanuzi juu yake.
Hakuizuii mkuu, ila kunawawezesha kiasi kwamba kina Dangote wanaweza kukuta hawahitaji kuja. Kumbuka, kiwanda cha Dangote kikiwa cha mzawa kuna faida kwamba mzawa hatahitaji ku-repatriate profi (yaani kutoa fedha faida ya kiwanda kwenda nje), bali anakuwa na nafasi kubwa na motivation ya ku-diversify kwenda investment nyingine ndani ya nchi badala ya kupeleka capital kwenda kwao

Sasa suala kubwa ni kwamba, ili Dangote iwe ya Mtanzania badala ya Mnigeria, utamsaidiaje huyu Mtanzania?

Zenawi wa Ethiopia alijaribu, lakini hakuwa makini, kwa sababu jitihada yake ya ku-support investors wa ndani ilisababisha inflation kubwa sana. Ni kama vile useme Nitatoa bilioni 2 za Tanzania kwa watanzania efu mja waanzishe maduka. Matokeo ni kwamba hela ya ndani inakuwa nyingi sana kwenye mzunguko, na nyanya zinapanda bei hadi kufikia shs elfu tano nyanya moja.

Lakini Dangote akija, anakuja na foreign capital ambayo sanasana itafanya shilingi ndio iadimike, kwa sababu inabidi abadilishe dola zake kuwa shilingi ili alipe wafanyakazi, na demand ya shilingi inakuwa kubwa, wakati dollar ipo nje nje inaletwa na kina Dangate. Lakini bado itabdidi uwe makini, maana Dangote akitaka kutoa faida itabidi umpe dola, hawezi kutoa shilingi kwenda Nigeria
 
Back
Top Bottom